Menu

Fiqhi


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Makosa na matanabahisho katika kuzuru

1. Kusafiri na kujisumbua kwa safari kwa lengo la kuzuru kaburi na sehemu za turathi zilizoko Madina. Lililowekwa na Sheria ni kufunga safari kuuzuru Msikiti wa Mtume , na ziyara ya kaburi yake inaingia ndani.

2. Kuelekea upande wa kaburi Wakati wa kuomba Dua

3. Kumuomba Mtume na kutaka haja kwake, badala ya Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na Aliyetukuka, ni miongoni mwa ushirikina mkubwa kabisa.

4. Kujipukusa na kuta za Chumba alichozikwa Mtume ndani yake kwa lengo la kupata baraka ni miongoni mwa mambo ya uzushi yaliyoharamishwa na ni miongoni mwa njia zinazopelekea kwenye ushirikina.

5. Kuinua sauti kwenye kaburi ya Mtume na kisimamo kirefu, na kukariri salamu kwa mbali kila anapoingia na kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto juu ya kifua wakati wa kutowa salamu kama vile anavyo fanya akiwa kwenye Swala.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


ADABU YA KUZURU MSIKITI WA MTUME ﷺ

1. Mwenye kuzuru afikapo msikitini ni sunna kwake atangulize mguu wake wa kulia na aseme:

 

اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ]    رواه مسلم]

 

[Ewe Mola! Nifungulie milango ya rehema zako]    [Imepokewa na Muslim.].

2. Ataswali rakaa mbili za kuuamkia msikiti, na ikiwa ataziswali kwenye sehemu ya Raudha (Bustani ya Pepo) basi ni bora zaidi.

3. Ni sunna kuizuru kaburi ya Mtume na marafiki zake wawili: Abu Bakr kisha ‘Umar.

4. Ni sunna kwa mwenye kuuzuru Msikiti wa Mtume aswali Swala Tano ndani ya Msikiti wa Mtume, na amtaje Mwenyezi Mungu na kumuomba kwa wingi na kuswali sunna ya ziada hasa-hasa kwenye sehemu ya Raudha tukufu.

5. Ni sunna azuru msikiti wa Baqii’ kwa ajili ya kuswali humo, ingawa kuuzuru siku ya Jumamosi ni bora zaidi, kwa Hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:

 

كَانَ رَسُولُ اللهِ يَأْتِي مَسْجِدَ قُبَاءٍ رَاكِبًا وَمَاشِيًا فَيُصَلِّى فِيهِ رَكْعَتَيْنِ» وفي لفظ: «كَانَ يَأْتِي قُبَاءً» يَعْنِي كُلَّ سَبْتٍ]   رواه مسلم]

 

[Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akienda kwenye msikiti wa Qubaa’ akiwa anapanda na akiwa anatembea, na akiswali hapo rakaa mbili]. Na katika tamshi lingine: (Alikuwa akiujia msikiti wa Qubaa, yaani: siku ya Jumamosi]  [Imepokewa na Muslim.].

6. Ni sunna kuzuru makaburi ya Baqii’ [ Baqii’: ni mahali ambapo Mswahaba wengi walizikwa hapo.], makaburi ya mashahidi na kaburi ya Hamza, kwa kuwa Mtume alikuwa akiwazuru na kuwaombea na kusema:

 

السلام عليكم أهلَ الديار من المؤمنين والمسلمين، وإنا إن شاء الله بكم لَلَاحقون، أسأل الله لنا ولكم العافية]   رواه مسلم]

 

[Amani iwashukie nyinyi watu wa nyumba za Waumini na Waislamu. Na sisi, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni wenye kukutana na nyinyi. Tunajiombea Mwenyezi Mungu uzima na tunawaombea na nyinyi]    [Imepokewa na Muslim.].



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Majina ya mji wa Mtume wa Madina
1. Madina:
Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

 

8:يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ}   المنافقون}

 

[Wanasema: lau tutarudi Madina watawatoa walio watukufu zaidi wale walio wanyonge zaidi]    [63: 8].

