SOMO LA FIQHI
Sharti tunazozikusudia hapa ni zile sharti za kusihi Swala.
Kwanza kabisa tufahamishe Maana ya sharti :
Sharti ya kitu ni lile jambo au tendo ambalo upatikanaji wa kitu husika unalitegemea jambo/tendo hilo lakini lenyewe si sehemu ya kitu hicho.
Mfano:
Mmea ili upatikane/uwepo juu ya uso wa ardhi unahitaji maji pamoja na kuwa maji sio sehemu ya mmea huo.
Kwa hivyo basi maji ni sharti katika upatikanaji na kuwepo kwa mmea kwani bila ya maji hakuna mmea lakini bado mvua haiwi ni sehemu ya mmea huo.
Baada ya kujua ainisho la sharti, hebu sasa tuziangalie sharti za kusihi kwa swala moja baada ya jingine :
Suali: Ni yapi Mashrti ya kusihi Swala?
Jawabu: Masharti ya kusihi Swala ni haya yafuatayo:
1. KUINGIA WAKATI
Swala ya faradhi ina wakati ambao haiswihi kabla yake, wala baada yake isipokuwa kwa dharura. Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا} النساء:103}
[Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalum.] [4: 103]
yaani imefaradhiwa katika vipindi maalumu.
2. KUTWAHIRIKA NA HADATHI
A. Kutwahirika na hadathi ndogo (tukio la kutokuwa na udhu)
Nako kunapatikana kwa kutawadha. Mtume ﷺ anasema:
لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ] رواه البخاري]
[Mwenyezi Mungu hatakubali Swala ya mmoja wenu akitokewa na tukio la kutokuwa na udhu mpaka atawadhe.] [ Imepokewa na Bukhari.]
B. Kutwahirika na hadathi kubwa:
nako ni kunapatikana kwa kuoga, kwa neno la mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا} النساء:6}
[Na mkiwa na janaba jitwahirisheni.] [5: 6]
Na yoyote atakayekumbuka akiwa katika Swala kuwa hana udhu au ametokewa na jambo la kuharibu udhu katikati ya Swala, basi Swala yake itatanguka Na itamlazimu ajitoe Swalani ili ajitwahirishe na bila ya kutoa Salamu, kwa kuwa swala ishatanguka na bado haijamalizika, na utoaji salamu ndio mwisho wa Swala.
3. UTWAHARA WA NGOO, MWILI NA MAHALI.
A. Utwahara wa nguo,
kwa neno lake Mwenyezoi Mungu aliyetukuka:
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ} المدثر:4}
[Na nguo zako twahirisha] [74: 4]
B. Utwahara wa mwili
kwa ilivyothubutu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliipita kwenye kaburi mbili akasema:
إنهما ليعذبان ، وما يعذبان في كبير ؛ أما أحدهما فكان لا يستتر من البول] رواه البخاري]
[Hakika wawili hawa wanaadhibiwa, Na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa, Ama huyu alikuwa hajiepushi na hajikingi na mkojo.] (na mkojo usimuingie) [Imepokewa na Bukhari.]
C. Utwahara wa mahali.
kwa hadithi ya mbedui aliyekojoa msikitini, Mtume ﷺ alisema:
دعوه وأهريقوا على بوله ذنوباً من ماء - أو سجلا من ماء ] رواه البخاري ومسلم ]
[Muacheni na umwagieni mkojo wake ndoo ya Maji.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Suali: Mtu anapokosa sehemu ya kuswali atafanya nini?
Jawabu: Ardhi yote ni msikiti, kwa kuwa kuswali hapo inafaa. Mtume ﷺ amesema:
وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا، وأيما رجل من أمتي أدركته الصلاة فليصل] رواه البخاري ومسلم]
[Nimefanyiwa ardhi kuwa ni mahali pa kuswali na mahali pakujitwahirishia. Basi mtu yoyote miongoni mwa umma wangu aliyeingiliwa na kipindi cha Swala na aswali.]
[Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Suali: Ni sehemu gani zinazo katazwa mtu kuswali?
Jawabu: Sehemu zilizokatazwa, mtu kuswali ni kama vile kuswali makaburini na chooni, na sehemu ya malazi ya ngamia,kwa kuwa Mtume ﷺ alisema:
الأرض كلها مسجد إلا المقبرة والحمام] رواه الترمذي]
[Ardhi yote ni mahali pa kuswali, isipokuwa makaburini na chooni.] [Imepokewa na Tirmidhi.]
Na dalili ya sehemu ya malazi ya ngamia ni kauli yake Mtume ﷺ:
ولا تصلوا في أعطان الإبل] رواه الترمذي]
[Musiswali katika malazi ya ngamia] [Imepokewa na Tirmidhi.]
4. KUSITIRI TUPU.
Na tupu ya mwanamume: ni kuanzia kitovuni hadi gotini.
