SOMO LA FIQHI
1. Kila chenye kutoka kwenye mojawapo ya njia mbili, mfano wa mkojo, choo, upepo (kushuta) kwa neno lake Mwenyezi Mungu :
أو جاء أحد منكم من الغائط } النساء: 43}
[Au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake] [Al Nnisaa:43]
Na kwa Neno lake Mtume ﷺ:
لَا يَقْبَلُ اللَّهُ صَلَاةَ أَحَدِكُمْ إِذَا أَحْدَثَ حتى يتوضأ ] متفق عليه]
[Mwenyezi Mungu hakubali Swala ya mmoja wenu akitokwa na hadathi mpaka atawadhe] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
2. Kulala usingizi mzito ambao mtu hafahamu chochote. Na hi inaingia hapa, kama kukosa fahamu, na kupotezwa fahamu kikamilifu.
Kwa neno lake Mtume ﷺ:
العين وكاء السه فمن نام فليتوضأ،] رواه أحمد وابن ماجه بإسناد حسن]
[Macho mawili ni kifuniko cha Duburi (tupu ya nyuma) kwa yoyote atakae lala basi atawadhe] [Imepokewa na Ahmad na Ibnu Maajah kwa Isnaad mzuri]
3. Kugusa tupu ya mbele au ya nyuma kwa mkono bila ya kizuizi, kwa hadithi iliyo pokelewa na Busra binti Swafawan Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alimsikia mtume ﷺ akisema:
من مس فرجه فليتوضأ ] رواه النسائي وابن ماجه وصححه الألباني في صحيح النسائي ]
[Mwenye kugusa tupu yake na atawadhe] [ Imepokewa na Annasai na Ibnu Maajah na kusahihishwa na Al Bani katika Swahihi Al Nnasai ]
4. Kumgusa Mwanamke wa kando kwa matamanio,kwa neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[أو لا مستم النساء} [النساء: 43}
[Au mmewagusa wanawake] [Annisaa:43]
5. Kula nyama ya ngamia, kwa hadithi ya Jabir bin samurah kwamba mtu alimuuliza Mtume ﷺ:
أنتوضأ من لحوم الإبل؟ قال: نعم توضأ من لحوم الإبل ]. رواه مسلم ]
[Je, tutawadhe kwa kula nyama za ngamia? Akasema: Ndio] [Imepokewa na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.