Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


HALI YA KWANZA:

Awe na ada inayojulikana ya siku zake za hedhi kabla ya kujiwa na istihadhah:

Huyo atahesabu siku za kadiri ya ada yake kuwa ni hedhi na zinazosalia katika mwezi ni istihadhah, kwa hadithi ya ‘Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Fatimah binti Abi Hubaish Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sitwahiriki, je niache kuswali? Mtume akamwambia

 

اجتنبي الصلاة أيام حيضك ثم اغتسلي وتوضئي لكل صلاة ، ثم صلي]     رواه البخاري]

 

[Acha kuswali kadiri ya siku zako za kuingia hedhini, kisha oga na utwadhe kila Swala kisha uswali]    [Imepokewa na Bukhari.].

HALI YA PILI:

Asiwe na ada inayojulikana, lakini anaweza kupambanua baina ya damu ya hedhi na damu ya istuhadhah:
Basi huyu atatumia upambanuzi wake, kwa ilivyothubutu kwamba Fatimah binti Hubaish Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa kwenye damu ya istihadha, Mtume akamwambia:

إن دم الحيض دمٌ أسود يُعرِف، فإذا كان ذلك فأمسِكي عن الصلاة، فإذا كان الآخر فتوضَّئِي وصلِّي]      رواه أبوداود]

 

[Hakika damu ya hedhi, ni damu nyeusi inayojulikana. ikija, acha kuswali, na ikija ile nyingine tawadha na uswali, kwani damu hiyo ni kishipa]   [Imepokewa na Abu Daud.].

HALI YA TATU:

Asiwe na ada Maalumu na asiweze kupambanua:
Basi huyo atatumia ada za wengi wa wanawake, hivyo basi hedhi itakuwa ni siku sita au saba katika kila mwezi, ataanzia mwanzo wa kipindi anapoona damu, na siku zilizosalia zitahesabiwa ni istihadha. Hii ni kwa kauli yake Mtume kumwambia Hamnah binti Jahsh Radhi za Allah ziwe juu yake.

 

فتحيَّضي ستَّة أيَّامٍ أو سبعةً، ثمَّ اغتسلي، فإذا اسْتَنْقَأْتِ فصلِّي أربعةً وعشرين، أو ثلاثةً وعشرين، وصُومي وصلِّي؛ فإن ذلك يُجزئُك، وكذلك فافعلي كما تحيضُ النساءُ   وراه أبوداود والترمذي

 

[Basi hesabu kuwa wewe uko hedhini kwa siku sita au siku saba kisha oga, ukitakasika, basi swali kwa masiku ishirini na tatu na Ufunge na uswali, kwani hilo linakutosheleza. Na ufanye hivyo kama wanavyohidhi wanawake]    [Imepokewa na Abu Daud na At Tirmidhiy.]

Kwa hivyo atafanya kama wanavyotwahirika wanawake wengine, kulingana na nyakati zao za hedhi na utwahara.

HALI YA NNE:

Awe na ada Maalumu na aweze kupambanua:
Huyu atazingatia ada na siyo kupambanua, kwa kuwa ada ina udhibiti zaidi kwa mwanamke. Na anaposahau ada yake basi atatumia upambanuzi.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668258
TodayToday946
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 11

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6866cafe5250913181031541751567102
title_6866cafe525e17673120021751567102
title_6866cafe526ba13983467631751567102

NISHATI ZA OFISI

title_6866cafe5398e14933196811751567102
title_6866cafe53a5a14278092781751567102
title_6866cafe53b2a4264221281751567102 Add content here

HUDUMA MPYA

: 7 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com