Ama tupu ya mwanamke: ni mwili wake wote isipokuwa uso na vitanga vya mikono.
na dalili ni neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
خُذُوا زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُل مَسْجِدٍ} الأعراف:31}
[Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada,] [Al-A'araaf:31]
قَال ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا : الْمُرَادُ بِالزِّينَةِ فِي الآْيَةِ : الثِّيَابُ فِي الصَّلاَةِ
Asema Ibnu Abbas radhi za Allah ziwe juu yake "Makusudio ya pambo katika aya hii,ni kuvaa nguo katika Swala."
Na kwa neno lake Mtume:
لاَ يَقْبَل اللَّهُ صَلاَةَ حَائِضٍ إِلاَّ بِخِمَارٍ] رواه أبوداود والترمذي]
[Hakubali Mwenyezi Mungu swala ya Mwanamke alieingia hedheni (alie baleghe) ila kwa mtandio] [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy]
FAIDA
Kufinika mabega
Inamlazimu mwenye kuswali avae nguo yenye kufinika mabega yake na shingo yake, kwa kuwa Mtume alisema:
لَا يُصَلِّي أَحَدُكُمْ فِي الثَّوْبِ الْوَاحِدِ لَيْسَ عَلَى عَاتِقَيْهِ شَيْءٌ] رواه مسلم]
[Asiswali mmoja wenu kwa nguo moja bila ya kuwa kwenye mabega yake kitu chochote.] [Imepokewa na Muslim.]
Na kufanya hivyo ni Sunna kwa kauli ya jamhuri ya wanachuoni,na ni kuhishimu ibada ya Swala,isipokuwa Madh'habu ya imamu Ahmad anaona ni wajibu kufanya hivyo katika Swala ya Faradhi.
5. KULELEKEA KIBLA.
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ] البقرة:144]
[Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo.] [Al-Baqara:144]
MAELEZO KUHUSU KUELEKEA KIBLA
A. La wajibu kwa mwenye kuswali ndani ya msikiti wa Haram aielekee alkaba yenyewe. Ama yule anayeswali akiwa mbali na Alkaaba, basi ataelekea upande wa hiyo Alkaba na sio kuielekea yenyewe, kwa kuwa hawezi kuielekea yenyewe. Kwa hivyo, Mtume ﷺ alisema:
ما بين المشرق والمغرب قبلة] رواه الترمذي]
[baina ya mashariki na magharibi ni kibla.] [Imepokewa na Tirmidhi]
2. Swala ya Sunna kwa aliyepanda mnyama, kibla chake ni ule upande ambao kile kipando kinaelekea, kwa kuwa ilithubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akiswali juu ya kipando chake akielekea popote pale kile kipando kinapoelekea, na alikiswali witri juu yake, isipokuwa yeye hakuwa akiswali juu yake Swala za faradhi] [Imepokewa na Abu Dawud.]
Suali: Asiyejua Kibla Atafanya Nini?
Jawabu: Asiyejua kibla akiwa kwenye jengo au mahali penye watu walio karibu, atauliza au atajijulisha kibla kwa vibla vya misikiti au dira au jua au mwezi au vinginevyo. Akitoweza kujua basi atajitahidi na atafuata lile lenye nguvu katika dhana yake, kwa neno lake Mwenyezi Mungu:
فَاتَّقُوا اللَّهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ} التغابن:16}
[Muogopeni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza] [64: 16]
SOMO LA FIQHI
Swala za fardhi ambazo Muislamu amefaradhiwa na Mola wake kuziswali kila siku, mchana na usiku ni swala tano.
Kila moja miongoni mwa swala tano hizi ina wakati wake maalum ambao muislamu anawajibikiwa kuiswali ndani ya wakati huo.
1.ALFAJIRI.
2.ADHUHURI.
3. AL-ASIRI.
4.MAGHRIBI.
5.ISHAA.
Na dalili ya uwajibu wa kuswali mara tano kwa siku zimekuja aya kadha zikishiria nyakati hizi miongoni mwa aya hizo ni neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
{فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ} الروم:18
[Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na asubuhi,Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri.] [Al-Rruum:18]
رَوَى لَيْثٌ عَنْ الْحَكَمِ عَنْ أَبِي عِيَاضٍ قَالَ : قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ : " جَمَعَتْ هَذِهِ الآيَةُ مَوَاقِيتَ الصَّلاةِ : { فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ } الْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ { وَحِينَ تُصْبِحُونَ } الْفَجْرَ { وَعَشِيًّا } الْعَصْرَ { وَحِينَ تُظْهِرُونَ } الظُّهْرَ
Amepokea Al-layth kutoka kwa Al-Hakam kutoka kwa Abuu Iyaadh Amesema: Asema Ibnu Abbas: aya hii imekusanya nyakati za Swala zote "Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni" Maghribi na Ishaa "Mtakaseni Mwenyezi Mungu asubuhi," Al-fajiri "Wa'ashian" Alasiri "Wahiina Tudh'hiruun" Adhuhuri.
