Menu

Fiqhi


SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


1. Kula na kunywa kwa kukusudia ndani ya mchana wa Ramadhani
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ}    البقرة:187}

 

[Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni saumu mpaka usiku]    [Al-Baqarah – Aya 187]

MAS'ALA 

Je yafaa mtu kula kwasababu ya kazi?
Yoyote anayefanya kazi mahali pa mapishi ya mikate hivi na mahali pa kazi ngumungumu sio ruhusa kwao kutofunga (yaani hawafai kula mchana wa Ramadhani); kwasababu wamelazimika kama watu wengine kufunga Ramadhani.

 

MAELEZO 

Atakaye kula au kunywa kwa kusahau basi saumu yake imeswihi (iko sawa haina tatizo lolote), na inamlazimu kujizuia na vitu vinavyoharibu saumu pindi anapokumbuka; kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

من نسي  وهو صائم - فأكل أو شرب فليتمّ صومه ، فإنما أطعمه الله وسقاه]     رواه مسلم]

 

[Aliyesahau hali ya kuwa amefunga akala na kunywa, basi akamilishe saumu yake, kwani Mwenyezi Mungu amemlisha na kumnywesha (mtu huyo)]     [Imwpokewa na Muslim.].

- Kinaharibu saumu chochote kile kinachoingia tumboni kwa njia ya mdomoni au puani, na chochote kinachofahamika kuwa chakula au kinywaji, kama vile sindano za lishe/chakula. Ama sindano ambazo si za chakula, kama penicillin na mfano wake, hazifunguzi saumu, kwasababu sio chakula wala kinywaji, wala sio kwa maana ya chakula.

- Chochote kinachoingizwa mdomoni kwa ajili ya kutizama kitu na vipuliza hewa vya kutibu pumu na mfano kama huu, hakiharibu saumu.

- Wanja, na matone ya kitu majimaji kutonezwa kwenye jicho na sikio na mfano wa hivi viwili havivunji saumu, kwasababu hakuna dalili ya vitu hivi kuharibu saumu, na kwasababu jicho sio sehemu inayotegemewa kwa kuingilia chakula na kinywaji, na vile vile matone ya kitu majimaji kwenye sikio na puani, lakini ubora kwa haya matone ni kujitenga nayo, kwa jinsi alivyokataza Mtume kuhusu kupita mpaka katika kupandisha maji puani kwa aliyefunga, [Imwpokewa na Tirmidhi.] na kwasababu ni sehemu inayopitisha chakula hadi tumboni.

- Anapotumia mtu kitu ambacho hakiliwi au kinadhuru, kama vile sigara basi atakuwa amefungua, kwasababu amekitumia kupitia sehemu inayotumika kwa chakula, nayo ni mdomo, kama nayo itakavyofahamika kuwa chakula ama kinywaji.

- Hakiharibu saumu kitu ambacho kwamba huwezi kukiepuka, kama vile vumbi la njiani, na mabaki ya chakula yaliosalia kati ya meno.

Dawa inayotumika kama chakula inaharibu saumu.Sindano ya penicillin haiharibu saumu.(Hii ni sindano ya kukinga au kutibu madhara yanayosababishwa na bacteria).Vipuliza hewa vya kutibu pumu haviharibu saumu.Wanja haiharibu saumu.Sigara zinaharibu saumu.Mabaki ya chakula yaani katika meno hayaharibu saumu.

2. Kufanya Tendo la Ndoa
Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ}    البقرة:187}

 

[Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuingiliana na wake zenu]   [Al-Baqarah – Aya 187].

Na “Ar-Rafath” ni neno la kiarabu lililotumika katika Aya hii kumaanisha kuingiliana – yaani kufanya tendo la ndoa, basi yoyote atakaye ingiliana na mkewe au mumewe hali ya kuwa amefunga, saumu yake itakuwa imeharibika, na atalazimika ailipe siku hiyo, na pamoja na kuilipa ni juu yake kutoa kafara nzito, nayo ni kuacha huru mtumwa, akiwa hatopata mtumwa wa kumuacha huru, atalazimika kufunga miezi miwili mfululizo, na akiwa hawezi kufunga atalazimika kulisha masikini sitini, kama ilivyothibiti kutoka kwa Abu Hurerah radhi za Allah ziwe juu yake Anasema:

