Menu

Fiqhi


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Kuoga katika sheria lina hekima na faida nyingi, miongoni mwa hizo ni kama zifuatazo :

1. Kupata thawabu

Hii ni kwa sababu Kuoga kwa maana na mtazamo wa kisheria ni Ibaada kwa kuwa ndani yake kuna kutekeleza amri ya sheria na kuitumia hukumu ya sheria.

Kwa hivyo lina hili la utekelezaji amri na hukumu ya sheria ujira mkubwa.

Ni kwa mantiki hii ndio Bwana Mtume akatuambia :

 

الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ]    رواه مسلم]

 

[Twahara ni nusu ya imani]     [Imepokelewa na Muslim.]

Ni vema ikaeleweka wazi kuwa twahara imekusanya udhu, Kuoga, Tayammum na mengineyo.

2. Kuwa Msafi

Muislamu anapokoga, mwili wake hutakasika na kuwa msafi.

Usafi huu ni kinga kubwa ya vijidudu vinavyoweza kusababisha maradhi kama vile upele na humfanya muislamu anukie vema, kitu ambacho humkurubisha na watu kwani watu humteta mtu mchafu anukaye.

Imepokelewa kutoka kwa Bibi Aisha Allah amuwie radhi kwamba amesema :

 

كان أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم عمال أنفسهم، وكان يكون لهم أرواح، فقيل لهم: لو اغتسلتم.]   متفق عليه]

 

[Maswahaba wa Bwana Mtume ﷺ walikuwa wakijifanyia kazi wenyewe (na hawakuwa na watumishi) wakawa na harufu mbaya ya jasho. Wakaambiwa na Mtume

[Lau mngalikuwa mnakoga].    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na katika upokezi mwingine Mtume ﷺ Amesema:

 

[لو اغتسلتم يوم الجمعة]

 

[Lau mngalikuwa mnajitwahirisha kwa ajili ya siku ya Ijumaa].

3. Kuwa mchangamfu na kupata nguvu.

Mwili wa mwanadamu anapokoga huwa na nguvu mpya na kurudia kuwa katika hali ya uchangamfu baada ya ulegevu na uchovu ambao humsababisha uvivu na kutokujisikia kufanya jambo lolote zaidi ya kubweteka bwete!

Hili la kujisikia kuchoka na mwili kunyong’onyea hupatikana zaidi mara tu baada ya tendo la kujamiiana.

Kwa maneno ya jumla, Hikma ya kuoga kwa ajili ya twahara na usafi humuandaa mtu na kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwasiliana na kuzungumza na Mola Muumba wake ndani ya swala akiwa katika hali njema kabisa.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


MAANA YA KUOGA

Neno Kuoga au Josho ni matokeo ya tafsiri ya neno la kiarabu GHUSLU.

Neno hili lina maana mbili; ya kilugha na kisheria.

Kwa mtazamo wa kilughakukoga  ni kuyatiririsha maji kwenye kitu chochote kile kiwacho. Na Maana ya kisheria ni kitendo cha kuyapitisha maji mwili mzima kwa nia maalum kwa kusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu 

HUKUMU NA DALILI YA KUOGA JANABA:

Kuoga janaba kisheria ni Wajibu kwa kila Muislamu akipatwa na mojawapo wa mambo yatakayomlazimisha kukoga kama vile janaba kwa jimai au kukoga, hedhi, nifasi, uzazi na mengineyo kama tutakvyoeleza huko mbele.

Ulazima huu akipatwa na mambo haya ni juu ya kila Muislamu, mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kulitekeleza josho hilo.

Dalili na ushahidi wa Kuoga ni neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُواْ}       المائدة:5}

 

[Na mkiwa na janaba basi ogeni.]    [Al Maaida:6]

Na amesema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ}     البقرة:222}

 

[Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike.]     [Al Baqara:222]

Na dalili za usheria wa Kuoga zinapatikana ndani ya Qur'ani Tukufu, Sunna ya Mtume (Hadithi) na Ijmaai.

Miongoni mwa dalili za josho katika Qur'ani Tukufu :

 

إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}    البقرة:222}

 

[Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha ]    [Al Baqara:222].

Na Katika jumla ya dalili za Kuoga katika sunna ni ile hadithi iliyopopkelewa na Abu Hurayrah radhi za Allah ziwe juu yake amesema, amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:

 

حق على كل مسلم أن يغتسل في كل سبعة أيام يومًا يغسل فيه رأسه وجسده]     متفق عليه]

 

[Ni haki ya kila Muislamu kukoga siku moja katika juma, akaosha kichwa na mwili wake]

[Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Mapendeleo na muradi wa neno haki ni kwamba haifai kwa muislamu kuacha, na wanazuoni wameichukulia siku hiyo kuwa ni siku ya ijumaa.

Ijmaa ya wanazuoni mujitahidi imekongomana na kukubaliana kwamba kukoga kwa ajili ya nadhafa ni jambo lililosuniwa na kukoga kwa ajili ya kusihi ibada ni wajibu na hakuna hata mwanachuoni mmoja aliyelipinga kongamano hili.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Muislamu akiinuka kutoka usingizini na akataka kutawadha kwenye chombo, basi asichote humo kwa mikono yake mpaka aioshe mara tatu, kwa kauli yake Mtume :

 

إذا استيقظ أحدكم من نومه فلا يغمس يده في وضوئه حتى يغسلها ثلاثاً، فإن أحدكم لا يدري أين باتت يده]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Akiamka mmoja wenu kutoka kwenye usingizi, basi na asiuvike mkono wake chomboni mpaka auoshe mara tatu, kwani hujui mkono wake ulilala wapi]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Inapasa mtu awe na pupa la kuyafikisha maji kwenye kila kiungo kinacholazimu kuoshwa, hasahasa kwenye sehemu za baina ya vidole vya mikono na miguu, na baina ya ndevu na mashikio, pia visukusuku, vifundo na visiginyo kwa kauli yake Mtume :

 

وَيْلٌ لِلأَعْقَابِ مِنَ النَّارِ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Ole wa motoni kwa visiginyo]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

3. Asili ni kujengea yakini. Lau mtu alikuwa na yakini kuwa alitawadha kisha akafanya shaka kuwa udhu wake umetanguka, basi atajengea yakini yake nayo ni kuwa ana udhu. Na lau alikuwa na yakini kuwa hana udhu, kisha akafanya shaka: ametawadha au la? Basi yakini ni kuwa yeye hakuwa naudhu.

