Surah 40 Ghafir Verse 60
﴿.وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ ﴾
And your Lord says, "Call upon Me; I will respond to you." Indeed,
those who disdain My worship will enter Hell [rendered] contemptible
KATIKA MAMBO YA KHERI NA ADABU KWA JUMLA
Ikiingia jioni (yaani jua linapokuchwa wakati wa magharibi) wazuieni watoto wenu kutoka toka kwani mashetani wanatawanyika nyakati hizo, ikisha pita wakati waacheni. Na fungeni milango yenu na mtajeni Mwenyezi Mungu mnapoifunga, kwani shetani hafungui mlango ulio fungwa. Na fungeni viriba vyenu vya maji, na mtajeni Mwenyezi Mungu. Na funikeni vyombo vyenu na mtajeni Mwenyezi Mungu (funikeni) hata kama ni kwa kuwekea kitu ju. Na zimeni taa zenu. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
وصلى الله وسلم وبارك على نبينا محمد وعلى آله وأصحابه أجمعين
[Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowarehemu jamaa wa Ibrahim. Na mbariki Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowabariki jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe Umesifika na Umetukuka.]
KINGA YA MUISLAMU
Amesema Mtume ﷺ Mwenye kusema:
سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni zake]
kwa siku mara mia, atafutiwa madhambi yake hata kama yalikuwa mfano wa povu la bahari. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na Mtume ﷺ amesema : "Atakaye sema:
[ لا إله إلا وحده لا شريك لهُ ، لهُ الملك ، ولهُ الحمدُ ، وهو على كل شيء قدير عشر مرات ]
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Allaah hali ya kuwa peke yake hana mshirika ni wake Ufalme na ni zake kila sifa njema na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.] mara kumi, ni kama (thawabu za mtu) aliyewacha huru nafsi nne katika wana wa Ismail. [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na amesema Mtume ﷺ Kuna maneno mawili ni mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Rahmani (Mwenye kurehemu) nayo ni :
[ سبحان الله وبحمده سبحان الله العظيم ]
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni zake, ametakasika Allaah aliye Mtukufu] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na amesema Mtume ﷺ Kusema kwangu:
[ سبحان الله ، والحمد لله ،ولا إله إلا الله ، والله أكبر ]
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni za Allaah na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa]
ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua. [Imepokewa na Muslim.]
Na amesema Mtume ﷺ: [Hivi anashindwa mmoja wenu kuchuma kila siku thawabu elfu? Mtu mmoja miongoni mwa waliokaa akamuuliza “Atachuma vipi mmoja wetu thawabu elfu? Akamjibu ﷺ Aseme :
سُبْحَانَ اللهِ
[Ametakasika Allaah]
……. Mara mia moja, basi ataandikiwa thawabu elfu moja, au atafutiwa madhami elfu moja. [Imepokewa na Muslim.]
Na Mtume ﷺ amesema : Atakaesema:
سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وبِحَمْدِهِ
[Ametakasika Allaah aliye Mtukufu na sifa njema zote ni zake]
.. hupandiwa mtende peponi [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Al-Haakim.]
Na amesema Mtume ﷺ [Ewe Abdalla Bin Qays, hivi nikufahamishe (nikuonyeshe) hazina miongoni mwa hazina za pepo? Nikamwambia: Ndio Ewe Mtume wa Allaah. Akaniambia: ‘Sema:
لا حول ولا قوة إلا بالله
[Hakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na akasema Mtume ﷺ [Bora ya maneno kwa Allaah ni manne :
[سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ، لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إلاَّ باللهِ]
[Ametakasika Allaah na sifa njema ni za Allaah na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah , na Allaah ni Mkubwa]
…. Si vibaya kuanza kwa lolote katika haya. [Imepokewa na Muslim.]
Alikuja mtu mmoja wa shamba kwa Mtume ﷺ akamwambia, nifundishe maneno nitakayoyasema. Mtume ﷺ akamwambia : Sema:
لاَ إِلهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، اللهُ أَكْبَرُ كَبيراَ والْحَمْدُ للهِ كَثيراً، سُبْحَانَ اللهِ رَبِّ العَالَمينَ، لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ العَزيزِ الْحَكِيمِ
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Allaah hali ya kuwa peke yake wala hana mshirika wake, Allaah ni Mkubwa tena sana, na sifa njema zote ni za Allaah tena nyingi sana. Ametakasika Allaah mola wa viumbe vyote, hapana uwezo wala nguvu ila ni za Allaah , Mwenye Kutukuka Mwingi wa Hekima]
yule mtu kisha akasema “Haya ni ya Allaah ni yapi yangu? Mtume akamwambia, Sema:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وارْزُقْنِي
[Ewe Allaah nisameh na unirehemu na uniongoze na uniruzuku] [Imepokewa na Muslim.]