 

جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه وسلم فقال: هلكت، قال: وما شأنك، قال: وقعت على امرأتي في رمضان، فقال: هل تجد ما تعتق رقبة. قال: لا، قال: فهل تستطيع أن تصوم شهرين متتابعين، قال: لا، قال: فهل تستطيع أن تطعم ستين مسكيناً، قال: لا أجد، فأتى النبي صلى الله عليه وسلم بعرق فيه تمر، فقال: خذ هذا فتصدق به، فقال: أعلى أفقر منا؟ ما بين لابتيها أفقر منا، ثم قال: خذه فأطعمه أهلك.      رواه البخاري ومسلم

 

[Alikuja mtu mmoja kwa Mtume ﷺ akasema nimeangamia. Mtume akamuuliza: Una nini? Akajibu: Nimemuingilia mkewangu ndani ya Ramadhani. Mtume akamuuliza: Waweza kuacha mtumwa huru?. Akajibu: Siwezi.. Mtume akamuuliza: je waweza kufunga miezi miwli mfululizo? Akasema: Siwezi. Mtume akamuuliza: Basi waweza kulisha masikini sitini?. Akasema: Siwezi. Mtume akamwambia: Kaa. Akakaa. Mtume ﷺ akaleta chombo ambacho ndani yake mna tende. Akasema: Chukua (hiki chombo) wende ukatolee sadaka. Akasema yule mtu: Je kuna fakiri zaidi yetu? (yaani maskini kuliko familia yake). Mtume akacheka mpaka yakaonekana magego ya meno yake, akasema: Lisha familia yako ( hizo tende)]    [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].

MAELEZO 

Na inakuwa kafara inafuata mfumo huu, hivyo basi mtu asilishe maskini isipokuwa akiwa hawezi kufunga hiyo miezi miwili mfululizo, wala asifunge isipokuwa ikiwa hawezi kuacha huru mtumwa.

 

JE MWANAMKE ANALAZIMIKA KUTOA KAFARA?

Na inamlazimu mwanamke kutoa kafara ikiwa ameridhiana na mumewe kufanya tendo la ndoa, na iwapo amelazimishwa na mumewe kuingiliana basi saumu yake imeharibika na itamlazimu mwanamke huyo kuilipa saumu hiyo peke yake bila ya kutoa kafara.

 

JE KUJITOA MANII KWA MKONO KUNALAZIMU KAFARA?

Na ni katika maana ya jimai (tendo la ndoa) kujitoa manii kwa kukusudia, Mtu akitokwa na manii kwa kubusiana, au kwa kugusa au kwa kutumia mkono, basi saumu yake itaharibika, kwa sababu hiyo ni katika shahawa inao haribu saumu, na itakuwa ni juu yake kuilipa saumu yake wala hatolazimika kutoa kafara, kwa sababu kafara imekuja kwa tendo la ndoa peke yake.

Mtu akibusu au akigusa au akifikiria akatokwa na madhii saumu yake ni swahihi. kwa kutokuwa na dadili yakuharibu saumu kwa kutokwa na madhi

Mtu anapo lala akaota, au akatokwa na manii bila ya shahawa kama kuwa mgonjwa, saumu yake ni swahihi kwa sababu hayakutoka kwa hiyari yake.

Mtu anapo amka na janaba la tendo la ndoa kabla ya alfajiri au akaota, saumu yake ni swahihi na ni juu yake kuoga ili apate kuswali alfajiri na jamaa, imethubutu kutoka kwa bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume :

 

أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كان يُصبح جُنُبًا من جماعٍ ثم يغتَسِلُ ويصوم]     متفق عليه]

 

[Alikuwa akiingiliwa na Alfajiri na yeye akiwa na janaba la mkewe, kisha akioga na akifunga.]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

3. kujitapisha kwa kusudi
Nao ni mtu kutoa kilichoko tumboni kutokana na chakula au kinywaji kwa njia ya mdomo kwa kusudi, ama akishindwa na akatoka bila ya khiyari yake haiathiri saumu yake kwa neno lake Mtume :

 

من ذرعه القيء فليس عليه قضاء، ومن استقاء عمدا فليقض]     رواه أبو داود والترمذي وغيرهما وصححه الحاكم]

 

[Mwenye kushindwa na matapishi basi hana haja ya kukidhi na mwenye kujitapisha kwa kusudi basi alipe]     [Imepokewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na kusahihishwa na Al Haakim]

4. Damu ya Heidhi na Nifasi

Wakati wowote mwanamke atakapo ona damu ya hedhi au nifasi japo kuwa ni wakati wa jioni kabla ya kutwa jua kwa mda mchache saumu yake itaharibika na atawajibika kuilipa

 

 SUALA: JE KUUMIKA HUVUNDA SAUMU?

