SOMO LA FIQHI
Suala: Ni nini Maana ya ihram (Kuhirimia)
Jawabu: Maana ya Ihram kilugha: Ni kuzuia
Ama maana ya Kuhirimia kisheria:
"Ni nia ya kuingia kwenye ibada ikifungamana na mojawapo ya matendo ya Hijja"
Na haifungamani Iharamu ila kwa nia, Mtu hahisabiwi kuwa amehirimia kwa kule kuazimia kwenda hijja au Umra kwa sababu toka aliposafiri mji wake huwa ameazimia kuhiji au kufanya umra, na wala hawi ni mwenye kuhirimia kwa kuvaa ihram au kuleta talbiya bila kutia nia ya ibada ya hijja kwa neno lake Mtume ﷺ :
إنما الأعمال بالنيات وإنما لكل امرئ ما نوى] متفق عليه]
[Hakika amali zote ni kwa nia na kila mtu hulipwa kama alivyo nuiya] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
SOMO LA FIQHI
Suali: Ni nini maana ya Miiqaat (Nyakati)
Jawabu: Nyakati kilugha ni kuweka mpaka baina ya vitu viwili.
Ama kwa istilahi ya sheria
Ni mipaka iliyowekwa na sharia kwa ajili ya ibada na yawakati na Namahali.
AINA YA NYAKATI
Kwanza: Nyakati za mahali
Nyakati za mahali
Ni sehemu zilizowekwa na Sheria kuhirimia kutoka hapo
Haifai kwa anyetaka kuhiji au kufanya Umra azipite sehemu hizo isipokuwa awe amehirimia. Nazo ni sehemu tano:
1. Dhul Hulaifah
Nayo ipo upande wa kusini wa mji wa Mtume wa Madina, na unaitwa «Abyaar ‹Ali». Iko mbali na Makka kwa masafa ya kilimita 420.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Madina.
2. Juhfah:
Nayo iko karibu ya mji wa Raabigh, na ina umbali wa kiasi cha kilomita 186 kutoka Makka.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Shaam, Masri na nchi za upande wa maghribi
3. Yalamlam:
Nayo ni bonde kubwa kwenye njia ya watu wa Yaman kwenda Makka.
Kwasasa inaitwa: Assa›diyyah, na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 120.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Yaman.
4. Qarnul Manaazil:
Na sasa inaitwa ( Assaylul Kabiir), na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 75.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Najd na Twaif. Na juu yake, kwenye njia ya Twaif upande wa Hadaa kuna mahali panapoitwa Waadii Muharram.
Na pote pawili ni sehemu ya kuhirimia watu wa Najd na wale wanaokuja kupitia njia ya Twaif.
5. Dhaatu'Irq:
na sasa inaitwa (Dhariibah au Khuraibaat).
Napo ni mahali upande wa Mashariki ya Makka. Umbali wake na Makka ni kiasi cha kilomita 100. Na kwa sasa hapo mahali pamehamwa.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa upande wa Mashariki (Iraki, Irani na nchi za nyuma yake. Na dalili ya yaliyopita ni ni riwaya iliyopokewa kutoka kwa Ibnu Abbas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:[Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliwawekea watu wa Madina Dhulhulaifah iwe ni mahali pa wao kuhirimia, akawawekea watu wa Sham hapo Juhfa. Akawawekea watu wa Najd hapo Qarnulmanaazil, Akawawekea watu wa Yaman hapo Qarnulmanaazil na akasema:
هُنَّ لَهُنّ وَلِمَنْ أَتَى عَلَيْهِنَّ مِنْ غَيْرِهِنَّ] رواه البخاري]
[Sehemu hizo ni zao wao na wanaokuja hapo kati wa watu wa maeneo mengine wanaotaka kuhiji au kufanya Umra] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Ama Dhaatu ‘Irq haikutajwa kwenye hadithi iliyotangulia, na lililowekwa ni ‘Umar ibnu l- Khattaab [Imepokewa na Bukhari.].
MAELEZO
- Mwenye kuvuka sehemu hizi za mikati bila ya kuhirimia ni lazima kurudi na kuhirimia ikiwezakana, na isipoweza kufanya hivyo basi atawajibika kutoa fidiya, nao ni mbuzi atakae mchinja makka na agawanye nyama yake kwa masikini wa makka.