2. Twaba:
Amepokewa Jabir bin Samurah Radhi za Allah ziwe juu yake akisema:

 

إِنَّ الله تَعَالَى سَمَّى الْمَدِينَةَ طَابَةَ]     رواه مسلم]

 

[Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu  akisema: [Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ameipa Madina jina la Twaba]   [Imepokewa na Muslim.].

3. Twayiba:
Amepokewa Zaid bin Tahabit Radhi za Allah ziwe juu yake akisema akipokea kutoka Mtume (saw) akisema:

 

إِنَّهَا طَيْبَةُ، تَنْفِي الذُّنُوبَ كَمَا تَنْفِي النَّارُ خَبَثَ الْفِضَّةِ]    متفق عليه]

 

[Hiyo ni Twayiba, inaondoa dhambi kama ambapo moto unaondoa uchafu wa fedha] [Imepokewaq na Bukhari na Muslim.].

Fadhila za mji wa Mtume

1. Sa'ad bin Abii Waqqaasw Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:

 

الْمَدِينَةُ خَيْرٌ لَهُمْ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ، لَا يَدَعُهَا أَحَدٌ رَغْبَةً عَنْهَا إِلَّا أَبْدَلَ الله فِيهَا مَنْ هُوَ خَيْرٌ مِنْهُ، وَلَا يَثْبُتُ أَحَدٌ عَلَى لَأْوَائِهَاِ  وَجَهْدِهَا إِلَّا كُنْتُ لَهُ شَفِيعًا أَوْ شَهِيدًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ 

[Madina ni bora kwao lau walikuwa wanajua. Haiachi mtu yoyote kwa kutoipenda isipokuwa Mwenyezi Mungu humweka mtu bora kuliko yeye awe ni badala yake. Na yoyote atakayevumilia shida zake na usumbufu wake, nitakuwa ni muombezi wake au shahidi wake Siku ya Kiyama]    [Imepokewa na Muslim.].

2. Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kwamba Mtume amesema:

 

أُمِرْتُ بِقَرْيَةٍ تَأْكُلُ الْقُرَى يَقُولُونَ يَثْرِبُ وَهْيَ الْمَدِينَةُ، تَنْفِي النَّاسَِ كَمَا يَنْفِي الْكِيرِ خَبَثَ الْحَدِيدِِ.]  متفق عليه]

 

[Nimeamrishwa kwenye kitongoji (nimeamrishwa nigurie hapo, niteremkie hapo na niishi hapo.) kinachokula vitongoji (watu wake wata washinda watu wa miji mingine na kitakuwa ni kituo cha majeshi ya Kiislamu.), wanakiita Yathrib, nayo ni Madina, inawaondoa watu , kama vile kiriba kinvyoondoa uchafu wa chuma]  [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].


 


SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Hukumu ya kuzuru Msikiti wa Mtume ﷺ

Kuuzuru Msikiti wa Mtume si miongoni mwa masharti ya Hija wala nguzo zake wala wajibu zake. Hilo ni sunna, na inafaa ifanywe wakati wowote.

Na ni wajibu liwe lengo la ziara ni kuswali kwenye huo Msikiti na sio kaburi. Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kumpokea Mtume kuwa alisema:

 

لَا تُشَدُّ الرِّحَالُ إِلَّا إِلَى ثَلَاثَةِ مَسَاجِد: الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ، وَمَسْجِدِ الرَّسُولِ ﷺ ، وَالمَسْجِدِ الأَقْصَى]    رواه مسلم]

 

[Hakufungwi safari isipokuwa kwenda kwenye misikiti mitatu: Msikiti wa Haram, Msikiti wa Mtume na Msikiti wa Aqswa]    [Imepokewa na Muslim.].