Kauli yenye nguvu ni kuwa kuumika hakuvundi saumu kwa sababu Mtume ﷺ Aliumika na hali yakuwa amefunga, Amepokewa kutoka kwa said Al’khudriy radhi za Allah ziwe juu yake akisema

 

رخص رسول الله في القبلة للصائم والحجامة]     أخرجه الدارقطني]

 

[Aliruhusu Mtume wa Mwenyezi Mungu Kubusu kwa aliyefunga na kuumika,]     [Imepokewa na Al Daarqutniy]. Lakini inachukizwa kuumika kwa ajili ya kudhofika,

 

سئل أنس بن مالك هل كنتم تكرهون الحجامة للصائم؟ قال : لا ، إلا من أجل الضعف]      رواه البخاري]

 

[Aliulizwa Anas bin Maalik radhi za Allah ziwe juu yake Mulikuwa mukichukiza kuumika kwa alie funga? Akasema la ila kwa ajili ya kudhofika.]     [Imepokewa na Bukhari]

Haidhuru mtu kutokwa na damu katika jaraha, au kung’oa jino au kutokwa na damu za puwa, au kutoa damu kwa ajili ya kujipma, au kujitolea, yote haya hayaharibu saumu.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Kupitisha mpaka katika kusukutuwa na kupandisha maji puani.
Na hii ni kwa ajili ya kuhofia maji yasije yakaingia tumboni mwake, kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

وبالغ في الاستنشاق إلا أن تكون صائما]      رواه أبوداود والترمذي]

 

[Na fanyeni sana katika kupandisha maji puani isipokuwa wakati mtu amefunga saumu] [Imwpokewa na Abuu Daud na Tirmidhiy.]

2. Kumpiga busu kwa matamanio ya kimapenzi.

Inachukizwa kwa aliyefunga saumu ikiwa anachelea nafsi yake kutokwa na manii au kusisimukwa kwa matamanio ya kimapenzi.

Na ni juu ya aliyefunga kujiepusha na kila ambalo litampelekea kusisimukwa na kuleta harakati za kuibuka matamanio ya kimapenzi, na ikiwa anaamini nafsi yake kwamba haitompelekea katika hisia za matamanio ya kimapenzi basi hakuna kosa kwake kum’busu mkewe au mke kumbusu mumewe; kutoka kwa Bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake anasema:

 

كان يقبل وهو صائم، وكان أملككم لإربه]     متفق عليه]

 

[Alikuwa Mtume ﷺ akipiga busu hali yakuwa amefunga na alikuwa ni m’bora zaidi kuliko nyinyi katika kumiliki matamanio ya kimapenzi]     [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].

Na kwa ajili hii inachukizwa kubashiriana kimapenzi kwa kijana kinyume na mzee kwa kuwa kijana damu yake ni moto zaidi, kutoka kwa Abu Hureirah anasema:

أن رجلا سأل النبي صلى الله عليه وسلم عن المباشرة للصائم فرخص له، وأتاه آخر فسأله فنهاه، فإذا الذي رخص له شيخ والذي نهاه شاب.    رواه أبوداود 

 

[Kwamba kuna mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ kuhusu kubashiriana mke na mume kwa aliyefunga, Mtume akampa ruhusa ya kufanya hivyo, na akaja mwengine akauliza (swali hilo hilo), Mtume akamkataza, kwani yule aliyempa ruhusa alikuwa ni mzee, na yule aliyemkataza alikuwa ni kijana.]   [Imwpokewa na Abuu Daud.]



SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


1. Kuoga, na kukaa mahali penye maji ili kupata baridi.

2. Kumeza mate na makohozi.

3. Kuonja chakula ili kujua kiwango cha sukari au chumvi yake kwa kutumia ulimi peke yake, kwa sharti asiingize chochote katika chakula hicho hadi kwenye koo.