Na neno lake Mwenyezi Mungu:
أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا} الإسراء:78}
[Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima] [Al-Israai:78]
Jua linapo pinduka ni Swala ya Adhuhuri na Alasiri, "mpaka giza la usiku" ni Swala ya Maghribi na Swala ya Ishaa "na Qur'ani ya Al-fajiri" ni Swala ya Al-fajri, kama ilivyo pokelewa na Ibnu Abbas na wengine katika Salaf Mungu awarehemu.
NA KATIKA SUNNA
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا ، " أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ مُعَاذًا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِلَى الْيَمَنِ فَقَالَ : ادْعُهُمْ إِلَى شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذَلِكَ فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدِ افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ رواه البخاري ومسلم
Imepokelewa na Ibn Abbaas – Allah awaridhie kwamba Mtume ﷺ alimtuma Mua'adh – Allah amridhie – kwenda katika nchi ya Yemen (kulingania dini) akamwamiba:
[Walinganie (Waite) kutamka shahada kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na kwamba mimi Muhammad ni Mjumbe wa Allah, ikiwa wao watalitii hilo (watalikubali) basi wafahamishe kwamba Allah amefaradhisha juu yao swala tano mchana na usiku………] [Bukhaariy na Muslim.]
Kauli yake Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipomwambia yule mkazi wa majangwani ambaye alimuliza swala zilizo faridhi juu yake.
فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَعَلَى آلِهِ وَسَلَّمَ : " خَمْسُ صَلَوَاتٍ فِي الْيَوْمِ وَاللَّيْلَةِ " ، قَالَ : هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُنَّ ؟ ، قَالَ : " لا ، إِلا أَنْ تَطَّوَّعَ رواه البخاري ومسلم
Akasema Mtume ﷺ : [Swala tano kila mchana na usiku] Yule mkazi wa majangwani akamuuliza (tena). Je, ninalazimika na swala nyingine zisizo hizo (tano) (Mtume) akamjibu [Hapana ila swala za suna] [Imepokewa na Bukhaary na Muslim.]
Na neno lake Mtume ﷺ:
فَرَضَ اللَّهُ عَلَى أُمَّتِي لَيْلَةَ الْإِسْرَاءِ خَمْسِينَ صَلَاةً، فَلَمْ أَزَلْ أُرَاجِعُهُ وَأَسْأَلُهُ التَّخْفِيفَ حَتَّى جَعَلَهَا خَمْسًا فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ] رواه مسلم]
[Amefaridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umati wangu Lailati Israai, Swala khamsini, sikuwacha kumrejelea (Mwenyezi Mungu Mtukufu) na kumuomba kupunguziwa mpaka Akazijaalia tano kwa kila siku - mchana na usiku] [Imepokelewa na Muslim]
SOMO LA FIQHI
Suali: Ni zipi Fadhla za Swala?
Jawabu: Swala ina Fadhla nyingi Miongoni mwa fadhla zake ni hizi:
1. Swala ni nuru kwa mwenye kuswali. Mtume ﷺ amesema:
والصلاة نور] رواه مسلم]
[Na Swala ni Nuru] [ Imepokewa na Muslim.].
2. Swala ni kafara ya dhambi. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema:
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ} هود:114}
[Na simamisha Swala ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zinazokaribiana na mchana. Hakika mema yanafuta maovu. Hayo ni makumbusho kwa wenye kukumbuka] [11: 114].
Na amesema Mtume ﷺ:
رَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ، هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ؟ ، قَالُوا: لَا يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ، قَالَ: فَذَلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، يَمْحُو اللهُ بِهِنَّ الْخَطَايَا رواه البخاري ومسلم
[Mnaonaje, lau kuna mto mlangoni mwa mmoja wenu ambao anaoga ndani yake kila siku mara tano, je kutasalia chochote cha uchafu mwilini mwakeWakasema: Hakutasalia uchafu wowote katika mwili wake. Akasema Mtume ﷺ: Huo ndio mfano wa Swala tano,. Mwenyezi Mungu kwa hizo Swala anayafuta madhambi] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Swala ni sababu ya mtu kuingia Peponi. Mtume ﷺ alimwambia Rabi’ah bin Ka’ab, alipomtaka wasuhubiane naye Peponi,: Mtume akamjibu:
فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ ، بِكَثْرَةِ السُّجُودِ ] رواه مسلم]
[Nisaidie kwa kuishughulisha nafsi yako kwa kusujudu sana] [Imepokewa na Muslim.].
SOMO LA FIQHI
Suali: Ni ipi hukmu ya mwenye kuacha swala?
