Menu

Adhkaar (Dua)


KINGA YA MUISLAMU


 20920.imgcache


Alikuwa Mtume  akienda kulala usiku anakusanya viganja vyake kisha akivipuliza na akivisomea Suratul-Ikhlaasw, na Suratul-Falaq, na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani na usoni na mbele.

akifanya hivyo mara tatu.     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Mtume  amesema : [Ukienda kulala soma Ayatul-Kursiy mpaka uimalize kwani Allaah ataendelea kukuhifadhi wala hakukaribii Shaytwaan mpaka asubuhi]

 

[.....اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُـوَ الـحَيُّ القَيّـومُ لا تَأْخُـذُهُ سِنَـةٌ وَلا نَـوْمٌ ]

[Imepokewa na Bukhari.]

 

Amesema Mtume [Anayesoma aya mbili za mwisho wa Suratul-Baqarah usiku zinamtosheleza]

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ) ( لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى

الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَآ أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِين

[Imepokelewa na Bukhari na Muslim.]

 

Mtume  pia amesema: [Akiamka mmoja wenu kutoka usingizini kisha akarudi basi akikukute kitanda kwa shuka yake mara tatu na amtaje Mwenyezi Mungu kwani hajui kilicho kuja baada yake. Na Akilala aseme:]

 

[ بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي ، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فارْحَـمْها ، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين ]

 

[Kwa jina lako Mola wangu, nimeweka ubavu wangu na kwa ajili yako nitaunyanyua, na ukiizuia (ukiichukua) roho yangu basi  irehemu na ukiirudisha basi ihifadhi kwa kile unacho wahifadhi nacho waja wako wema.]         [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

 اللّهُـمَّ  إِنَّـكَ خَلَـقْتَ نَفْسـي  وَأَنْـتَ تَوَفّـاهـا لَكَ ممَـاتـها وَمَحْـياها ، إِنْ أَحْيَيْـتَها فاحْفَظْـها ، وَإِنْ أَمَتَّـها فَاغْفِـرْ لَـها . اللّهُـمَّ  إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ العـافِـيَة

 

[Ee Mwenyezi Mungu  hakika Wewe umeiumba nafsi yangu nawe utaiua, ni kwako uhai wa nafsi yangu na ufaji wake, ukiipa uhai basi ihifadhi, na ukiifisha (ukiiua) basi isamehe.  Ee Allaah  hakika mimi nakuomba afya njema.]        [Imepokea na Muslim na Ahmad.]

Alikuwa Mtume  akitaka kulala anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake  kisha anasema:

 

 اللّهُـمَّ قِنـي عَذابَـكَ يَـوْمَ تَبْـعَثُ عِبـادَك ]  ثلاث مرات]

 

[Ee Mwenyezi Mungu nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakayo wafufua waja wako.]

Mara tatu  [Imepokewa na Abuu Daud.]

 

[ بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَمـوتُ وَأَحْـيا ]

 

[Kwa jina lako Ee Mwenyezi Mungu ninakufa na ninakuwa hai.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Mtume  amesema: [Hivi  niwafahamishe juu ya kitu ambacho ni bora zaidi kuliko mtumishi wakati munapolala; Msabihini Allaah mara thelathini na tatu, kisha msifuni Allaah  mara thelathini na tatu, na kisha mtukuzeni mara thelathini na tatu kwani kufanya hivi ni bora kwenu kuliko mtumishi.]

سُبْـحانَ الله ]  ثلاثاً وثلاثين]

[Ametakasika Mwenyezi Mungu]  Mara thelathini na tatu.

 أَلْحَمْدُ لِلَّه]   ثلاثاً وثلاثين]

[Sifa njema zote ni za Mwenyezi mungu]  Mara thelathini na tatu.

اللَّه أكْبَرُ]  ثلاثاً وثلاثين ]

[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa]   Mara thelathini na tatu.       [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

اللهم ربَّ السموات السبع،ورب العرش العظيم،ربنا ورب كل شيء، فالق الحب والنوى، ومُنزل التوراة والإنجيل والفرقان، أعوذ بك من شر كل شيء أنت آخذٌ بناصيته،اللهم أنت الأول فليس قبلك شيء،وأنت الآخر فليس بعدك شيء، وأنت الظاهر فليس فوقك شيء، وأنت الباطن فليس دونك شيء، اقض عنا الدَّيْنَ واغننا من الفقر

 

