Menu

Fiqhi


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Masiku ya Tashriiq
Ni siku tatu, siku ya kumi na moja na siku ya kumi nambili na siku ya kumi na tatu katika Mwezi wa Mfungotatu zimeitwa kwa jina hilo kwa sababu nyama za Udh’hiya zikikatwakatwa na kuanikwa juani ili zikauke na Mtume ﷺ Alisema kuhusu masiku haya

 

أَلاَ وَإِنَّ هَذِهِ الأَيَّامَ أَيَّامُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ وَذِكْرِ اللهِ عَزَّ وَجَلَّ]    رواه أبوداود]

 

[Jueni ya kuwa masiku haya ni masiku ya kula nakunywa na kumtaja Mwenyezi Mungu]    [Imepokewa na Abuu Daud]



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Maelekezo
Muislamu ajiepushe na kuwaudhi ndugu zake Mahujaji wakati wa kutupa vijiwe jamaraat, nawakati wakufanya ibada nyinginezo za hija.

Ahakikishe kuwa kijiwa kimeingie kwenye ndani ya birika, baadhi ya watu wanakosea wakidhani kuwa unapo rusha kijiwe ni kulenga kiguzo na kijiwe kisingie kwenye birika, na baadhi hutupa kijiwa akiwa mbali na birika na kijiwe kisingie kwenye birika basi mwenye kutupa namna hiyo huwa hakutekeleza wajibu wa kutupa.

- Na ni juu ya Muislamu asivuke mipaka katika kurusha vijiwe asitupe jiwe kubwa au kurusha viatu, sunna ni kijiwe kiwe kikubwa kidogo kuliko dengu kwa Hadithi ya Jaabir bin Abdillah Radhi za Allah zimfikie yeye Nakasema:

رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَمَى الْجَمْرَةَ بِمِثْلِ حَصَى الْخَذْفِ]    رواه مسلم]

 

[Nimemuona Mtume ﷺ Akilitupia jamara kwa kijiwe kidogo mfano wa koko ya tende]        [ Imepokewa na Muslim.]

Na vjiwe vyakutupa ni vidogo atavishika kwa vidole viwili na kutupa].

- Na akitupa vijiwe vyote kwa mara moja hahisabiwi ila kijiwe kimoja, na lau ataviweka kwenye kitu avirushe vyote kwa pamoja haitasihi bali ni lazima kupatikane kurusha.


 


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Haji atakapofika muzdalifa atanza na Swala ataswali Maghrib na Ishaa kwa kuzikusanya na kupunguza Swala ya isha, kabla kuteremsha mizigo na vitu vyake.

2. Nilazima kulala Muzdalifa usiku wake na ataswali Alfajiri mapema, na haifai kuondoka muzdalifa kabla ya Alfajiri ila kwa wenye udhuru, kama watu madhaifu katika wanawake, na watoto na kwa wale wanaofuatana nawao, ambao wanawatumikia wao yafaa kuodoka nawao mwisho wa usiku Mwezi unapo zama.

3. Anapo maliza kuswali Alfajiri inapendekezwa kwa mahujaji aende kwenye Mash’aril haram, na aeleke kibla na azidishe dhikri na Dua hali yakuwa ameinuwa mikono yake na ataendelea kufanya hivyo mpaka kupambazuke sana, na sehemu yoyote atakapo simama Muzdalifa yafaa, kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

وقفت هاهنا وجمع كلها موقف]   رواه مسلم]

 

[Nimesimama hapa na jam’u yote ni mahali pakisimamo]   [Imepokewa na Muslim]

na makusuduio ya Jam’u ni Muzdalifa.

4. Anapoondoka haaji kutoka muzdalifa inapendekezwa aokote vijiwe saba pekeyake kwa ajili yakutupa kwenye jamaraat, ama masiku yalio baki ataokota vijiwe mina au sehemu yoyote atakapo okota yafaa



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Mpangilio wa Matendo katika Siku ya Iddi
Sunna katika mipangilio ya siku ya idd ni kama inavo fuata:

1.Kutupa vijiwe.

