KINGA YA MUISLAMU
[ بسم الله وعلى سُنة رسول الله ]
أبو داود 3/314بسند صحيح وأحمد
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa mwenendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.] [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad.]
DUA YA KUMUINGIZA MAITI NDANI YA KABURI
KINGA YA MUISLAMU
إن لله ما أخذ وله ما أعطى . وكل شيء عنده بأجل مُسمى ...فلتصبر ولتحتسب
البخاري 2/80 ومسلم 2/636
[Kwa hakika ni Chake Mwenyezi Mungu Alichokichukua, na ni chake Alichokitoa, na kila kitu Kwake kina muda maalum]
(.......kisha Mtume ﷺ akimwambia:) "basi vumilia na taka malipo kwa Allaah" ] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
na akisema:
[ أعظم الله أجرك ، وأحسن عزاءك وغفر لميتك ]
[Ayafanye mengi Allaah malipo yako, na Akufanye kuzuri kutaaziwa (kuhaniwa) kwako na Amsamehe maiti wako.]
...basi ni bora [Tazama Al-Adhkaar ya Imam Al-Nnawawiy]
DUA YA KUMTAAZI ALIYEFILIWA
KINGA YA MUISLAMU
اللهم اغفر له وارحمه، وعافه ،واعف عنه ،وأكرم نُزُله ، ووسع مُدخلهُ ، واغسله بالماء والثلج والبرد ، ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله وزوجاً خيراً من زوجه، وأدخله الجنة ،وأعذه من عذاب القبر ( ومن عذاب النار
مسلم 2/663
[Ewe Mwenyezi Mungu msamehe na umrehemu na umuafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake (kaburini) na upanue kuingia kwake, na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama unavyoitakasa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na muingize peponi na mkinge na adhabu ya kaburi (na adhabu ya moto).] [Imepokewa na Muslim.]
اللهم اغفر لحينا وميتنا ، وشاهدنا وغائبنا ، وصغيرنا وكبيرنا ، وذكرنا وأُنثانا ، اللهم من أحييته منا فأحيه على الإسلام ، ومن توفيته منا فتوفه على الإيمان اللهم لا تحرمنا أجره ولا تضلنا بعده
ابن ماجه 1/480 وأحمد 2/368
[Ewe Mwenyezi Mungu, msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa, na aliyopo na asiyekuwepo, na mdogo kati yetu na mkubwa, na mwanamume kati yetu na mwanamke. Ewe Mwenyezi Mungu unaemueka hai kati yetu basi mweke katika Uislamu, na uliyemfisha basi mfishe juu ya iman. Ewe Mwenyezi Mungu usitunyime thawabu zake wala usitupoteze baada yake.] [Imepokewa na Ibnu Maajah na Ahmad.]
اللهم إن فلان بن فلان في ذمتك،وحبل جوارك،فقه من فتنة القبر وعذاب النار،وأنت أهل الوفاء والحق .فاغفر له وارحمهُ إنك أنت الغفور الرحيم
أخرجه ابن ماجه
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika (fulani bin fulani) yuko katika dhima yako na kamba ya ujirani wako, basi mkinge na fitina ya kaburi na dhabu ya moto nawe ndiwe mstahiki wa utekelezaji na ukweli, basi msamehe na umrehemu hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu.] [Imepokea na Ibnu Maajah.]
اللهم عبدك وابن عبدك وابن أمتك احتاج إلى رحمتك ،وأنت غني عن عذابه،إن كان مُحسناً فزده في حسناته، وإن كان مُسيئاً فتجاوز عنه
أخرجه الحاكم وصححه ووافقه الذهبي
[Ewe Mwenyezi Mungu, mja wako na mtoto wa kijakazi chako, nimuhitaji wa rehema yako, nawe huhitaji na kumuadhibu, kwa hivyo akiwa ni mwema mzidishie katika mema yake na akiwa ni muovu msamehe madhambi yake.] [Imepokewa na Al-Haakim na akasahihisha na kuafikiwa na Al-Dhahabiy.]
DUA YA KUMUOMBEA MAITI WAKATI ANAPOSWALIWA
KINGA YA MUISLAMU
[اللهم أعذه من عذاب القبر]
أخرجه مالك في الموطأ 1/288 وابن أبي شيبه في المصنف 3/ 217 والبيهقي 4/9
[Ewe Mwenyezi Mungu mlinde na adhabu ya kaburi] [Imepokewa na Imam Maalik na Ibnu Abiy Shayba na Al-Bayhaqiy.]
اللهم اجعله فرطاً وذخراً لوالديه ،وشفيعاً مجاباً .اللهم ثقل به موازينها وأعظم به أجورهما ، وألحقهُ بصالح المؤمنين ، واجعلهُ في كفالة إبراهيم ، وقه برحمتك عذاب الجحيم ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله ، اللهم اغفر لاسلافنا ، وأفراطنا ، ومن سبقنا بالإيمان
[Ewe Mwenyezi Mungu mjaaliye kuwa nikitangulizi na akiba kwa wazazi wake na nikiombezi chenye kukubaliwa dua yake. Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yake zifanye nzito mizani za wazazi wake na yafanye mengi malipo yao, na mkutanishe na wema wa waumini na mjaaliye awekatika dhamana ya Ibrahim na umuepushe kwa rehema yako na adhabu ya moto, na mbadlishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kulko jamaa zake. Ewe Mwenyezi Mungu, wasamehe waliotangulia na waliopita na waliotutangulia katika Uislamu.]
Alikuwa Al-Hassan Radhi za Allah ziwe juu yake anamsomea mtoto mdogo Suratul Fatiha kisha anasema:
اللهم اجعله لنا فرطاً ،وسلفاً وأجراً
[Ewe Mwenyezi Mungu mfanye kwetu sisi ni kitangulizi cha malipo na dhamana na malipo.] [Imepokewa na Al-Baghawiy na Abdulrazaaq.]
DUA YA MAITI YA MTOTO MCHANGA WAKATI WA KUMSWALIA
KINGA YA MUISLAMU
اللهم اغفر لفلان ( باسمه) ورفع درجته في المهديين، واخلفه في عقبه في الغابرين، واغفر لنا وله يا رب العالمين ، وافسح له في قبره ونور له فيه مسلم 2/634
[Ewe Mwenyezi Mungu msamehe (jina la maiti) na ipandishe daraja yake katika wailoongoka, na weka badili yake kwa aliyowacha nyuma na utusamehe sisi na yeye ewe Mola wa viumbe vyote na umkunjulie yeye katika kaburi lake na umtilie mwangaza ndani yake.] [Imeokewa na Muslim.]
DUA YA KUMFUNGA MACHO MAITI
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.