[Ee Mwenyezi Mungu  Mola wa mbingu saba na Mola wa arshi tukufu, Mola wetu na Mola wa kila kitu Mwenye kuichanua tembe ya mbegu na kokwa na alieteremsha Tawraat na Injiyl na Qur-aan, najikinga kwako kutokana na shari ya kila kitu. Wewe  ndie mwenye kukamata utosi wake. Ee Allaah, Wewe ndie wa Mwanzo hakuna kabla yako kitu, nawe ndie wa Mwisho, hakuna baada yako kitu, na wewe ndiye uliewazi, hakuna juu yako kitu chochote na Wewe ndiye uliyefichika hakuna kilichojificha chini yako. Tulipie madeni yetu na utuepushe na ufakiri.]        [Imepokew na Muslim.]

 

[الـحَمْدُ للهِ الَّذي أَطْـعَمَنا وَسَقـانا، وَكَفـانا، وَآوانا، فَكَـمْ مِمَّـنْ لا كـافِيَ لَـهُ وَلا مُـؤْوي]

[Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametulisha na ametunywesha na akatutosheleza na akatuhifadhi, ni wangapi ambao hawana wa kuwatosheleza wala wa kuwahifadhi.]     [Imepokewa na Muslim.]

 

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيبِ وَالشّـهادةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كُـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه، أَشْهـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ   نَفْسـي، وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى  نَفْسـي  سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم

 

[Ee Mwenyezi Mungu mjuzi wa yaliyojificha na yaliyo wazi, Muumba wa mbingu na ardhi, mola wa kila kitu na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, najilinda kwako na shari ya nafsi yangu na shari ya Shaytwaan na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu.]      [Imepokewa na Abuu Daud]

 

Ukitaka kulala tawadha wudhuu kama wa Swalah kisha lalia ubavu wako wa kulia kisha sema:

اللّهُـمَّ أَسْـلَمْتُ نَفْـسي إِلَـيْكَ، وَفَوَّضْـتُ أَمْـري إِلَـيْكَ، وَوَجَّـهْتُ وَجْـهي إِلَـيْكَ، وَأَلْـجَـاْتُ ظَهـري إِلَـيْكَ، رَغْبَـةً وَرَهْـبَةً إِلَـيْكَ، لا مَلْجَـأَ وَلا مَنْـجـا مِنْـكَ إِلاّ إِلَـيْكَ، آمَنْـتُ بِكِتـابِكَ الّـذي أَنْزَلْـتَ وَبِنَبِـيِّـكَ الّـذي أَرْسَلْـت

 

[Ee Mwenyezi Mungu nimeisalimisha nafsi yangu kwako, na nimekuachia mambo yangu Wewe na nime uelekeza uso wangu kwako na nimeutegemeza mgongo wangu kwako, kwa matajarajio na kwa kukuogopa, hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila kwako, nimekiamini kitabu chako ulicho kiteremsha na Mtume wako uliyemtuma.]

Amesema Mtume ﷺ [kwa mwenye kusema haya kisha ukifa utakuwa umekufa katika Uislamu.]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]


SIKILIZA NYIRADI ZA KULALA 




KINGA YA MUISLAMU


 azkar 


Imepokelewa kutoka kwa  Anas  Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:  Amesema Mtume [Kukaa pamoja na watu wanaomtaja Mwenyezi Mungu  Aliyetukuka  kuanzia Swalah ya Al-Fajiri  mpaka kuchomoza jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuacha huru watu wanne miongoni mwa wana wa Ismail na kukaa na watu wanaomtaja  Mwenyezi Mungu  Aliyetukuka  kuanzia baada ya Swalah ya Al-Asiri mpaka kuchwa jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuwaacha huru watu wanne.]      [Imepokewa na Abuu Daud].

 

اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

 

Mwenye kusoma (Ayatul-Kursiy) pindi anapoamka atalindwa  kutokana na majini mpaka jioni, na atakaeisoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi.     [Imepokewa na Hakim na Al-Twabraniy na kusahihishwa na Al-Baaniy]

 

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ


قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ


قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

ثلاث مرات

من قالها ثلاث مرات حين يصبح وحين يمسي كفته من كل شيء . أبو داود 4/ 322 والترمذي 5/ 567وانظر صحيح الترمذي 3/ 182

 

[Mwenye kusisoma (sura hizi) mara tatu asubuhi na jioni zinamtosheleza na kila kitu.]      [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]

 