2. Kuchinja.

3. Kunyoa au kupunguza.

4. Kufanya Twawafu.

5. Kufanya sai kwa mwenye sai,

Na lau atatanguliza moja katika mambo haya juu ya jengine yafaa na hakuna ubaya wowote, kwa sababu MtumeAliruhusu hilo, lau mtu atanyoa kwanza kisha akatupa mawe itasihi, na lau atachinja kwanza kisha akafanya Twawafu kisha akatupa vijiwe ni sawa, kwa sababu hakulizwa Mtume ﷺ kwa mwenye kutanguliza jambo na kuakhirisha jengine ila akisema:

 

افْعَلْ وَلاَ حَرَجَ]      متفق عليه]

 

[Fanya na hakuna ubaya]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Kuhalalishiwa Mara ya Kwanza na Kuhalalishiwa Mara ya Pili:-

Kuhalalishiwa ya kwanza:

Ni kuhalalishiwa yote yale yalokuwa ni haramu kufanya kwa mwenye kuwa katika ihram isipokuwa kufanya tendo la ndoa au kufunga ndoa itakuwa si halali kwake kufanya hivyo, na inapatikana mtu kuhalalishiwa kwa kufanya mawili katika yanao fuata:

kutupa vijiwe kwenye jamaraat, kunyoa au kupunguza, kufanya Twawafu pamoja nakufanya sai kwa atake kuwa na sai

Kuhalalishiwa mara ya pili:

Ni kuhalalishiwa kufanya yote yale yaliokuwa ameharamishiwa kufanya alipokuwa kwenye ihram, na hupatikana uhalali wapili kwa kufanya yale yalio tangulia yote pamoja.

- Kuchinja haina mafungamano na kuhalalishiwa, lau atachelewesha kuchinja mpaka siku ya pili siku ya kumi na moja, na akafanya yale mengine siku ya idd atakuwa amehalalishwa.


 


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Inahisabika kuwa mtu amesimama arafa kwa kuweko mwenye kuhiji uwanja wa arafa siku ya tisa, sawa akiwa amesimama ama amekaa ama amelala ama amepanda, na silazima kuwa amesimama.

2. Kusimama arafa ni Nguzo miongoni mwa nguzo za Hijja na haisihi Hija ya mtu ikiwa hakusimama Arafa, na mwenye kukosa kusiamam Arafa huwa ameikosa Hija kwa neno lake Mtume :

 

 الحج عرفة ]  رواه احمد والترمذي]

 

[Hija ni Arafa]    [Imepokewa na Ahmad na Attirmidhiy]

3. Unaanza wakati wa kisimamo cha Arafa kuanzia kutoka kwa Alfajiri siku ya tisa mpaka Alfajiri ya siku ya kumi, mwenye kusiama Arafa katika wakati huu japo kidogo hali yakuwa ni mtu afaaye kusimama hija yake itasihi, na mwenye kukosa kusimama wakati huu hija yake haikusihi Amepokea Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume Amesema:

 

من أدرك عرفة قبل أن يطلع الفجر فقد أدرك الحج]     رواه الترمذي]

 

[Mwenye kuipata arafa kabla ya Alfajiri basi ameipata hija]    [Imepokewa na Attirmidhiy na Amesahihsha Al’albaniy katika swahihil-jaami’ No(5995)]

4. Arafa yote ni uwanja wa kisimamo, na Mtume alisimama kwenye jabali karibu na Swakharaat hali yakueleka kibla na wala hakupanda juu ya jabali Amesema:

 

ووقفت ههنا. وجمع كلها موقف]    رواه مسلم]

 

[Nimesimama hapa na Arafa yote ni sehemu ya kisimamo]  [Imepokewa na Muslim]

ikiwa ataweza kusimama alipo simama Mtume ﷺ ni uzuri na asipo weza atasimama sehemu yoyote, wala haifai kusimama kwenye jangwa wala kupanda jabali,

5. Ni juu ya mwenye kuenda hijja akumbuke kuwa siku ya Arafa ni siku kubwa na ina fadhla kubwa, na Mwenyezi Mungu anawakirimu waja wake, na ajifakhiri mbele ya malaika wake, na nisiku ambao watu huacha huru na moto.

Amesema Mtume ﷺ:

 

ما من يوم أكثر من أن يعتق الله فيه عبدا من النار من يوم عرفة وإنه ليدنو ثم يباهي بهم الملائكة فيقول : ما أراد هؤلاء]   رواه مسلم]

 

[Hakuna siku ambao Mwenyezi Mungu huacha waja wake huru na moto kuliko siku ya Arafa, na siku hiyo Mwenyezi Mungu anakurubia kisha anajifakhirisha na waja wake kwa Malaika, na anasema: wataka nini wajawangu hawa?]    [Imepokewa na Muslim] yatakikana kwa hajji kufaidika na masaa ya siku hii tukufu, na kujadidisha Tawba na kujihisabu nafsi yake wala asipoteze wakati wake kwa kuzunguka ovyo na kuzungumza upuzi na kufanya mijadala.


 

Subcategories

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668589
TodayToday1277
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 19

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6867104ebca9913575685191751584846
title_6867104ebcba48779209881751584846
title_6867104ebcc9c1299173701751584846

NISHATI ZA OFISI

title_6867104ebea4a4797999641751584846
title_6867104ebeb3317429840401751584846
title_6867104ebec1513869341121751584846 Add content here

HUDUMA MPYA

: 2 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com