SOMO LA FIQHI
MAANA YA ITIKAFU
Itikafu ki-lugha: Ni kujilazimisha na jambo fulani, na kujifunga nafsi yako juu ya kulifanya jambo hilo.
Ama Maana ya Itikafu ki-sheria:
Ni kujilazimisha kukaa ndani ya msikiti kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu.
Usharia wa Itikafu
Kufanya itikafu ni katika matendo yaliyo bora sana, na twa’a tukufu. Kutoka kwa A’isha Mungu awe naye radhi anasema:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعْتَكِفُ الْعَشْرَ الأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ] رواه البخاري ومسلم]
[Alikuwa Mtume ﷺ akifanya itikafu katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
Na inaruhusiwa ki-sheria kwetu sisi na kwa waliokuja kabla yetu kufanya itikafu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ} البقرة:125}
[Na tuliagana na Ibrahim na Ismail: Itakaseni Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu na wanao jitenga huko kwa ibada, na wanao inama na kusujudu.] [Al-Baqarah –Aya 125].
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.