أصبحنا وأصبح الملك لله، والحمد لله، لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير، ربِّ أسألك خير ما في هذا اليوم وخير ما بعده وأعوذ بك من شر ما في هذا اليوم وشر ما بعده ربِّ أعوذ بك من الكسل وسوء الكبر، ربَّ أعوذ بك من عذابٍ في النار وعذاب في القبر

مسلم 4/ 2088

[Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah , na sifa njema ni zake Allaah , hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Allaah , hali yakuwa peke yake, hana mshirika.  Niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ee Mola, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajilinda Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Ee Mola, najilinda Kwako, kutokana  na uvivu, na ubaya wa uzee (uzee mbaya) Ee Mola najilinda Kwako kutokana na adhabu ya  moto na adhabu ya kaburi.]    [Imepokewa na Muslim.]

Na ikiingia jioni useme

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير ، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر     مسلم 4/ 2088

[Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah , na sifa njema ni zake Allaah , hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Allaah , hali yakuwa peke yake, hana mshirika.  Niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ee Mola, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajilinda Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Ee Mola, najilinda Kwako, kutokana  na uvivu, na ubaya wa uzee (uzee mbaya) Ee Mola najilinda Kwako kutokana na adhabu ya  moto na adhabu ya kaburi]     [Imepokewa na Muslim.]

 

[اللهم بك أصبحنا وبك أمسينا وبك نحيا وبك نموت وإليك النشور]

الترمذي 5/ 466 وانظر صحيح الترمذي 3/ 142

[Ee Allaah  kwa sababu yako tumeingia katika asubuhi, na kwa ajili yako tumeingia jioni, na kwa ajili yako ndio  tumekuwa hai, na kwa ajili yako tutakufa, na kwako tutafuliwa.]      [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]

 

Na ikifika jioni aseme

 

[اللهم بك أمسينا، وبك أصبحنا، وبك نحيا وبك نموت، وإليك المصير]

الترمذي 5/ 466 وانظر صحيح الترمذي 3/ 142

[Ee Allaah  kwa ajili yako tumefika jioni, na kwa ajili yako tumefika asubuhi, na kwa ajili yako tuko hai na kwa ajili yako tutakufa na ni kwako tu marejeo.]        [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]

 

اللهم أنت ربي لا إله إلا أنت خَلَقتني وأنا عَبْدُك وأنا على عهدك ووعدك ما استطعت أعوذ بك من شر ما صنعت أبوء لك بنعمتك علي وأبوء بذنبي فاغفر لي فإنه لا يغفر الذنوب إلا أنت          أخرجه البخاري 7/150

 

[Ee Allaah  Wewe ni Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja wako, nami niko juu ya  ahadi yako, na agano lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda kwako kutokana  na shari ya nilicho kifanya, nakiri  kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe.]    [Imepokewa na Bukhari.]

 

اللهم إني أصبحت  أشهدك وأشهد حملة عرشك ، وملائكتك وجميع خلقك ، أنك أنت الله لا إله إلا أنت وحدك لا شريك لك ، وأن محمداً عبدك

ورسولك"  (أربع مرات حين يصبح أو يمسي 

أخرجه أبو داود 4/ 317 والبخاري في الأدب المفرد برقم 1201 والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 9، وابن السني

 

[Ee Allaah  hakika mimi nimefika asubuhi nakushuhudia na nina washuhudia wabeba wa arshi yako na malaika wako, na viumbe vyako vyote kwamba Wewe ndiye Allaah  hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa peke yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wako na ni Mtume wako.]     (Atasema hivi mara nne, asubuhi au jioni)  Atakaye yasema haya asubuhi au jioni mara nne Mwenyezi Mungu aliyetukuka atamuepusha na moto. [Imepokewa na Abuu Daud na Bukhari katika Adabul-Mufrad na Al-Nnasai na Ibnu Sunniy.]

 

[اللهم ما أصبح بي من نعمة أو بأحد من خلقك فمنك وحدك لا شريك لك ، فلك الحمد ولك الشكر]

أخرجه أبو داود 4/318 ، والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 7وابن السني برقم 41 وابن حبان

[Ee Allaah  sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe chako chochote, na neema ila inatoka kwako hali ya kuwa peke yako huna mshirika wako, ni zako  sifa njema na nizako shukurani.]  

Atakae yasema haya kila asubuhi basi atakuwa ametekeleza  shukurani ya siku nzima, na atakae yasema jioni atakuwa ametekeleza shukurani ya usiku mzima

[Imepokewa na Abuu Daud na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy na Ibnu Hibban.]

