SOMO LA FIQHI
MAELEZO
1. Iwapo mwanamke anajua wakati wa hedhi yake, lakini akawa amesahau idadi ya siku zake za hedhi, basi atashika hesabu ya ada wanawake wengi.
2. Iwapo mwanamke anajua idadi ya siku zake za hedhi, lakini akawa amesahau wakati wa hedhi yake, iwapo ni mwanzo wa Mwezi au ni mwisho wake, atahesabu mwanzo wa Mwezi idadi ya siku zake za Hedhi. Akisema kuwa yamjia mwanzo wa Mwezi lakini hawezi kujuwa ni lini wakati wake, atashika hesabu kuanzia mwanzo wa nusu idadi ya siku ilipokuwa Hedhi yake ikimjia, kwa kuwa nusu ya mwezi ndio kadiri iliyo karibu zaidi ya kudhibiti wakati wake.
3. Kikipita kipindi cha hedhi, na mwanamke yuko kwenye istihadha basi ataoga kisha atafunga kitambaa kwenye tupu yake. Na hukumu yake itakuwa ni ile ya Twahara, ataswali na atafunga, na haitamdhuru Damu itakayomtoka baada ya kutawadha kwa kuwa ana udhuru, na atafanya mojawapo ya mambo matatu katika Twahara:
A) Atawadhe kwa kila Swala baada ya wakati kuingia. Hilo ni baada ya kuosha tupu yake na kuifunga kitambaa, kwa kauli ya Mtume ﷺ kumwambia Fatimah binti Hubaish Radhi za Allah ziwe juu yake :
ثم توضئي لكل صلاة] رواه البخاري]
[Kisha tawadha kwa kila Swala na uswali] [Imepokewa na Bukhari.].
B). Aicheleweshe Adhuhuri mpaka kabla ya Alasiri, kisha aoge na aswali Adhuhuri na Alasiri, na atafanya hivi katika Swala nyingine. Hii ni kwa neno lake Mtume ﷺ kumwambia Hamnah binti Jahsh Radhi za Allah ziwe juu yake:
فَإِنْ قَوِيتِ عَلَى أَنْ تُؤَخِّرِي الظُّهْرَ وَتُعَجِّلِي العَصْرَ، ثُمَّ تَغْتَسِلِينَ حِينَ تَطْهُرِينَ، وَتُصَلِّينَ الظُّهْرَ وَالعَصْرَ جَمِيعًا، ثُمَّ تُؤَخِّرِينَ المَغْرِبَ، وَتُعَجِّلِينَ العِشَاءَ، ثُمَّ تَغْتَسِلِينَ، وَتَجْمَعِينَ بَيْنَ الصَّلَاتَيْنِ، فَافْعَلِي، وَتَغْتَسِلِينَ مَعَ الصُّبْحِ وَتُصَلِّينَ، وَكَذَلِكِ فَافْعَلِي، وَصُومِي إِنْ قَوِيتِ عَلَى ذَلِكَ رواه إبن ماجة
[Na ukiweza kuchelewesha Adhuhuri na kuitanguliza Alasiri, kisha ukaoga unapo twahirika na ukakusanya baina ya Swala (mbili) Adhuhuri na Alasiri, kisha ukachelewesha Swala ya Magharibi na akaitanguliza Swala ya Isha, kisha uoge, na ukusanye Swala mbili, basi fanya hivyo. Na ukauoga wakati wa wa swala ya Alfajiri na ukswali basi fanya hivyo, na ufunge, kama waeza kufunga] [Imepokewa na Ibnu Maajah.].
4. Mwanamke akitokwa na damu kwa sababu yoyote ile, kama operesheni, na ikatiririka, basi yeye ni mojawapo wa hali mbili:
Hali ya Kwanza: Ijulikane kuwa hatapata hedhi. Huyu hazipitishwi kwake hukumu za istihadhah, wala haachi kuswali wakati wowote, na ile damu ni ya ugonjwa na kuharibika kwa kitu, na atatawadha kwa kila Swala.
Hali ya Pili: Ijulikane kuwa yeye inamkinika kuingia hedhini. Huyu hukumu yake ni ya istihadhah.
5. Inafaa kumuingilia mwanamke aliye kwenye istihadhah.kwa kuwa Sheria haikumkataza.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.