Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suali: Ni ipi hukmu ya kufanga?

Jawabu: Hukumu ya kufunga saumu
Imegawanyika saumu ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka katika sheria vigawanyo vifuatavyo:

1. SAUMU YA WAJIBU
Nayo iko sampuli mbili:

Sampuli ya kwanza: Ni Saumu aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu Subhanahu Wataala kwa waja wake. nayo ni saumu ya kufunga mwezi wa Ramadhani, na saumu hii ni nguzo moja wapo katika nguzo za Uislamu.Kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}    البقرة:183}

 

[Enyi mlo Amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu."  [Al-Baqara:183]

Na kama ilivyo kuja kwenye hadithi ya Bwana Mtume ﷺ:

 

بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان     رواه البخاري ومسلم 

 

[Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Sampuli ya pili: Ni Saumu ambayo kwamba mja ndiye anayekuwa sababu ya kuwajibishwa yeye mwenyewe kuifunga, kama vile saumu ya nadhiri na saumu ya kafara.

2. SAUMU ZA SUNNA
Nayo ni kila saumu ambayo kwamba sheria ya kiislamu imependekeza saumu hiyo kufungwa, kama kufunga siku ya Jumatatu na Alhamisi, na kufunga siku tatu za kila mwezi, na kufunga siku ya A’shura, na kufunga masiku kumi ya mwanzo wa mwezi wa Dhilhijja, na kufunga siku ya A’rafah.

 

MASHARTI YA KUWAJIBIKA KUFUNGA

 

Suali: Ni yapi Mashrti ya mtu kuwajibika Kufunga:

Jawabu: Masharti ya mtu kuwajibika Kufunga ni haya yafuatayo:
1. Uislamu: Haimlazimu kafiri kufunga.

2. Kubaleghe: Sio lazima kwa mtoto mdogo kufunga, lakini huamrishwa kufunga akiwa anaweza ili kumpa mazoezi ya saumu naye azoee.

3. Kuwa na akili: Sio wajibu kwa mwendawazimu kufunga.

4. Uwezo wa kufunga: Sio wajibu kufunga kwa mtu ambaye hawezi kufunga (labda amekuwa mzee sana ama afya yake haimruhusu kuhimili saumu).

5. Kwa Mwanamke asiwe kuwa kwenye ada yake ya Mwezi, au damu yanifasi.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668058
TodayToday746
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 11

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68669fa61b9784948877771751556006
title_68669fa61ba5e5169141801751556006
title_68669fa61bb461234970901751556006

NISHATI ZA OFISI

title_68669fa61d0cd8878783401751556006
title_68669fa61d1a53917590831751556006
title_68669fa61d27c19955603421751556006 Add content here

HUDUMA MPYA

: 13 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com