 

اللهم عافني في بَدَني، اللهم عافني في سمعي، اللهم عافني في بصري، لا إله إلا أنت .اللهم إني أعوذ بك من الكفر، والفقر، اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر لا إله إلا أنت         ثلاث مرات

أبو داود 4/ 324، وأحمد 5/ 42 والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم   22 وابن السني برقم 69 والبخاري في الأدب المفرد

[Ee Allaah nipe afya ya mwili wangu, Ee Allaah nipe afya ya usikizi wangu, Ee Allaah nipe afya ya uwoni wangu,hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe Ee Allaah hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.]   mara tatu   [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad na Al-Nnisaai.]

 

[ حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم ]

أخرجه ابن السني 

[Allaah ananitosha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, kwake Yeye nimetegemea, na Yeye ni Mola wa Arshi Tukufu.]     [Imepokewa na Ibnu Sunniy]

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ  وَأهْـلي وَمالـي ، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي ، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي ، وَمِن فَوْقـي ، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

أبو داود وابن ماجه وانظر صحيح ابن ماجه 2/332

[Ee Allaah  nakuomba msamaha na afya duniani na akhera.  Ee Allaah  hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na jamaa zangu, na mali yangu, Ee Allaah nisitiri uchi wangu, na unitulize  khofu yangu, Ee Allaah  nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, najuu yangu, na najilinda kwa utukufu wako kwakutekwa chini yangu.]     [Imepokewa na Abuu Daud.]

 

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيْبِ وَالشّـهادَةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه ، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت ، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ   نَفْسـي  وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه ، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى  نَفْسـي  سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم

 الترمذي وأبو داود .انظر :صحيح الترمذي3/ 142

[Ee Allaah , Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyowazi, muumba wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu, na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki  ila Wewe, najilinda kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na shari ya shetani na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu.]     [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Abuu Daud]

 

 بسم الله الذي لا يضرُّ مع اسمه شيء في الأرض ولا في السماء وهو السميع العليم]    ثلاث مرات]

 أخرجه أبو داود 4/ 323 والترمذي 5/ 465 وابن ماجه وأحمد 

 

[Kwa jina la Allaah  ambae hakidhuru kwa jina lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, nae ni Msikivu na ni Mjuzi.]    (mara tatu )     [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy na Ahmad.]

 

رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّـاً وَبِالإسْلامِ ديـناً وَبِمُحَـمَّدٍ  صََلى الله عليه وسلم  نَبِيّـاً ]    ثلاث مرات ]

أحمد 4/ 337 والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 4 وابن السني برقم 68 وأبو داود 4/418 والترمذي 5/465

[Nimeridhika kuwa Allaah ndie Mola wangu, na Uislamu ndio dini yangu, na Muhammad ﷺ  kuwa ni Mtume wangu.]          [Imepokewa na Ahmad na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]

 

 

يا حَـيُّ يا قَيّـومُ بِـرَحْمَـتِكِ أَسْتَـغـيث ، أَصْلِـحْ لي شَـأْنـي كُلَّـه ، وَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـين

الحاكم وصححه ووافقه الذهبي 1/ 545 وانظر صحيح الترغيب والترهيب 1/273

 

[Ewe Uliyehai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu  yote, wala usiniachie  mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia) hata kwa muda (mdogo kama muda) wa kupepesa jicho]      [Imepokewa na Haakim na akasahihisha na kuafikiwa na Al-Dhahabiy.]

 

أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم ، فَـتْحَهُ ، وَنَصْـرَهُ ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ ، وَهُـداهُ ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه

 أبو داود 4/ 322 وحسن إسناده شعيب وعبد القادر الأرناؤوط في تحقيق زاد المعاد 2/ 273

 

[Tumeingia asubuhi  na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Allaah, Mola wa viumbe vyote, Ee Allaah   hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii.]      [Imepokewa na Abuu Daud.]

 

Na ikiingia jioni useme:

 

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة ، فَتْحَهـا ، وَنَصْـرَهـا ، وَنـورَهـا وَبَـرَكَتَـهـا ، وَهُـداهـا ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا 

 

[Tumeingia jioni  na imefika jioni na Ufalme ni wa Allaah, Mola wa viumbe vyote, Ee Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya usiku huu,  ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu.]

