Menu

Fiqhi


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


NAMNA YA KUTAYAMAMU.

1. Aupige mchanga kwa mikono yake pigo moja.

2. Kisha aipulize kupunguza vumbi.

3. Kisha apanguse uso wake kwa hiyo mikono mara moja.

4. Kisha apanguse upande wa nje wa wa vitanga vya mikono. Apanguse sehemu ya nje ya kitanga cha mkono wa kulia kwa sehemu ya ndani ya kitanga cha mkono wa kushoto, kisha nje ya kitanga cha mkono wa kushoto kwa sehemu ya

Na dalili ya namna ya kutayamamu ni hadithi ya Ammar Radhi za Allah ziwe juu yake

 

أن النَّبِيَّ ﷺ ضَرَبَ بِكَفَّيْهِ الْأَرْضَ، وَنَفَخَ فِيهِمَا، ثُمَّ مَسَحَ بِهِمَا وَجْهَهُ وَكَفَّيْهِ]     متفق عليه]

 

[Kwamba Mtume ﷺ alipiga ardhi kwa vitanga vyake viwili vya mkono, akavipuliza kisha akapangusa uso wake na vitanga vyake kwavyo]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

FARADHI ZA KUTAYAMAMU.

1. Kutia nia.

2. Kupangusa uso.

3. Kupangusa vitanga vya mikono.

4. Kufuatanisha: aanze kupangusa uso kisha vitanga viwili vya mikono.

5. Kufuliliza: Apanguse mikono miwili baada ya kupangusa uso papo kwa papo.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. YANAPOKOSEKANA MAJI

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

 

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا}     المائدة:6}

 

[Na mkitopata maji tayamamuni]   [5: 6].

Na mtu haambiwi kuwa amekosa maji iwapo hakuyatafuta.

2. KUSHINDWA KUYATUMIA MAJI
Kama mgonjwa au mkongwe asiyeweza kutembea, na akawa hana wa kumsaidia kutawadha.

3. WAKATI WA KUCHELEA MADHARA KWA KUTUMIA MAJI
Miongoni mwa hayo:

a) Mgonjwa ambaye angeyatumia maji ugonjwa wake utazidi.

b) Mtu aliye mahali penye baridi kali na asiwe na kitu cha kupasha maji moto na akawa na yakini lau ataoga atapatikana na ugonjwa.

Hii ni kwa hadithi iliyothubutu kuwa Mtume   alimkubalia ‘Amr bin al-’Asw alipowaswalisha wenzake hali akiwa ametayamamu kwa sababu ya baridi kali   [Imepokewa na Abu Daud.].

c) Awapo mahali mbali na hana maji isipokuwa kidogo ambayo anayahitajia kwa kunywa na hawezi kuleta mengine.



SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Yanayoharamishwa kwa ajili ya hedhi na nifasi

1. KUJAMIANA 

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ}     البقرة:222}

[Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi.wala msiwaingilie mpaka watahirike. Wakisha twahirika basi waendeni alivyo kuamrisheni mwenyezi mugnu.]    [2: 222]

Na kwa kauli ya Mtume ilipoteremka aya hii:

 

اصنعوا كل شيء إلا النكاح]       رواه مسلم] 

 

[Fanyeni kila kitu isipokuwa kuundama]   [Imepokewa na Muslim.].

MAELEZO 
1. Mwenye kumuingilia mkewe na hali yuko katika hedhi hupata dhambi na itamlazimu kafara na huyo mke pia atoe kafara iwapo aliridhia.

Na kafara ni kutoa sadaka kadiri ya dinari moja au nusu dinari ya dhahabu, kwa hadithi ya Ibnu Abbas kumpokea Mtume juu ya mtu anayemuingilia mkewe na hali yuko kwenye hedhi kuwa alisema:

 

يتصدق بدينار أو بنصف دينار]    رواه أبوداد والنسائي]

 

[Atatoa sadaka Dinari moja au nusu dinari]     [Imepokewa na Abuu Dawud na Annisaai.].