4. Kunusa harufu ya manukato na visafisha hewa.

FAIDA

Matumizi ya mswaki kwa mtu aliyefunga
Yaruhusiwa kutumia mswaki kwa mtu aliyefunga wakati wowote ule, sawasawa iwe ni kabla ya kuzama kwa jua kwa kuingia jioni au baada ya hapo, na vilevile uwe mswaki wenyewe uko majimaji au mkavu, lakini anatahadharishwa aliyefunga ikiwa mswaki anaotumia uko majimaji kusije kukaingia chochote kooni wakati anapiga mswaki; kwa sababu kuingia kwa kitu kooni kunaharibu saumu yake.



SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


1. Kula daku na kuchelewesha kula daku hadi karibu sana na kuadhiniwa alfajiri
Kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

تسحروا فإن في السحور بركة]      رواه البخاري ومسلم]

 

[Kuleni daku, hakika katika kula daku kuna Baraka]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na inahesabika kula daku kwa kupatikana chakula kingi au kidogo, hata kama ni tama la maji kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

السُّحُورُ أَكْلَةٌ بَرَكَةٌ فَلا تَدَعُوهُ وَلَوْ أَنْ يَجْرَعَ أَحَدُكُمْ جَرْعَةً مِنْ مَاءٍ فَإِنَّ اللَّهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى الْمُتَسَحِّرِينَ]     رواه أحمد]

 

[Daku uchache wake ni baraka, basi msiache kula daku, hata kama atakunywa mmoja wenu tama la maji, kwani Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanawaswalia wenye kula daku]   [Imepokewa na Ahmad.]

Na inapendekezwa kuchelewesha kula daku, kutoka kwa Zaid ibn Thaabit radhi za Allah zimfikie yeye Anasema:

 

تَسَحَّرْنَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثُمَّ قَامَ إِلَى الصَّلَاةِ قُلْتُ كَمْ كَانَ بَيْنَ الْأَذَانِ وَالسَّحُورِ قَالَ قَدْرُ خَمْسِينَ آيَة]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Tulikula daku pamoja na Mtume ﷺ, kisha tukasimama kuswali (yaani swala ya alfajiri), anasema Anas ibn Malik: nikasema: ilikuwa ni kipindi cha mda gani kati ya kula kwenu hiyo daku na kuswali? Akasema: kiwango cha (kusoma) Aya hamsini)]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

FAIDA

Kunywa wakati adhana inapo adhiniwa

Mtu anaposikia adhana na kinywaji chake kipo mkononi mwake basi anaruhusiwa kunywa hadi amalize; kutoka kwa Abu Hureirah anasema: Amesema :

 

إذا سمع أحدكم النداء والإناء على يده فلا يضعه حتى يقضي منه حاجته]     رواه أبوداود]

 

[Atakaposikia mmoja wenu adhana na hali ya kuwa chombo cha kunywea maji kipo mkononi mwake basi asikiweke kando mpaka amalize haja yake ya kutumia hicho chombo]   [Imepokewa na Abuu Daud.]

Na wanazuoni wamesema kuhusu hadithi hii ni kwa Yule ambae ana shaka kutokeza kwa alfajiri, ama akihakikisha kuwa alfajiri imetokeza kwa huyu hafai kuendelea kula wala kunywa, na akiendelea kufanya hivyo Saumu yake imebatilika na itamlazimu Ailipe

2. Kufanya haraka katika kufungua saumu.
Yapendekezwa kwa aliyefunga kufanya haraka kufungua saumu yake pindi tu anapohakikisha kwamba jua limezama na kuingia jioni.; kwa kauli ya Mtume:

 

لا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الْفِطْر]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Watu wangali katika kheri pindi wanapoharakisha kufungua saumu zao.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

FAIDA

Na inapendekezwa mtu kufungua saumu kwa rutab (tende tosa), asipopata rutab basi afungue kwa tende, na hizo tende ziwe ni hesabu isiyogawanyika kwa mbili (kama vile tende moja, tatu, tano na mfano huu), asipopata tende basi na anywe matama ya maji; kulingana na hadithi ya Anas ibn Malik, anasema: “Alikuwa Mtume ﷺ anafungua saumu kwa Rutab (Tende Tosa) kabla hajaswali, na ikiwa hakuna Rutab basi alikuwa akifungua kwa tende kidogo hivi, na ikiwa hakuna tende alikuwa akinywa [ Hasaa: alikunywa.] matama ya maji” [Imepokewa na Tirmidhi.].