 

أَصْـبَحْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام ، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص ، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

 أحمد  3/ 406 و 407 وابن السني في عمل اليوم والليلة برقم 34 وانظر : صحيح الجامع 4/ 209

 

[Tumeingia asubuhi na maumbile ya kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad  ﷺ na mila (dini) ya baba yetu Ibraahiym iliyo sawa hali yakuwa  musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.]       [Imepokewa na Ahmad na Ibnu Sunniy.]

Na ikiingia jioni Aseme:

 

أَمْسَيْنا  علـى فِطْـرَةِ الإسْلام ، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص ، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

 

[Tumeingia jioni na maumbile ya kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad ﷺ na mila (dini) ya baba yetu Ibraahiym iliyo sawa hali yakuwa  musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Allaah.]

 

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ]  مائة مرة ]

 رواه مسلم4 / 2071 

[Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema zote nizake.]   mara mia moja      [Imepokewa na  Muslim.]

 

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير]    عشر مرات أو مرة واحدة عند الكسل]

أبو داود 4/319 وابن ماجه وأحمد 4/60

 

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah  peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake sifa njema zote na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah]

 

Amesema Mtume  Mwenye kusema inapoingia asubuhi

 

[ لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير ]

 

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah  peke yake hana mshirika wake, niwake Ufalme na nizake  sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.]

kwa siku mara mia, basi ana thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikwa thawabu mia  moja na atafutiwa madhambi mia moja, na atakuwa na kinga ya shetani kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake.   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

 سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه ]       ثلاث مرات إذا أصبح]

مسلم 4/2090

[Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake, kwa hisabu ya viumbe vyake, na radhi yake, na uzito wa arshi yake, na wino wa maneno yake.]  mara tatu kila asubuhi  [Imepokewa na Muslim.]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً وَرِزْقـاً طَيِّـباً ، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً]   إذا أصبح]

 أخرجه ابن السني في عمل اليوم والليلة برقم 54وابن ماجه برقم 925وحسن إسناده عبد القادر وشعيب الأرناؤوط في تحقيق زاد المعاد 2/375

 

[Ee Allaah, nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa]    Kila Asubuhi.      [Imepokewa na Ibnu Sunniy na Ibnu Maajah.]

 أَسْتَغْفِرُ الَّلهَ وَ أَتُوبُ إِلَيْهِ ]   مائة مرة في اليوم]

البخاري مع الفتح 11/ 101 ، ومسلم 4/ 2075

[Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu na ninarejea Kwake.]  mara  mia kwa siku    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

Alikuwa Mtume ﷺ akisema asubhuhi  na jioni :

 

[ أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ ]

 

[Najilinda na maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari aliyoiumba.]  mara tatu jioni  

Mwenye  kuisema jioni mara tatu hatodhuriwa na mdudu wa sumu (kama nyoka au kitumbo-ng'e) usiku huo . [Imepokewa na Ahmad na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy]

 

 اللهم صل وسلم على نبينا محمد ]   عشر مرات]

 

[Ewe Mwenyezi Mungu mfikishie rehma na amani Mtume wetu Muhammad ﷺ]

Asema Mtume 

[Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shifaa (msamaha) siku ya Qiyaamah.]        [Imepokewa na Al-Twabraniy.]


SIKILIZA NYIRADI ZA ASUBUHI NA JIONI 




KINGA YA MUISLAMU


 فضل وصفة الدعاء بعد الفراغ من الذكر بعد الصلاة 600x332


 

[ أستغفر الله " ثلاثاً .." اللهم أنت السلام ، ومنك السلام ، تباركت يا ذا الجلال والإكرام]

 مسلم1/ 414

[Naomba msamaha Mwenyezi Mungu” (mara tatu)  Ewe Mwenyezi Mungu  Wewe ndie Amani, na Kwako ndiko kutokako amani, Umetukuka Ewe Mwenye Utukufu na Ukarimu]   [Imepokewa na Muslim]

  

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ اللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ 

البخاري 1 /255 ومسلم 1 / 414

[Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu  hali ya kuwa peke yake hana mshirika, niwake Ufalme, na ni Zake sifa njema, na Yeye ni muweza wa kila kitu.  Ewe Mwenyezi Mungu  hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri kwani kwako wewe ndio utajiri.]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

لا إله إلا الله وحده لا شريك له،له الملك وله الحمد وهو على كل شئ قدير،لا حول ولا قوة إلا بالله،لا إله إلا الله،ولا نعبد إلا إياه ، له النعمة وله الفضل ،وله الثناء الحسن،لا إله إلا الله مخلصين له الدين ولو كره الكافرون        مسلم 1/ 415

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu  hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake  sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza, hapana uwezo  wala nguvu ila vyote vinatokana  na Mwenyezi Mungu  hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, wala hatumuabudu ila Yeye, ni Zake neema, na niwake ubora, na nizake sifa nzuri zote, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kumtakasia dini yake, ijapokuwa wanachukia makafiri.]      [Imepokewa na Muslimu.]

