Menu

Adhkaar (Dua)


DUA YA KUJILINDA NA DAJJAL


 DAJJAL


 

[ من حفظ عشر آيات من أول سورة الكهف عصم من الدجال ]

مسلم 1/555

Amesema Mtume :

[Yoyote anaehifadhi kwa moyo aya kumi za mwanzo wa Suratul-Kahf atakuwa na kinga ya kujiepusha na Dajjal.]        [Imepokewa na Muslim.]

Pia ni katika Sunnah kujilinda na Mwenyezi Mungu  kutokana na fitna ya Dajjal baada ya tashahhud ya mwisho katika kila swala.



DUA YA KUMUOMBEA ALIYEKUFANYIA WEMA


 JAZAKALLAH


 

[ جَزَاكَ الله خيراً ]

أخرجه الترمذي رقم 2035 

[Mwenyezi Mungu akulipe wema]      [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]


DUA YA KUMUOMBEA ALIYEKUFANYIA WEMA


 



KAFARA YA KIKAO


 kafaraa


 

[ سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك ]

 أخرجه أصحاب السنن

[Kutakasika ni Kwako ewe Mwenyezi Mungu na sifa njema zote ni Zako. Nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea Kwako]     [Imepokewa na wapokezi wa Hadithi]

 

عن عائشة رضي الله عنها قالت : ماجلس رسول الله صلى الله عليه وسلم مجلساً قط ، ولا تلا قرآناً ، ولا صلى صلاة إلا ختم ذلك بكلمات قالت : فقلت : يارسول الله أراك ما تجلس ( مجلساً ) ولا تتلو قرآنا ، ولا تصلي صلاة إلا ختمت بهؤلاء الكلمات ؟ قال : نعم ( من قال خيراً خُتم له طابع على ذلك الخير ، ومن قال شراً كن له كفارة  ،  سبحانك وبحمدك لا إله إلا أنت أستغفرك وأتوب إليك

Imepokelewa kutoka kwa mama wa Waumini 'Aaishah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hajapatapo kukaa Mtume kikao wala kusoma Qur'ani wala kuswali ila atamaliza na du'aa hii’ Amesema mama wa Waumini 'Aaishah radhi za Allah ziwe juu yake nikamuuliza “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nakuona hukai kikao chochote wala husomi Qur’ani wala huswali swala yoyote ile ila unaimalizia kwa kusoma maneno haya kwanini hasa? Akasema [Ndio anayesema kheri amalize kwa kheri na anayesema shari yanakuwa maneno haya ni kafara kwake]

 

[ سُبْحـانَكَ وَبِحَمدِك، لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْكَ ]

 

[Kutakasika ni Kwako na sifa njema zote ni Zako, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea Kwako]      [Imepokewa na Al-Nnasaai, na Ahmad.]


SIKILIZA DUA YA KAFARA YA KIKAO


  



KINGA YA MUISLAMU


 MADHAMBI


Imepokelewa kutoka kwa Abdillahi bin Sarjis radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimjia Mtume nikala katika chakula chake kisha nikamwambia :

 

[ غَفَـرَ اللهُ لَكَ يا رَسـولَ الله ]

 

[Mwenyezi Mungu Akusamehe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu]

Akaniambia

[ وَلَكَ ]

 

[Nawe akusamehe]      [Imepokewa na Ahmad na Al-Nnasaai.]


KUMUOMBEA DUA ANAEKUOMBEA MSAMAHA KWA MWENYEZI MUNGU


 



UTAJO UNAOSOMWA KATIKA KIKAO


 dua ya kikao


Imepokelewa kutoka kwa Ibn Omar amesema : "Alikuwa akihisabiwa Mtume kusoma kwake dua hii katika kikao kimoja ikifika idadi ya mara mia kabla hajasimama"

 

[ رَبِّ اغْفِـرْ لي، وَتُبْ عَلَـيَّ، إِنَّكَ أَنْـتَ التَّـوّابُ الغَـفُورُ ] 

 

[Mwenyezi Mungu nisamehe na nikubalie toba yangu, hakika Wewe ni mwingi wa kukubali toba, mwingi wa kusamehe]      [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]


UTAJO UNAOSOMWA KATIKA KIKAO


 


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668569
TodayToday1257
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 25

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68670cb603e8719548771121751583926
title_68670cb60ffa97572407581751583926
title_68670cb6100b11182211501751583926

NISHATI ZA OFISI

title_68670cb6116d81002365821751583926
title_68670cb6117d110518178561751583926
title_68670cb6118bc6524189361751583926 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com