Amesema Shekhe wa Uislamu Ibnu Taimiyya: “Iwapo lengo lake la safari ni kuzuru kaburi ya Mtume na sio kuswali kwenye Msikiti wake…. Basi msimamo wa maimamu na wengi wa wanavyuoni ni kuwa hili halikuwekwa na Sheria wala halikuamrishwa…Na Hadithi kuhusu kuzuru kaburi ya Mtume zote ni dhaifu kwa itifaki ya wajuzi wa Hadithi, bali ni Hadithi zilizobuniwa. Hakuna yoyote miongoni mwa wakusanyaji wa Vitabu vya Sunna za Mtume aliyepokea Hadithi hizo, na hakuna yoyote aliyesimamisha hoja kutegemea hadithi yoyote katika hizo” [Majmuu’ al- Fataawaa, juzu. ii, uk. 26].



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Maana ya mnyama wa Udh’hiya

Ni yule anayechinjwa miongoni mwa wanyama howa siku za idd ya kuchinja kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

Hukumu ya kudhahi
Ni sunna iliyotiliwa mkazo, kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنۡحَرۡ}   الكوثر: 2}

 

[Basi mswalie Mola wako na uchinje]   [108: 20].

Na kwa Hadithi ya Anas Radhi za Allah ziwe juu yake:

 

أن النبي ﷺ ضَحَّى بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ ، ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ، وَسَمَّى وَكَبَّرَ، وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا]   رواه الترمذي]

 

[Kwamba Mtume alidhahi (alichinja) kondoo wawili wazuri  [ Amlah: Mnyama mwenye weupe na weusi, na weupe ukawa ni mwingi zaidi.] wenye pembe  Aliwachinja kwa mkono wake. Akapiga bismillahi na akaleta takbiri na akaweka guu lake juu mbavu zao]             [Imepokewa na Tirmidhi].

Wakati wa kuchinja mnyama wa Udh’hiya

Wakati wa kuchinja unaanza baada ya Swala ya Idd ya kuchinga mpaka jua la siku ya mwisho wa siku za Tashriiq kuzama (Siku ya kumi na moja, kumi nambili na kumi na tatu za mwezi wa Mfungotatu).

Mnyama wa Udh’hiya anayetosheleza
1. Mbuzi au kondoo mmoja anamtosheleza mtu mmoja. Na anaweza kumshirikisha anayemtaka katika thawabu, kwa kuwa Mtume alipotaka kuchinja mnyama wake wa kudhahi alisema:

 

[بِاسْمِ اللهِ، اللَّهُمَّ تَقَبَّلْ مِنْ مُحَمَّدٍ، وَآلِ مُحَمَّدٍ، وَمِنْ أُمَّةِ مُحَمَّدٍ]    [متفق عليه]

 

[Bismillahi. Ewe Mola mtakabalie Muhammad na jamaa za Muhammad na umma wa Muhammad]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Ngamia mmoja na Ng’ombe mmoja wanawatosheleza watu saba.  Yafaa kwa watu saba kushirikiana katika Ngamia au Ng’ombe, kwa kauli ya Jabir:

 

فَأَمَرَنَا رَسُولُ اللهِ أَنْ نَشْتَرِكَ فِي الإِبِلِ وَالْبَقَرِ، كُلُّ سَبْعَةٍ مِنَّا فِي بَدَنَةٍ ( البدنة: هي الناقة، ذكرا كانت أو أنثى) ]. رواه مسلم]

 

[Akatuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu tushirikiane katika ngamia na ng’ombe, kila watu saba miongoni mwetu kwa ngamia mmoja (Badanah: ni ngamia, awe ni mwanamke au mwanamke.) ]    [Imepokewa na Muslim.].

Miaka ya mnyama inayotosheleza kwa Udh’hiya

Jadha› wa kondoo: Naye ni mwenye miezi sita.

Thanii wa mbuzi: ni mwenye mwaka mmoja.

Thanii wa ng’ombe: ni mwenye miaka miwili.

Thanii wa ngamia: ni mwenye miaka mitano.