 

 [سبحان الله ، والحمد لله ، والله أكبر ( ثلاثاً وثلاثين ) لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير ]

مسلم 1/ 418من قال ذلك دبر كل صلاة غفرت خطاياه وإن كانت مثل زبد البحر مسلم 1/ 418

[Ametakasika Mwenyezi Mungu” (mara thelathini na tatu) "Sifa njema zote niza Mwenyezi Mungu” (mara thelathini na tatu) "Mwenyezi Mungu  ni Mkubwa” (mara thelathini na tatu), Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu , hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme na nizake sifa njema na Yeye ni Mueza wa kila kitu.]      [Imepokewa na Muslim.]

Kisha utasoma  Suratul-Ikhlaas, Na Suratul-Falaq na Suratu-Nnas, yaani

 

بسم الله الرحمن الرحيم{ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ*اللَّهُ الصَّمَدُ*لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ * وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَدٌ} بسم الله الرحمن الرحيم {قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ * مِن شَرِّ مَا خَلَقَ *وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ * وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ * وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ } بسم الله الرحمن الرحيم{ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ * مَلِكِ النَّاسِ * إِلَهِ النَّاسِ *مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ * الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ * مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ } بعد كل صلاة مرة واحدة , وبعد صلاة المغرب والفجر ثلاث مرات

أبو داود 2/86 والنسائي 3/ 68 وانظر صحيح الترمذي 2/8

Kila baada ya swala mara moja, na baada ya swala ya Alfajiri na Magharibi utasoma hizo mara tatu tatu.        

Pia ni katika sunna kusoma Aayatul Kursiy baada ya kila Swala Nayo ni: 

 

اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ }  عقب كل صلاة

 من قرأها دبر كل صلاة لم يمنعه من دخول الجنة إلا أن يموت . والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 100 ، وابن السني برقم 121 وصححه الجامع 5/339 وسلسلة الأحاديث الصحيحة 2/697 برقم 972

[Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.]           [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy.]

 

لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد ، يحيي ويميت وهو على كل شئ قدير ]  عشر مرات بعد صلاة المغرب والصبح]

رواه الترمذي 5/515 وأحمد 4/ 227 وانظر تخريجه في زاد المعاد 1/300   

 [Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki, ila Mwenyezi Mungu, hali yakuwa peke yake, hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na nizake sifa njema, anahuisha, anafisha, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.]  Mara kumi baada ya Swala ya Alfajiri na ya Magharibi.]     [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ahmad.]    

 

[ اللهم إني أسألك علماً نافعاً ، ورزقاً طيباً ، وعملاً متقبلاً "بعد السلام من صلاة الفجر ] 

 ابن ماجه وغيره وانظر صحيح ابن ماجة1/ 152 ومجمع الزوائد 10/111

 

[Ewe Mwenyezi Mungu  nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa.]    Baada ya kutoa salamu ya Swala ya Alfajiri   [Imepokewa na Ibnu Maajah]


SIKILIZA NYIRADI BAADA YA KUTOA SALAM




KINGA YA MUISLAMU


 اجمل دعاء للحبيب


Amesema Jaabir Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu  akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur’an. Anasema   ‘Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:

 

 اللهم إني أستخيرك بعلمك ، وأستقدرك بقدرتك ، وأسألك من فضلك العظيم فإنك تقدِرُ ولا أقدِرُ ، وتعلم ولا أعلم ، وأنت علام الغيوب ، اللهم إن كنت تعلم أن هذا الأمر -يسمي حاجته - خير لي في ديني ومعاشي وعاقبة أمري - أو قال : عاجلة وآجله - فاقدره لي ويسره لي ، ثم بارك لي فيه ، وإن كنت تعلم أن هذا الأمر شر لي في ديني ومعاشي وعاقبة أمري - أو قال : عاجله وآجله - فاصرفه عني واصرفني عنه ، واقدر لي الخير حيث كان ، ثم ارضني به

 