Na akiwa hakupata kitu chochote cha kufungulia saumu basi atanuia kufungua saumu kwa moyo wake, na hili litamtosheleza kwamba amefungua.

 

MAS'ALA

Atakae Funguwa kwa bahati mbaya
Atakapo kula mtu aliyefunga hali ya kudhania kwamba jua limezama na kuingia jioni, au kwa kutoelewa kutokeza kwa alfajiri, kisha ije kum’bainikia kinyume na alivyodhania, basi haimlazimu kwake kuilipa saumu hiyo; kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukfu:

 

:5لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ}    الأحزاب}

 

[Wala si lawama juu yenu mkikosa, lakini (kuna lawama) katika yale ziliyoyafanya nyoyo zenu kwa kusudi ]     [ Al-Ahzab- Aya 5]  

Na kauli yake Mtume :

 

إن الله تـجاوز لي عن أمتي الـخطأ والنسيان وما استكرهوا عليه]      رواه إبن ماجة والبيهقي]

 

[Hakika ya Mwenyezi Mungu amewaondoshea umma wangu (hawaandikiwi madhambi) kwa jambo watakalolikosea bila ya kukusudia na kwa watakayofanya kwa kusahau, na kwa watakayolazimishwa kufanya]  (hali ya kuwa wao wenyewe wanayachukia)”  [ Imepokewa na Ibnu Maajah na Al Bayhaqiy.]

3. kuomba Dua wakati wakufungua saumu.
Kwa ilivyo Thubutu kutoka kwa Mtume Alipokuwa akifunguwa Saumu Akisema:

 

ذَهَبَ الظَّمَأُ وَابْتَلَّتْ الْعُرُوقُ وَثَبَتَ الْأَجْرُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ]    رواه أبوداود]

 
 
[Kiu imeondoka, na jasho limekuwa majimaji (limeanza kutokeza), na yamepatikana malipo (ya thawabu) apendapo Mwenyezi Mungu]    [Imepokewa na Abuu Daud.].

Na amesema Mtume ﷺ:

 

 للصائمِ عند فِطْرِهِ دَعْوَةً ما تُرَدُّ]     رواه إبن ماجة]

 

[Hakika kwa aliyefunga saumu wakati anapofungua kuna dua isiyorudi]   [ Imepokewa na Ibnu Maajah.]  yaani dua inayokubalika moja kwa moja mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

4. Kuacha mambo ya upuzi na mambo machafu.
Kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

إذا كان يوم صوم احدكم فلا يرفث ولا يصخب وإن قاتله أو سابه احد فليقل إني امرؤ صائم]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Ikiwa ni siku ambayo mmoja wenu amefunga, basi asifanye mambo machafu, [ Yarfuth Kufanya mambo machafu: yatokamana na neno uchafu, nako ni kutamka matamshi mabaya, na vile vile hutumika neno hili kumaanisha tendo la ndoa na vitangulizi vya tendo hili.] wala asikemee wenziwe[ Yaskhab: Yuwakemea: yatokamana na neno kemea, nako ni kubishana na kupiga ukulele.], anapotukanwa na mtu, au anapopigwa vita basi na aseme: Mimi ni mtu niliyefunga] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

مَنْ لَمْ يَدَعْ قَوْلَ الزُّورِ وَالْعَمَلَ بِهِ فَلَيْسَ لِلَّهِ حَاجَةٌ فِي أَنْ يَدَعَ طَعَامَهُ وَشَرَابَهُ]    رواه البخاري]

 

[Asie acha maneno machafu na kuyatumia basi Mwenyezi Mungu hana haja kwa mtu huyo kuacha chakula chake na kinywaji chake]     [Imepokewa na Bukhari.]