4. Muislamu anapotawadha, akaosha viungo vinavotakikana kuoshwa kwa mwenye kutawadha, mara mojamoja au mara mbilimbili, au vingine mara moja na vingine mara mbili au mara tatu, udhu wake ni sahihi.

5. Mtu akiswali bila ya udhu kwa kusahau, itamlazimu kurudia Swala anapokumbuka.

6. Mtu akitawadha kisha akaingiwa na njisi, basi ataiondoa najisi wala harudii kutawadha, kwa kuwa kuingiwa na najisi hakutangui udhu.


 


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Kuleta nia kwa sauti wakati wa kutawadha.

2. Kutumia maji kwa kupita kiasi.

3. Kuzidisha maosho matatu katika kutawadha, kwa riwaya iliyopokewa kuwa mbedui alikuja kwa Mtume kumuuliza juu ya kutawadha, akamuonesha udhu mara tatutatu kisha akasema:

 

هَكَذَا الْوُضُوءُ، فَمَنْ زَادَ عَلَى هَذَا فَقَدْ أَسَاءَ وَتَعَدَّى وَظَلَمَ]      رواه أبوداود والنسائي وأحمد]

 

[Kutawadha ni namna hii. Na mwenye kuzidisha hapo amekosea, amepita mpaka na amedhulumu]  [Imepokewa na Abu Daud na Annasai na Ahmad.]

Lakini inafaa kuongeza zaidi ya maosho matatu iwapo atakuwa hakukisafisha kiungo kwa maosho matatu, kama mtu aliyeingiwa na mafuta au kitu kingine mkononi.

4. Kutoeneza maji katika kutawadha, kwa riwaya iliyopokewa kuwa mtu alitawadha, akaacha paku kadiri ya ukucha kwenye nyayo, Mtume akaliona na aksema: [Rudi utawadhe kwa uzuri]   [ Imepokewa na Muslim.] akarudi kisha akaswali.

Na inaingia kwenye kukosa kueneza maji ya udhu:

a- kutoosha vifundo viwili vya miguu

b- kutoosha visukusuku kwa sababu ya wembamba wa mikono ya kanzu.

c- kutoosha weupe ulioko baina ya masikio na ndevu.

d- Kutoosha kitanga cha mkono wa kushoto pamoja na mkono wa kushoto.

e- mwenye kutawadha naye una mapaku ya mafuta.

f- kutawadha kwa mwanamke na juu ya vidole vyake pana pambo lenye kuzuia maji kufika kwenye ngozi.

g- kutofikisha maji kwenye vidole vya miguu iwapo maji hayapiti baina ya vdole.

5. Kupangusa shingo:

Si miongoni mwa matendo ya kutawadha,

6. kuleta dhikiri ambazo hazikuja katika Sheria, mfano:

a- kuomba dua maalumu katika kuosha kila kiungo.

b- kumwambia “zamzam” mwenye kutawadha.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Tunakusudia kusema kwa istilahi (wenye udhuru) wale watu ambao ambao wana maradhi yanayowafanya wasiweze kuuhifadhi udhu wao kama wanavyoweza watu wengine katika hali ya kawaida.

Hawa ni pamoja na mtu mwenye maradhi ya mchuchuro wa mkojo, hawezi kuuzuia mkojo, saa zote hutokwa na mkojo au anatokwa na upepo (ushuzi) mara kwa mara.

Au mwanamke aliyepatwa na maradhi ya kutokwa na damu ya mbobo/ugonjwa, hii ni damu itokayo kwa wingi katika wakati usiokuwa wa damu ya ada ya kila mwezi (hedhi).

Hukumu ya udhu wa watu hawa ni kwamba wanatakiwa watawadhe kila unapoingia wakati wa kila swala, wasitawadhe kabla ya kuingia wakati kwa kuwa wanatakiwa kufululiza baina ya udhu na swala.

Hii ni kwa sababu kisheria hawana udhu kwani wana hadathi ya kudumu na udhu wao ni wa ruhusa maalum waliyopewa na sheria ili waweze kuyatekeleza yale yote yasiyotekelezeka bila ya udhu, kama vile swala, tawafu na kadhalika.

Wataswali kwa udhu huo swala wazitakazo za suna au za fardhi.

Udhu wa watu hawa utabatilika na kutenguka mara tu unapoingia wakati wa swala nyingine. Akitaka kuswali basi itamlazimu kutawadha tena.

Haya yote yanaonyesha wepesi wa sheria ya Kiislamu ambayo imejengwa juu ya misingi ya wepesi na kuondosha uzito na ugumu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu :

 

 وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ}   الحج:22}

 

[Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim.]   [22:78].


Subcategories

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668589
TodayToday1277
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 19

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6867104ebca9913575685191751584846
title_6867104ebcba48779209881751584846
title_6867104ebcc9c1299173701751584846

NISHATI ZA OFISI

title_6867104ebea4a4797999641751584846
title_6867104ebeb3317429840401751584846
title_6867104ebec1513869341121751584846 Add content here

HUDUMA MPYA

: 4 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com