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yaliyofichikana.   Ewe Mwenyezi Mungu  iwapo jambo hili kutokana na ujuzi wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali ) basi nakuomba uniwezeshe nilipate, na unifanyie wepesi, kisha  unibariki, na iwapo unajua kwamba  jambo hili ni shari kangu katika dini yangu namaisha yangu na mwisho wa  jambo langu (karibu na mbali) basi liepushe na mimi naminiepushe nalo, na  nipangie  jambo jengine lenye  kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo.]          [Imepokewa na Bukhari]

 

وما ندم من استخار الخالق ، وشاور المخلوقين المؤمنين وتثبت في أمره ، فقد قال سبحانه  { وَشَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ

 

Na hajuti mwenye kumtaka ushauri (muelekezo) Mwenyezi Mungu  na akawashauri waja waumini na akajidhatiti jambo lake Amesema Mwenyezi Mungu 

kumwambia Mtume Wake [Na ushauriane nao katika mambo, na ukiazimia kufanya jambo, basi tegemea kwa Mwenyezi Mungu]   Suratul Imraan: 159


SIKILIZA DUA YA SWALATUL-ISTIKHARA




KINGA YA MUISLAMU


 a muslim man praying alone


 

اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،ومن عذاب جهنم،ومن فتنة المحيا والممات ،ومن شر فتنة المسيح الدجال

البخاري 2/ 102 ومسلم 1/ 412 واللفظ لمسلم 

[Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakutaka unihifadhi na adhabu za kaburi, na adhabu ya (moto wa) jahannam, na fitna ya uhai, na ya kufa, na shari ya fitna ya Masihi-dajjaal.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر،وأعوذ بك من فتنة المسيح الدجال،وأعوذ بك من فتنة المحيا والممات، اللهم إني أعوذ بك من المأثم والمغرم 

البخاري 1/ 202 ومسلم 1/ 412  

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najilinda Kwako kutokana  na fitna ya Masihi-dajjaal, na najilinda Kwako kutokana na fitna ya uhai na ya mauti, Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda Kwako kutokana na dhambi na deni.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

 اللهم إني ظلمت نفسي ظلماً كثيراً ، ولا يغفر الذنوب إلا أنت ، فاغفر لي مغفرة من عندك وارحمني إنك أنت الغفور الرحيم 

البخاري 8/168 ومسلم 4/ 2078

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, dhulma kubwa, na hasamehe madhambi ila Wewe, basi nisamehe msamaha kutoka Kwako, na unirehemu, hakika Wewe  ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kurehemu]        [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

[ اللهم اغفر لي ما قدمت وما أخرت وما أسررت وما أعلنت وما أسرفت وما أنت أعلم به مني أنت المقدم وأنت المؤخر لا إله إلا أنت]

 مسلم 1/ 534

[Ewe Mwenyezi Mungu  nisamehe niliyoyatanguliza, na niliyoyachelewesha, na niliyoyafanya kisiri, na niliyoyafanya kwa dhahiri na niliyoruka mipaka, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi, Wewe ndiye mwenye kutanguliza na Wewe ndiye mwenye kuchelewesha, hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.]       [Imepokewa na Muslim]

 

[ اللهم أعني على ذكرك ، وشكرك وحسن عبادتك]

 أبو داود 2/ 86والنسائي 3/ 53 وصححه الألباني في صحيح أبو داود 1/ 284

[Ewe Mwenyezi Mungu  nisaidie kukukumbuka, na kukushukuru, na uzuri wa kukuabudu]      [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Nnasai na kusahihishwa na Al-Baaniy katika Sunan Abii Daudu]

 

[ اللهم إني أعوذ بك من البخل وأعوذ بك من الجبن ، وأعوذ بك من أن أرد إلى أرذل العمر ، وأعوذ بك من فتنة الدنيا وأعوذ بك من عذاب القبر ]

 البخاري 6/35

[Ewe Mwenyezi Mungu  najilinda Kwako kutokana na ubakhili, na najilinda kwako kutokana na uwoga, na najilinda kwako kutokana na kurudishwa kwenye umri duni, na najilinda kwako kutokana  na fitna ya dunia na adhabu ya kaburi]            [Impokewa na Bukhari]

 

[ اللهم إني أسألك الجنة وأعوذ بك من النار ]

 أبو داود وانظر صحيح ابن ماجه 2/ 328

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakuomba pepo na najilinda kwako kutokana na moto.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah]

 

