SOMO LA FIQHI
Hukumu ya Kukaa Itikafu
"Kufanya itikafu ni Sunna wakati wowote ule, na ubora wake zaidi kuifanya ni katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani; kwasababu Mtume ﷺ alidumu katika kufanya itikafu kwenye kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani" [Zaadul-Ma’ad.].
Masharti ya Kukaa Itikafu
1. Kutia niya.
Mwenye kufanya itikafu anatia niya ya kujilazimisha kukaa ndani ya msikiti kwa lengo la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kumuabudu; kwa kauli ya Mtume ﷺ:
إنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ] رواه البخاري ومسلم]
[Hakika kila Amali ni kwa niya ya mtu] [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
2. Msikiti atakaofanyia Itikafu uwe ni msikiti wa kuswali swala ya jumaa.
Haifai kufanya Itikafu isipokuwa Msikitini kwa neno lake Mwenyezi Mungu:
وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ} البقرة:187}
[Hali yakuwa mumekaa itikafu msikitini] [Al-baqara: 187]
Na kwa kitendo chake Mtume ﷺ kwani hakufanya Itikafu isipokuwa Msikitini.
Na kufanya itikafu msikiti usio swaliwa Jamaa itampelekea Mwenye kufanya Itikafu kutoka mara kwa mara kuenda kuswali jamaa kwa sababu Swala ya jamaa kwake ni wajibu, na kule kutoka mara kwa mara hukosekana maana ya Itikafu. Ama mwanamke husihi Itikafu yake msikiti wowote sawa uwe msikiti waswaliwa jamaa au hauswaliwi, na hii ni ikipelekea kutopatikana fitna katika kukaa kwake itikafu, ama ikipatikana fitna haifai na atakatazwa.
Na ubora uwe msikiti unaswaliwa swala ya ijumaa lakini hilo si katika masharti ya itikafu
3. Kuwa twahara kutokamana na hadathi kubwa.
Haifai kwa mwenye janaba kufanya Itikafu, wala mwenye damu ya heidhi, wala mwenye damu ya nifasi, kwa kule kukosekana kwao ruhusa ya kukaa ndani ya msikiti.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.