SOMO LA FIQHI
MAANA YA ISTIHADHA
Istihadha: Ni kutiririka damu kutoka kwenye tupu ya mwanamke ikawa haikomi kabisa au ikatike kwa kipindi kichache.
TOFAUTI BAINA YA DAMU YA HEDHI NA YA ISTIHADHA
DAMU YA ISTIHADHA | DAMU YA HEDHI |
Nyekundu nyepesi | Nyeusi nzito |
Haina harufu | Ina harufu mbaya yenye kuchukiza |
Inaganda (inashikana) | Haigandi (haishikani) |
Inatoka kwenye kishipa cha uzao cha karibu | Inatoka mwisho wa uzao |
Damu ya kuashiria kasoro, ugonjwa na uharibikaji | Damu ya afya na ya kawaida |
Haina wakati maalumu |
Inatoka wakati maalumu |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.