Dinari moja ni grama nne na robo za dhahabu.

2. Aliyoko hedhini akiingia twaharani, haifai kwa mumewe kumuundama (kumuingilia) mpaka aoge, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

 

وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ}      البقرة:222}

 

[Wala msiwaingilie mpaka watahirike. (kutokana na damu) 

[Wakisha twahirika]  (yaani: wakaoga.) 

[basi waendeni alivyo kuamrisheni mwenyezi mugnu.]     yaani: kuundama.    [2: 222] 

2. KUSWALI 

Kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

فإذا أقبلت الحيضة فاتركي الصلاة . فإذا ذهب قدرها ، فاغسلي الدم عنك وصلي]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Ikija hedhi yako acha kuswali, na ikiondoka Mda wake basi Jisafishe damu kisha uswali]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

 

MAELEZO 

1. Mwanamke haimlazimu kulipa swala akitwahirika, Kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa aliulizwa juu ya aliyekuwa na hedhi kulipa Saumu na kutolipa Swala, akasema:

 

كنا نحيض عند رسول الله صلى الله عليه وسلم فيأمرنا بقضاء الصيام ولا يأمرنا بقضاء الصلاة]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Tulikuwa tukipatwa na Hedhi wakati tukiwa na Mtume  ﷺ  akituamrisha kulipa saumu na wala hakutuamrisha kulipa Swala]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Iwapo mwenye hedhi atawahi rakaa nzima ya wakati wa Swala, itamlazimu aswali, iwe ni rakaa ya mwanzo ya wakati au ya mwisho wake. Ikiwa atawahi sehemu ya wakati ambayo haikundukii rakaa moja, basi haimlazimu kuswali, kwa kauli ya Mtume :

 

مَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنْ الصَّلَاةِ فَقَدْ أَدْرَكَ الصَّلَاةَ]      رواه البخاري ومسلم]

 

[Mwenye kuwahi rakaa moja ya Swala amewahi Swala]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

3. KUFUNGA SAUMU 

Kwa kauli yake Mtume :

[Kwani akiingia katika hedhi si ataacha kuswali na kufunga? Wakasema (wanawake): “Ndiyo”]    [Imepokewa na Bukhari.].

 

MAELEZO
Akitwahirika mwenye hedhi kabla ya Alfajiri na akafunga, basi Saumu yake itakuwa sahihi, ingawa hakuoga mpaka baada ya Alfajiri

4. KUSHIKA MSAHAFU

Kwaneno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ}     الواقعة:79}

 

[Hawaigusi isipokuwa walitwahirishwa]   [56: 79]

Na kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

لا يمس القرآن إلا طاهر]     رواه مالك في الموطأ]

 

[Hagusi Qur'ani ila aliye twahara]    [Imepokewa na Malik katika Muwatta’]

5. KUTUFU AL KAABA 
Kwa neno la Mtume kumwambia Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake

 

افعَلي ما يفعَلُ الحاجُّ، غير ألَّا تطوفي بالبيتِ حتى تطهُرِي]    متفق عليه]

 

[Fanya kile anachokifanya mwenye kuhiji isipokuwa usitufu Alkaaba mpaka uwe twahara]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na Asema Ibn ‘Abbas Radhi za Allah za Allah ziwe juu yake :

 

أُمر الناس أن يكون آخر عهدهم بالبيت، إلا أن أنه خفف عن المرأة الحائض]      رواه البخاري ومسلم]

 

[Wameamrishwa watu iwe mwisho wa kukutana kwao na Alkaaba ni kutufu, isipokuwa mwanamke mwenye hedhi amehafifishiwa hilo]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

6. KUKAA MSIKITINI ISIPOKUWA KWA MPITA NJIA.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا}  النساء:43}

 

[Enyi mlioamini! Msikaribie swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge]   [4: 43]

na kwa neno la Mtume :

 

لا أحل المسجد لحائض ولا لجنب]    رواه أبوداود بسند ضيف]

 