- Mwenye kupita sehemu za Mikaati kwa mtu asie kuwa ni wasehemu hiyo basi atahirimi hapo, lau mtu wakutoka najdi amekuja kwa njia ya watu wa madina atahirimia sehemu ya watu wa madina (Abyaar Ali)
- Mtu ikiwa nymba yake iko ndani ya sehemu ya kuhirimia kwa upande wa makka basi Mtu huyu atahirimia hija na umra sehemu alipo Mfano wa watu wa Jiddah na Bahra na Ashraa’i.
- Mwenye kuja kwa njia ya anga na bara, na bahari, huyu atahirimia akiwamkabala na sehemu ya Mikati iliyo karibu. Kwa kauli ya umar binl-khatwab (angaliyani mkabala wake kutoka kwenye njia yenu) [Imepokewa na Bukhari.]
- Mwenye kutia nia ya kuhiji kwa mtu wa makka au asie kuwa mtu wa makka huyu atahirimia makka, ama akitaka kufanya Umra atatoka kwenda tan’iim na Ji’iraan nazo ni sehemu ziko nje ya mipaka ya haram
Pili: Nyakati za kuhirimia
Nyakati za kuhirimia
Zama za kuhiji na kufanya Umra
A. Nyakati za Hijja
Ni miezi ya Hija nayo ni: Mfungomosi, Mfungopili na siku kumi za Mfungotatu.
kama alivyo sema Mwenyezi Mungu:
الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ} البقرة:197}
[Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija.] [Al Baqara:197]
B. Nyakati za Umra
Ni mwaka mzima
SOMO LA FIQHI
Suali: Ni yapi masharti ya Kuwajibika Hijja ?
Jawabu: Kuwajibika Hijja kuna shuruti tano:
Ya Kwanza, kuwa ni Muislam,
kwani Hija ni ibada sawa na ibada nyengine kama vile, Sala, Saumu, Zaka. Kwa sababu kafiri ibada zake hazikubaliwi .Kwa neno lake Mwenyai mungu mtukufu:
وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ} التوبة:54}
[Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake,] [Al Tawba:54]
Ya Pili, kuwa ni balegh,
Mtoto mdogo kabla ya balegh halazimiki na Hija; sawa na ibada nyengine. Hivi ni kwa neno lake Mtume :
رُفِعَ الْقَلَمُ عَنْ ثَلاثَةٍ : عَنْ النَّائِمِ حَتَّى يَسْتَيْقِظَ ، وَعَنْ الصَّبِيِّ حَتَّى يَحْتَلِمَ ، وَعَنْ الْمَجْنُونِ حَتَّى يَعْقِلَ] رواه أبوداود]
[Imeinuliwa kalamu kwa watu watatu (hawaandikiwi dhambi) aliyelala mpaka azunduke, mtoto mapaka abaleghe na mwendawazimu mpaka apate akili] [Imepokewa na Abuu Daud].
Lakini lau mtoto mdogo atahirimia hija basi hija yake itasihi.Hii ni kwa hadithi ya Ibnu ‹Abbas radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mwanamke mmoja alimuinulia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ mtoto, na akasema: «Je, huyu ana Hija? Mtume akasema:
نعم ، ولك أجر] رواه مسلم]
[Ndio, nawe una thawabu] [Imepokewa na Muslim.].
Lakini haimtoshelezi na Hijja ya Uislamu, na itahesabiwa ni Sunna,na atakapo baleghe atawajibika kuhiji tena ikiwa na uwezo.
Ya Tatu, awe ni mwenye akili timam;
mgonjwa wa akili mwenda wazimu haimlazim Hija, sawa na ibada nyengine. Kwa hadithi iliyotangulia.
Ya Nne, kuwa huru,
Asie kuwa huru hawajibikiwi na Hija, kwa sababu anakuwa ni mwenye kumtumikia bwana wake,huwajibikiwa na Hija pale anapokuwa huru. Kwa hadithi ya Mtume:
أيما عبد حج ثم عتق فعليه حجة أخرى] رواه أحمد والبهقي والحاكم]
[Mtumwa yeyote yule akihiji kisha akapewa uhuru, itamlazim ahiji tena]. [Imepokewa na Ahmad na Al Bayhaqiy na Al Haakim].