Mnyama bora wa Udh’hiya
Mnyama bora ni ngamia ikiwa atatolewa mzima kwa sababu thamani yake iko juu na nimanufaa kwa mafakiri kisha ni Ngo;mbe ikiwa atatolewa mzima kisha Mbuzi, kisha fungu la saba la Ngamia kisha fungu la saba la Ngo’mbe

Aibu za mnyama wa Udh’hiya
1. Aibu zinazozuia kutosheleza [Inazuilia kutosheleza: Haisihi kumchinja kama mnyama wa kudhahi.]
‹Awraa’: Ni mnyama mwenye ila machoni mwake, na anaingia ndani ya huyo mnyama kipofu.

‹Arjaa›: Ni mnyama asiyeweza kutembea.

‹Ajfaa’: Ni mnyama aliyekonda asiye na mafuta.

Mgonjwa ambaye ugonjwa wake uko wazi:

Dalili ya hayo ni Hadithi iliyopokewa na Baraa bin Aazib Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema: 

 

لَا يَجُوزُ مِنَ الضَّحَايَا الْعَوْرَاءُ الْبَيِّنُ عَوَرُهَا، وَالْعَرْجَاءُ الْبَيِّنُ عَرَجُهَا، وَالْمَرِيضَةُ الْبَيِّنُ مَرَضُهَا، وَالْعَجْفَاءُ الَّتِي لَا تُنْقِي [ لا تنقي: أي ليس فيها مخ]ِ   . رواه مسلم

 

[Haifai kudhahi kwa mnyama mwenye jicho moja ambaye kasoro katika jicho lake iko wazi, na mnyama kiguru ambaye kiguru chake kiko wazi, na mngonjwa ambaye ugonjwa wake uko wazi, na aliyekonda asiye na mafuta   [ Laa tanqii: hana bongo.] ]  [Imepokewa na Muslim.]

Na zinakutanishwa na hizi, aibu ambazo hufanana na hizi au ni mbaya zaidi kuliko hizi.

2. Aibu zisizozuia kutosheleza kudhahi
AL-Batraa›: Asiye na mkia.

AL-Jammaa›: asiye na pembe kimaumbile.

AL-Khaswiyy: Kondoo ailiyekatwa konde zake za dhakari.

Alie na mpasuko kwenye sikio lake au tundu, au pembe yake imevunjika.

Haya yaliyotajwa kuhusu kinachotosheleza katika kudhahi ndiyo hayo hayo kuhusu tunuku na fidia.

Kugawanya nyama ya Udh’hiya
Imeruhusiwa na sharia kwa mwenye kudhahi ale theluthi ya nyama yake, na akiitoa sadaka yote inafaa, na akila nyingi ya ile nyama pia inafaa.

Faida
Mwenye kutaka kudhahi, haifai akate nywele zake na kucha zake na kitu chochote mwilini mwake ungiapo mwezi wa Mfungotatu mapaka achinje. Hii ni kwa hadithi iliyopokewa na Ummu Salama Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume alisema:

 

إِذَا دَخَلَتِ الْعَشْرُ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّىَ فَلاَ يَمَسَّ مِنْ شَعَرِهِ وَبَشَرِهِ شَيْئًا]    رواه مسلم]

 

[Zinapoingia Siku kumi (za mwezi wa mfungo tatu) na akataka mmoja wenu kudhahi, basi asiondowe chochote katika nywele zake na mwili wake]   [Imepokewa na Muslim.].

Ama wale ambao wanafanyiwa tendo la kudhahi, kama mke na watoto, si haramu kwao kuondoa nywele au uchafu wa mwilini kama kucha.


Subcategories

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6669050
TodayToday187
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 16

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_686774e080abd14791831221751610592
title_686774e080ba810313685471751610592
title_686774e080c8920998439151751610592

NISHATI ZA OFISI

title_686774e0822496786258031751610592
title_686774e08231f5664734651751610592
title_686774e0823f6213873201751610592 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com