[Mimi simhalalishii msikiti mwenye hedhi wala mwenye janaba]       [imepokewa na Abuu Daud kwa Isnadi dhaifu]

MAELEZO

1. Si makosa kwa mwenye hedhi kupita msikitini akijihifadhi na asichelee kuuchafua msikiti, kwa ujumla wa maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyetuka: {Isipokuwa wapita njia} [4: 43]

2. Ni haramu kwa mwenye hedhi kukaa kwenye eneo la kuswalia Idi, kwa neno lake Mtume :

 

وَيَعْتَزِلُ الحُيَّضُ المُصَلَّى]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Na wajiepushe na kuhudhuria mahali pa kuswali Idi]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

7.TALAKA
Ni haramu kwa mume kumuacha mkewe akiwa na hedhi, kwa neno lake mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ}    الطلاق:1}

 

[Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda]  [65: 1].

Yaani waelekee kwenye eda maalumu wakati wa kuachwa.

Na talaka ya mwenye hedhi inapita ingawa ni haramu na ni uzushi katika Dini.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


MAANA YA KUTAYAMAMU 
Kutayamamu kilugha: Ni Kukikusudia kitu na kukielekea
Ama Maana yake kisheria: Ni Kupukusa uso na viganja vya mikono miwili kwa ardhi Twahara kwa nia ya kujitwahirisha

HUKMU YA KUTAYAMAMU
Inapasa kutayamamu yakikosekana maji au ikawa haiwezikani kuyatumia kwa jambo linalolazimu utwahara kama vile Swala. na kutayamamu kunapendekezwa katika kufanya jambo linalopendekezwa kama vile kusoma Qur'ani.

DALILI ZA KUTAYAMAMU 

Kutayamamu kumethibiti katika Qur-ani Tukufu, Sunna na Ijmaa ya Wanachuoni.

Dalili ya Kutayamamu katika Qur'ani.

1. Mwenyezi Mungu  Anasema:

 

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ}     النساء:43}

 

[Mkitopata maji kusudieni ardhi nzuri, mpanguse nyuso zenu na mikono yenu ]    [4:43]

Ama Dalili yake katika Sunna.

2. Amesema Mtume :

 

أعطيت خمسا ، لم يعطهن أحد من الأنبياء قبلي : نصرت بالرعب مسيرة شهر ، وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا ، فأيما رجل من أمتي أدركته الصلاة فليصل     رواه البخاري

 

[Nimepewa mambo matano hakuna aliyepewa kabla yangu: Nimenusuriwa kwa kitisho masafa ya mwezi, nimefanyiwa ardhi kuwa ni mahali pa kuswali na pa kujitwahirishia: kwani yoyote katika umma wangu atakayeingiliwa na kipindi cha Swala na aswali]             [Imepokewa na Bukhari.].

Ama Ijmaa, wanazuoni wote wamekogomana na kukubaliana kuwa tayamamu imefanywa kuwa ni sheria, itumike badala ya ya udhu na josho katika hali na mazingira maalum yaliyobainishwa na sheria.

HEKIMA YA SHERIA KUWEKA KUTAYAMAMU

1. Kuwasahilishia umma wa Mtume Muhammad

2. Kuepusha madhara yanayosababishwa na utumiaji maji katika hali ya ugonjwa, na baridi kali na mfano wa hayo.

3. Kudumisha mafungamano ya ibada yasikatike kwa kukosekana maji, au kutoweza kuyatumia



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi 


MAELEZO 

1. Iwapo mwanamke anajua wakati wa hedhi yake, lakini akawa amesahau idadi ya siku zake za hedhi, basi atashika hesabu ya ada wanawake wengi.

2. Iwapo mwanamke anajua idadi ya siku zake za hedhi, lakini akawa amesahau wakati wa hedhi yake, iwapo ni mwanzo wa Mwezi au ni mwisho wake, atahesabu mwanzo wa Mwezi idadi ya siku zake za Hedhi. Akisema kuwa yamjia mwanzo wa Mwezi lakini hawezi kujuwa ni lini wakati wake, atashika hesabu kuanzia mwanzo wa nusu idadi ya siku ilipokuwa Hedhi yake ikimjia, kwa kuwa nusu ya mwezi ndio kadiri iliyo karibu zaidi ya kudhibiti wakati wake.