5. Kuzidisha kufanya Ibada kwa wingi.
Kama kusoma Qur’an, na kufanya adhkari kumtaja Mwenyezi Mungu, na kuswali swala ya Tarawehe, na visimamo vya usiku wakati watu wamelala, na kufanya visimamo vya usiku wa Lailatul Qadri, na kuswali swala za sunnah, na kutoa sadaka, na kuwa mkarimu na kujitahidi katika kufanya mambo ya kheri, na kuwalisha waliofunga wakati wa kufungua saumu zao, na kwenda Umrah, kwasababu matendo mema siku ya Ramadhani malipo yake yanaongezeka mara nyingi sana, kutoka kwa Ibn Abbas anasema:

 

كَانَ رَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -اجود الناس وَكَانَ اجود مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ، وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ الْقُرْانَ، فَلَرَسُولُ اللَّهِ -صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -اجود بِالْخَيْرِ مِنْ الرِّيحِ الْمُرْسَلَةِ‏. ‏     رواه البخاري

 

[Alikuwa Mtume ﷺ ni mkarimu kushinda watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibril, na alikuwa Jibril akikutana na Mtume kila usiku wa mwezi wa Ramadhani, ikawa anamfundisha Qur’ani , basi Mtume ﷺ pindi anapokutana na Jibril alikuwa mkarimu katika mambo ya kheri kushinda upepo mkali uliotumwa.]   [Imwpokewa na Bukhari.].

6. Kujitahidi kwa Ibada hasa kumi lamwisho katika Mwezi wa Ramadhani
Imepokewa na bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake  Amesema:

 

كان النبي إذا دخل العشر شد مئزره، وأحيا ليله، وأيقظ أهله]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Alikuwa Mtume ﷺ likingia kumi la mwisho akijifunga kibobwe [(Shadda mi’zarah) Nikinaya cha mtu kujitihidi katika ibada zaidi kuliko ilivo zowewa. Na kumesemwa ni kinaya cha mtu kujiepusha na mkewe,  na akiuhuisha usiku na akiwamsha wakezake]   [Imwpokewa na Bukhari na Muslim.]  akiwatanabahisha kwa ajili ya ibaada na akiwahimiza juu yake.



SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Saumu ya Ramadhani ina nguzo mbili za msingi, ambazo kusihi kwa saumu kunazitegemea.

Nguzo ya kwanza: Ni kutia nia: nao ni kuazimia kufunga mwezi wa Ramadhani. Na nia mahala pake ni moyoni na sio lazima kwa ulimi. Na wala haikupokelewa kwa Mtume kuwa alikuwa akiitemka nia na vile vile haikupokelewa kwa Maswahaba wake watukufu.

Kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Hakika kila jambo analolifanya (mwanadamu) ni kulingamana na nia yake, na hakika kila mtu atalipwa kulingana na alivyonuilia]        [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na kwa neno lake Mtume ﷺ:

 

من لم يبيت الصيام من الليل فلا صيام له]     رواه الترمذي] 

 

[Asiyeleta nia ya swaumu usiku, hana swaumu]. Imepokelewa na Tirmidhiy]

Na uwajibu huu wa kutia nia ni kwa upande wa saumu ya fardhi tu. Ama saumu za sunna, nia inatosha hata baada ya kuingia kwa mchana maadamu mtu hajatenda lo lote miongoni mwa yabatilishayo saumu.

 

عائشة رضي الله عنه : دخل علي رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات يوم ، فقال : [هل عندكم شيء ؟ ]  قلنا : لا . قال :[ فإني صائم ] . رواه مسلم 

Imepokelewa kutoka kwa Bibi Aysha-Allah amuwiye radhi-kwamba Mtume wa Allah-Rehema na Amani zimshukie aliingia kwake siku moja na kuuliza: [Je, mna cho chote?] Nikamjibu: Hapana, akasema: [Basi hakika mimi nimefunga].      [Imepokewa na Muslim]

 

Nguzo ya pili: Nikujizuia na yote yenye kuharibu Saumu  tokea kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuzama kwa jua, kwa ushahidi wa neno lake Allah Mtukufu:

 

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ}    البقرة:187}

 

"Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku.     [2:187]


Subcategories

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668590
TodayToday1278
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 19

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6867104ebca9913575685191751584846
title_6867104ebcba48779209881751584846
title_6867104ebcc9c1299173701751584846

NISHATI ZA OFISI

title_6867104ebea4a4797999641751584846
title_6867104ebeb3317429840401751584846
title_6867104ebec1513869341121751584846 Add content here

HUDUMA MPYA

: 8 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com