Alikuwa mtu akisilimu, mtume anamfundisha kuswali kisha anamuamrisha kuomba kwa matamshi haya:
اللَّهُمَّ اغْفِرِ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وعَافِنِي وارْزُقْنِي
[Ewe Allaah nisamehe na unirehemu na uniongoze na unipe afya njema na uniruzuku] [Imepokewa na Muslim.]
Bora ya dua ni mtu kusema:
[الْحَمْدُ للهِ]
[Kila sifa njema ni za Allaah]
na bora ya utajo (uradi) ni mtu kusema:
لاَ إِلَه إِلاَّ اللهُ
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Allaah.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ibnu Maajah na Al-Haakim]
Mema yasiokwisha ni :
سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ،لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إلاَّ باللهِ
[Ametakasika Allaah na sifa njema zote ni za Allaah, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa, nahakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah.] [Imepokewa na Ahmad.]
VIPI ALIKWA MTUME ﷺ AKIMSABBIH MWENYEZI MUNGU
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla bin Amru radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: "Nimemuona Mtume ﷺ anahesabu kumsabbih Allaah kwa mkono wake wakulia. [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]
KINGA YA MUISLAMU
[ قال رسول الله صلى الله عيه وسلم :[ والله إني لاستغفر الله وأتوب إليه في اليوم أكثر من سبعين مرة
البخاري مع الفتح 11/101
Amesema Mtume ﷺ [Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia kwake katika kila siku zaidi ya mara sabini.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
[ وقال صلى الله عيه وسلم :[ يا أيها الناس توبوا إلى الله فإني أتوب في اليوم إليه مائة مرةً
مسلم 4/2076
Mtume ﷺ amesema: [Enyi watu tubieni kwa Mwenyezi Mungu kwani mimi ninatubia kwake kwa siku mara mia.] [Imepokewa Muslim.]
[وقال صلى الله عيه وسلم :[ من قال أستغفر الله العظيم الذي لا إله إلا هو الحي القيوم وأتوب إليه ، غفر الله لهُ وإن كان فر من الزحف
أخرجه أبو داود 2/85 والترمذي 5/569 والحاكم وصححه ووافقه الذهبي
Amesema Mtume ﷺ yoyote anaesema :
[Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Yeye, aliye Hai aliyesimama kwa dhati yake, na ninarejea kwake.] Mwenyezi Mungu atamsamehe hata kama ana makosa ya kukimbia vitani. [Imepokewa na abuu Daud na Al-Ttirmidhiy na Al-Haakim.]
[ وقال صلى الله عيه وسلم :[ أقرب ما يكون الربُّ من العبد في جوف الليل الآخر فإن استطعت أن تكون ممن يذكر الله في تلك الساعة فكن
أخرجه الترمذي والنسائي 1/279 والحاكم
Na Amesema Mtume ﷺ [Wakati anaokuwa mja na Mola wake wako karibu zaidi ni katika nusu ya mwisho wa usiku. Ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu kwa wakati huo basi kuwa] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Al-Nnasaai na Al-Haakim.]
[وقال صلى الله عيه وسلم :[ أقرب ما يكون العبد من ربه وهو ساجد فأكثروا الدعاء
مسلم 1/350
Na Mtume ﷺ amesema: [Sehemu ambayo anakuwa mja yuko karibu mno na Mola wake ni wakati amesujudu, basi zidisheni dua wakati huo.] [Imepokewa na Muslim.]
[وقال صلى الله عيه وسلم :[ إنه ليغان على قلبي وإني لاستغفرُ الله في اليوم مائة مرة
أخرجه مسلم 4/2075
Na Mtume ﷺ amesema: [Huwa nimesahaulishwa kumtaja Mwenyezi Mungu na hakika mimi ninamuomba msamaha Mwenyezi Mungu mara mia kwa siku.] [Imepokewa na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.