 اللهم بعلمك الغيب وقدرتك على الخلق أحيني ما علمت الحياة خيراً لي وتوفني إذا علمت الوفاة خيراً لي ، اللهم إني أسألك خشيتك في الغيب والشهادة ، وأسألك كلمة الحق في الرضا والغضب ، وأسألك القصد في الغنى والفقر ، وأسألك نعيماً لا ينفد ، وأسألك قرة عين لا تنقطع ، وأسألك الرضا بعد القضاء ، وأسألك برد العيش بعد الموت ، وأسألك لذة النظر إلى وجهك والشوق إلى لقائك من غير ضرَّاء مضرة ولا فتنة مضلة ، اللهم زينا بزينة الإيمان ، واجعلنا هداة مهتدين

 النسائي 4/54،55وأحمد  4/364 وصححه الألباني في صحيح النسائي 1/ 281

[Ewe Mwenyezi Mungu , kwa ujuzi Wako wa mambo yaliyo fichikana, na uwezo Wako wa kuumba, niweke hai iwapo uhai ni bora kwangu, na nifishe iwapo kufa ni bora kwangu, Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakuomba khofu yako kwa siri na dhahiri na ninakuomba neno la haki wakati nimefurahi na wakati nimekasirika, na ninakuomba matumizi ya wastani wakati wa utajiri na wakati wa umaskini, na ninakuomba neema isiyokwisha na ninakuomba kituliza jicho (moyo) kisicho katika, na ninakuomba  kuridhia baada yakuwa umeshanipangia, na ninakuomba maisha ya utulivu baada ya kufa, na ninakuomba ladha ya kukutizama uso Wako, na shauku ya kukutana nawe, pasina madhara yanayodhuru, wala fitna yenye kupoteza.  Ewe Mwenyezi Mungu  tupambe kwa kipambo cha imani, na tujaalie tuwe waongozi wenye kuongoka.]                       [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ahmad na imesahihishwa na Al-Baaniy katika swahihi Al-Nnasaai]

 

[ اللهم إني أسألك يا الله بأنك الواحد الأحد الصمد الذي لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفواً أحد أن تغفر لي ذنوبي إنك أنت الغفور الرحيم ]

أخرجه النسائي بلفظه 3/52وأحمد 4/338 وصححه الألباني في صحيح النسائي 1/ 280

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakuomba, Ewe Mwenyezi Mungu  kwa vile Wewe ni Mmoja ulie pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote, nakuomba unisamehe makosa yangu hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe,, Mwenye kurehemu.]          [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ahmad na imesahihishwa na Al-Baaniy katika swahihi Al-Nnasaai.]

 

 اللهم إني أسألك بأن لك الحمد ، لا إله إلا أنت وحدك لا شريك لك ، المنان ، يا بديع السموات والأرض يا ذا الجلال والإكرام يا حي يا قيوم إني أسألك الجنة وأعوذ بك من النار 

رواه أهل السنن وانظر صحيح ابن ماجه 2/ 329

[Ewe Mwenyezi Mungu  hakika mimi nakuomba, kwa vile sifa njema zote ni Zako, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali yakuwa pekeyako, huna mshirika, mwingi wa kuneemesha.  Ewe Mtangulizi (muumbaji) wa mbingu na ardhi (bila kuwa na mfano kabla), Ewe mwenye Utukufu na  ukarimu, Ewe Ulie hai mwenye kusimama kwa dhati  Yako, hakika mimi nakuomba pepo , na najilinda  kwako kutokana  na moto.]         [Imepokewa kwenye vitabu vya Sunna]

 

[اللهم إني أسألك بأني أشهد أنك أنت الله لا إله إلا أنت،الأحد الصمد الذي لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفواً أحد]

أبو داود2/62 والترمذي 5/ 515 وابن ماجه 2/ 1267 وأحمد 5/360 وانظر صحيح ابن ماجه 2/ 329 وصحيح الترمذي 3/ 163

[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa vile ninakiri kwa hakika kwamba Wewe ni Mwenyezi Mungu  hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa pekee, mwenye kutegemewa kwa haja zote, ambae hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna mfano wake na kitu chochote]       [Imepokewa na Abuu Daud, na Al-Ttirmidhiy, na Ibnu Maajah,na Ahmad ]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6488929
TodayToday2035
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 83

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676f5f35434115176627291735352117
title_676f5f354352e10989320751735352117
title_676f5f354365119004435501735352117

NISHATI ZA OFISI

title_676f5f3550a0b15586391711735352117
title_676f5f3550b119554908241735352117
title_676f5f3550c0d5732490081735352117 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 5 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com