Lakini sharti hili limeondokwa kwa kutoweko watumwa zama zetu hizi.
Ya Tano, Kuwa na uwezo.
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنْ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلا} آل عمران:97}
[Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea……".] [Al 'Imraan : 97].
Sita. Kwa Mwanamke awe na maharimu yake
[Mahram: ni yule ambaye ni haramu kwa mwanamke kuolewa naye kama baba, ndugu na mjomba.]
Kwa hadithi ya Ibnu ‹Abbas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema: Nilimsikia Mtume ﷺ akisema:
لا تُسَافِرْ الْمَرْأَةُ إِلا مَعَ ذِي مَحْرَمٍ] رواه البخاري ومسلم]
[Hasafiri mwanamke isipokuwa pamoja na mtu maharimu yake]. [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Akainuka mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji, na mimi nimejisajili katika vita kadha na kadha. Akasema Mtume ﷺ: [Toka uende kuhiji na mkeo] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
SOMO LA FIQHI
Suali: Ni nini Maana ya Umra
Jawabu: Maana ya Umra Umra kilugha ni Ziara
Ama maana yake kisheria
Ni kuizuru Nyumba Takatifu (Alkaba) wakati wowote mtu anapotaka, kwa kutekeleza matendo ya ibada maalumu.
Suali: Ni ipi Hukumu ya Umra na fadhla zake
Jawabu: Umra ni wajibu wa mara moja katika umri kama vile hajji. Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّهِ} البقرة:196}
[Na timizeni Hija na 'Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu]. [Al Baqara : 196]
Na kwa kauli yake Mtume ﷺ :
الإسلام أن تشهد أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله ، وتقيم الصلاة ، وتؤتي الزكاة ، وتحج البيت وتعتمر ، وتغتسل من الجنابة ، وتتم الوضوء ، وتصوم رمضان ) رواه إبن خزيمة والدار قطني, وقال الدارقطني : هذا إسناد ثابت صحيح
[Uislamu ni ukubali kwamba hakuna mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe Swala, na utoe Zaka, na uikusudie Alkaba kwa ibada ya Hija na ufanye Umra, na uoge kutokana na janaba, na ukamilishe udhu, na ufunge Ramadhani] [Imepokewa na Ibnu Khuzaimah na AL-Ddaar Qutiniy na akasema isnadi yake ni thaabit na nisahihi]
Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة] رواه البخاري ومسلم]
[Umra mpaka Umra ni kafara ya dhambi baina yake, na Hija iliyokubaliwa haina malipo isipokuwa Pepo] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
SOMO LA FIQHI
Suali: Ni ipi hukumu ya Hijja na fadhla zake ?
Jawabu: Hijja ni mojawapo ya nguzo za Kiislamu. Mwenyezi Mungu Alioyetukuka Ameilazimisha kwa waja wake. Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:
وَلِلَّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ} سورة آل عمران:97}
[Ni haki ya Mwenyezi Mungu kwa watu waihiji Alkaba, kwa anayeweza kwenda huko. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi Hawahitajii walimwengu] [Al Imraan: 97]
Na amesema Mtume ﷺ:
بني الإسلام على خمس شهادة أن لا إله إلا الله وأن محمدا رسول الله وإقام الصلاة وإيتاء الزكاة وحج البيت وصوم رمضان] متفق عليه]
[Uislamu umejengwa juu ya misingi mitano: Kukubali kuwa hapana mola isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, kuikusudia Alkaba kwa Hija na kufunga mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na amsema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
مَنْ حَجَّ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبه] رواه الترمذي]
[Mwenye kuhiji asiseme maneno machafu [ Rafath: ni neno linalotumika kumaanisha maneno machafu.] na asitoke kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu [ Fusuuq: maasia.], atasamehewa dhambi zake zilizotangulia] [Imepokewa na Tirmidhi.].
Na Hijja ni lazima kwa umri mara moja.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.