SOMO LA FIQHI
Mwenye kuenda hija, ima huwa ametia nia ya kufanya (Tamattu’ ) Kufanya umra kisha kupumzika mpaka wakati wa haji au ametia nia ya ( Qiraan ) nayo nikutia nia ya umra na hija pamoja, na ima awe ametia nia ya(Ifraad) hija pekeyake mwenye kutia nia yatamatt’ huwa ametoka kwenye amali ya hija na akatoka kwenye ihram, ama mwenye kufanya qiraan na ifraad watabaki kwenye ihram zao, na shughuli za Hijja zinaanza terehe nane Mfungotatu. Mpaka siku ya kumi na tatu, Na maelezo yake ni kama yafuatayo kwa masiku:
Siku ya nane ya Mfungotatu (siku ya Tarwiyah)
1. Siku ya nane ni sunna kwa mja kuhirimia hijja kabla ya adhuhuri atahirimia pale alipo, ataoga, atajitia manukato, na atavaa nguo za ihramu na atasema:
لبيك اللهم لبيك .. لبيك لا شريك لك لبيك .. إن الحمد والنعمة لك والملك .. لا شريك لك
LABBAYKA ALLAHUMMA LABBAYKA, LABBAYKA LAA SHARIKA LAKA LABBAYKA, INNAL-HAMDA, WANNI’MATA LAKA WALMULKA, LAA SHARIIKA LAKA
Nimekuitikia, ewe Mola, kwa Hija! Nimekuitika ewe Mola nimekuitika! usiokuwa na mshirika nimekuitika! Sifa njema zote na neema ni zako, na ufalme, Usiokuwa na mshirika] [Imepokewa na Bukhari.].
2. Ataelekea Mina, ataswali huko Adhuhuri, Alasiri, na Magharibi, Isha na Alfajiri ya siku ifuatayo.
3. Ataswali kila Swala kwa katika wakati wake. Atazipunguza Swala za rakaa nne-nne azifanye mbilimbili. Na atasalia hapo Mina mpaka kutokea jua la siku ya tisa.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.