KINGA YA MUISLAMU
[ اللهم لا سهل إلا ما جعلته سهلاً وأنت تجعل الحزن إذا شئت سهلاً ]
رواة ابن حبان في صحيحه برقم 2427 (موارد) وابن السني برقم 351
[Ewe Mwenyezi Mungu hakuna jepesi ila ulilolifanya jepesi, nawe unalifanya gumu jepesi ukitaka.] [Imepokewa na Ibnu Hibban na Ibnu Sunniy.]
DUA YA AMBAE LIMEKUWA GUMU KWAKE JAMBO
KINGA YA MUISLAMU
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم واتفل على يسارك ] ثلاثاً]
مسلم 4/1729
[Najilinda na Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa]
Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu.
Imepokelewa kutoka kwa Uthman Ibn Al-Ass Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: [Nilimwambia Mtume ﷺ Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika shetani amenikalia kati yangu na kati ya swala yangu na kisomo changu, ananitatiza. Akasema Mtume ﷺ [Huyo ni shetani aitwae “Khanzab” ukimuhisi amekujia basi muombe hifadhi Mwenyezi Mungu nae, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu]
……nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akaniondoshea. [Imepokewa na Muslim.]
DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI
KINGA YA MUISLAMU
[ يستعيذ بالله ]
البخاري مع الفتح 6/336 ومسلم 1/120
[Atataka (aombe) hifadhi ya Mwenyezi Mungu] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
[ ينتهي عما شك فيه ]
البخاري مع الفتح 6/336 ومسلم 1/120
[Aondowe kile kitu alichokifanyia shaka] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
"يقول" آمنت بالله ورسله
مسلم 1/ 119
Kisha aseme [Nimemuamini Mwenyezi Mungu na mitume yake.] [Imepokewa na Muslim.]
{يقرأ قوله تعالى { هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
Kisha asome aya hii katika Qur’ani
[Yeye ndiye wa Mwanzo na wa Mwisho, na aliye Wazi, na aliyejificha, naye ni mjuzi wa kila kitu.]
[Imepokewa na Abuu Daud.]
DUA ALIYEPATWA NA SHAKA KATIKA IMANI YAKE
KINGA YA MUISLAMU
[ اللهم اكفني بحلالك عن حرامك ، وأغنني بفضلك عمن سواك ]
الترمذي 5/560
[Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze mimi na halali yako kutokana na haramu, na unitosheleze kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine usio Wewe.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]
[ اللهم إني أعوذ بك من الهم والحزن ، والعجز والكسل ،والبخل والجبن وضلع الدين وغلبة الرجال ]
البخاري7/ 158
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na hamu na huzuni na kutoweza na uvivu na ubakhili na uoga na uzito wa deni na kushindwa na watu.] [Imepokewa na Bukhari.]
SIKILIZA DUA YA KULIPA DENI
KINGA YA MUISLAMU
[ اللهم اكفنيهم بما شئت ]
مسلم 4/2300
[Ewe Mwenyezi Mungu , nitosheleze kutokana na wao kwa unachotaka.] [Imepokewa na Muslim.]
SIKILIZA DUA YA ANAEWAOGOPA WATU
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.