Jawabu: Hukumu ya mwenye kuacha Swala inategemea na namna anvyo itakidi juu ya swala na hii inakuwa ni hali mbili:
Hali ya kwanza: Mwenye kuacha Swala kwa kukanusha uwajibu wake:
Hali hii kwanza Atafahamishwa uwajibu wa Swala akiwa hajui. Na Akiendelea kukanusha, basi yeye atakuwa kafiri, mkanushaji wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na umoja wa Waislamu.
Hali ya pili: Mwenye kuacha Swala kwa uvivu:
Na kwa hali hii wanachuoni wamekhatalifiana juu Kauli mbili:
Kauli ya kwanza: Mwenye kuacha Swala kwa uvuvi atakuwa ni Faasiq wala hakufuru na kutoka katika Uislamu, na msimamo ni ndio msimamo wa wengi katika wanachuoni.
Na dalili walizo zitegemea ni neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
إِنَّ اللَّهَ لا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ} النساء:47}
[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye] [Al-Nnisaa:47]
Wanasema mwenye kuacha Swala atakuwa ameingia katika aya hii madamu hakuwa ni mwenye kumshirikisha mwenyezi Mungu
Na katika Hadithi wametolea dalili hadithi hii:
حديث عتبان بن مالك رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: [إن الله حرم على النار من قال لا إله إلا الله، يبتغي بذلك وجه الله] رواه البخاري
Amepokea Utbaan bin Maalik radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume Amesema [Hakika Mwenyezi Mungu amemuharimishia moto Mwenye kusema hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu akitaka kwa hilo uso wa Mwenyezi mungu.] [Imepokelewa na Bukhari]
Kauli ya pili: Mwenye kuacha Swala kwa kukusudia na uvivu atakuwa amekufuru. Na ni juu ya kiongozi amlinganie kuswali na amuorodheshee toba kwa muda wa siku tatu. Basi akitubia ni sawa, na akitotubia atamuua kwa kuwa ameritadi.
Na wametegemea neno lake Mwenyezi Mungu aliposema:
فَإِنْ تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ} التوبة:11}
[Basi wakitubu na wakashika Sala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini.] [Al-Tawba:11]
Wakasema aya inamanisha kuwa mtu asie swali si ndugu yenu katika Dini.
Na kwa kauli yake Mtume ﷺ:
العهد الذي بيننا وبينهم الصلاة، فمن تركها فقد كفر] رواه أحمد والترمذي]
[Ahadi iliyoko baina ya sisi na wao ni Swala. Yoyote yule atakayeiacha basi atakuwa amekufuru]
[Imepokewa na Tirmidhi.]
Na kauli yake ﷺ:
بين الرجل وبين الشرك والكفر ترك الصلاة] رواه مسلم]
[Hakika baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swala] [Imepokewa na Muslim.]
Na huu ndio msimamo ulio Mash'hri wa Madhhebu ya Imam Ahmad.na ndio kauli ya Sheikhul Islam Ibnu Taymiyah na Sheikh Ibnu baaz na Sheikh Ibnu Uthaymin kwa yule aliacha swala kabisa ama kwa yule anae swali na kuacha huyu hakufuru.
SOMO LA FIQHI
Suali: Nipi hukumu ya swala tano?
Jawabu: Swala tano ni wajibu kwa kila Muislamu, kulingana na Qur'ani, na Sunna na umoja wa wanavyuoni:
1. katika Qur’ani:
Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ} البقرة:43}
[Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wenye kurukuu] [Al-Baqara: 43].
Na Amesema tena katika aya nyingine:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا} النساء:103}
[Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu] [Al-Nnisaai:103]
2. Na katika Sunna:
بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان رواه البخاري ومسلم
Amesema ﷺ:[Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano: kushuhudia kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na mtume wake, na kusimamisha Swala, nakutoa Zaka, nakuhiji Alkaba na kufunga mwezi wa Ramadhani] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na imepokewa kutoka kwa Twalhah bin ‘Ubeidillah kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ kuhusu Uislamu, akasema ﷺ:
خمسُ صلواتٍ في اليوم واللَّيلة]، فقال هل عليَّ غيرها؟ قال: [لا، إلاَّ أن تَطوَّع] رواه البخاري ومسلم]
[Ni Swala tano mchana na usiku. Akasema: “Je, kuna nyingine zinazonilazimu sizizokuwa hizo?” Akasema: La, isipokuwa ukijitolea] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Umoja wa wanavyuoni:
Umma kwa umoja wao wamekubaliana juu ya uwajibu wa Swala tano kipindi cha mchana na usiku,na kuwafikiana bila ya khitilafu yoyote kwamba swala ni mojawapo ya nguzo za Uislamu.
SWALA INAMLAZIMU NANI?
Swala inamlazimu kila Muislamu, aliyebaleghe, mwenye akili, awe mwanamume au mwanamke.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.