Menu

Adhkaar (Dua)

 

DUA YA KUSOMWA AKIWA AMESIMAMA KATIKA MLIMA WA SWAFAA NA MARWA

 

Amesema Jaabir radhi za Allah ziwe juu yake, Mtume ﷺ alipokurubia Swafaa alisoma:

[...إِنَّ الصَّفَا والمَرْوَةَ مِنْ شَعائرِ الله]

[Hakika Swafaa na Marwah ni katika alama za kumtukuza Mwenyezi Mungu]

 

[ أَبْدَأُ بِمَا بَدَأَ اللهُ بِهِ ]

[Ninaanza kwa alichoanza Mwenyezi Mungu]

 Akaanza Swafaa akapanda mpaka akaiona Al-Kaabah kisha akaielekea na kusema:

[اللهُ أكْبَرُ, اللهُ أكْبَرُ, اللهُ أكْبَرُ]

[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa]

 kisha atasema yafuatayo mara tatu akomba dua (yoyote apendayo) baada ya kila mara:

لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake, wala hana mshirika wake, ni wake Ufalme nani zake sifa njema naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, ametekeleza ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amivishinda vikosi peke yake.]

….. Mtume  alisoma hivi mara tatu na baina yake akiomba dua, kisha akafanya akiwa Marwah kama alivyofanya Swafaa.    [Imepokewa na Muslim.]


DUA YA KUSOMWA AKIWA AMESIMAMA KATIKA MLIMA WA SWAFAA NA MARWA


 

DUA INAYOSOMWA BAINA YA NGUZO YA YEMEN NA HAJAR AL ASWAD (KATIKA AL KAABAH)

 

Alikuwa Mtume  akisema baina yake:

{ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ}

[Ewe Mwenyezi Mungu  tupe katika dunia hii wema na katika akhera  wema na utukinge na adhabu ya moto.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad na Al-Baghawiy.]


DUA INAYOSOMWA BAINA YA NGUZO YA YEMEN NA HAJAR AL ASWAD (KATIKA AL KAABAH)


 

 

VIPI ATALETA TALBIYAH ALIYEHIRIMIA KWA HIJJAH NA UMRA

 

[ لبيك اللهم لبيك ، لبيك لا شريك لك لبيك ، إن الحمد والنعمة لك والملك ، لا شريك لك ]

البخاري مع الفتح 3/ 408 ، ومسلم 2/841

[Nimekuitika Ee Allaah nimekuitika, nimekuitika huna mshirika wako nimekuitika, hakika sifa njema na neema na Ufalme ni vyako huna mshrika wako.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]


VIPI ATALETA TALBIYAH ALIYEHIRIMIA KWA HIJJAH NA UMRA


 

 

TAKBIRA ATAKAPOFIKA KATIKA HAJARUL AL-ASWAD

 

Mtume alitufu (kuzunguka Al-Kaabah) juu ya ngamia, kila anapofika katika Hajrat-Aswad (Jiwe jeusi) alikuwa anaashiria kwa fimbo yake na kusema:

[اللهُ أكْبَر]

[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa]   [Imepokewa na Bukhari.]


TAKBIRA ATAKAPOFIKA KATIKA HAJARUL AL-ASWAD


 

ANACHOSEMA MUISLAMU AKISIFIWA

 

[ اللهم لا تؤاخذني بما يقولون ، واغفر لي مالا يعلمون [واجعلني خيراً مما يظنون ]

 البخاري في الأدب المفرد برقم 761

[Ewe Mwenyezi Mungu usinichukulie kwa yale wanayoyasema na unisamehe kwa yale wasiyoyajua, (na unifanye bora kuliko wanavyonifikiria]    [Imepokewa na Bukhari katika Al-Adabul-Mufrid]


ANACHOSEMA MUISLAMU AKISIFIWA


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7887134
TodayToday267
Highest 05-20-2026 : 12580
US
Guests 76

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6a3b9f8bca24813415157051782292363
title_6a3b9f8bca29816971689861782292363
title_6a3b9f8bca2e54076838571782292363

NISHATI ZA OFISI

title_6a3b9f8bca8ea15629739661782292363
title_6a3b9f8bca9399215063681782292363
title_6a3b9f8bca985790717021782292363 Add content here

HUDUMA MPYA

: 9 + 3 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com