3. Kikipita kipindi cha hedhi, na mwanamke yuko kwenye istihadha basi ataoga kisha atafunga kitambaa kwenye tupu yake. Na hukumu yake itakuwa ni ile ya Twahara, ataswali na atafunga, na haitamdhuru Damu itakayomtoka baada ya kutawadha kwa kuwa ana udhuru, na atafanya mojawapo ya mambo matatu katika Twahara:

A) Atawadhe kwa kila Swala baada ya wakati kuingia. Hilo ni baada ya kuosha tupu yake na kuifunga kitambaa, kwa kauli ya Mtume ﷺ kumwambia Fatimah binti Hubaish Radhi za Allah ziwe juu yake :

 

ثم توضئي لكل صلاة]      رواه البخاري]

 

[Kisha tawadha kwa kila Swala na uswali]   [Imepokewa na Bukhari.].

B). Aicheleweshe Adhuhuri mpaka kabla ya Alasiri, kisha aoge na aswali Adhuhuri na Alasiri, na atafanya hivi katika Swala nyingine. Hii ni kwa neno lake Mtume kumwambia Hamnah binti Jahsh Radhi za Allah ziwe juu yake:

 

فَإِنْ قَوِيتِ عَلَى أَنْ تُؤَخِّرِي الظُّهْرَ وَتُعَجِّلِي العَصْرَ، ثُمَّ تَغْتَسِلِينَ حِينَ تَطْهُرِينَ، وَتُصَلِّينَ الظُّهْرَ وَالعَصْرَ جَمِيعًا، ثُمَّ تُؤَخِّرِينَ المَغْرِبَ، وَتُعَجِّلِينَ العِشَاءَ، ثُمَّ تَغْتَسِلِينَ، وَتَجْمَعِينَ بَيْنَ الصَّلَاتَيْنِ، فَافْعَلِي، وَتَغْتَسِلِينَ مَعَ الصُّبْحِ وَتُصَلِّينَ، وَكَذَلِكِ فَافْعَلِي، وَصُومِي إِنْ قَوِيتِ عَلَى ذَلِكَ    رواه إبن ماجة

 

[Na ukiweza kuchelewesha Adhuhuri na kuitanguliza Alasiri, kisha ukaoga unapo twahirika na ukakusanya baina ya Swala (mbili) Adhuhuri na Alasiri, kisha ukachelewesha Swala ya Magharibi na akaitanguliza Swala ya Isha, kisha uoge, na ukusanye Swala mbili, basi fanya hivyo. Na ukauoga wakati wa wa swala ya Alfajiri na ukswali basi fanya hivyo, na ufunge, kama waeza kufunga]   [Imepokewa na Ibnu Maajah.].

4. Mwanamke akitokwa na damu kwa sababu yoyote ile, kama operesheni, na ikatiririka, basi yeye ni mojawapo wa hali mbili:

Hali ya Kwanza: Ijulikane kuwa hatapata hedhi. Huyu hazipitishwi kwake hukumu za istihadhah, wala haachi kuswali wakati wowote, na ile damu ni ya ugonjwa na kuharibika kwa kitu, na atatawadha kwa kila Swala.

Hali ya Pili: Ijulikane kuwa yeye inamkinika kuingia hedhini. Huyu hukumu yake ni ya istihadhah.

5. Inafaa kumuingilia mwanamke aliye kwenye istihadhah.kwa kuwa Sheria haikumkataza.


Subcategories

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668580
TodayToday1268
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 20

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6867104ebca9913575685191751584846
title_6867104ebcba48779209881751584846
title_6867104ebcc9c1299173701751584846

NISHATI ZA OFISI

title_6867104ebea4a4797999641751584846
title_6867104ebeb3317429840401751584846
title_6867104ebec1513869341121751584846 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com