KINGA YA MUISLAMU
[ اللهم إنا نجعلك في نحورهم ونعوذ بك من شرورهم ]
أبو داود 2/89 وصححه الحاكم ووافقه الذهبي 2/142
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakufanya Wewe uwe katika vifua vyao na tunajikinga kwako na shari zao.] [Imepokewa na Abuu Daud na Kusahihishwa na Al-Haakim]
[ اللهم أنت عضدي وأنت نصيري ،بك أجول ،وبك أصول ، وبك أُقاتل ]
أبو داود 3/42 والترمذي 5/572
[Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ndie msaidizi wangu nawe ndie mnusura wangu, kwako ninazunguka na kwako ninavamia na kwako ninapigana.] [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]
[ حسبنا الله ونعم الوكيل ]
البخاري 5/172
[Mwenyezi Mungu anatutosheleza, naye ni mbora wa kutegemewa.] [Imepokewa na Bukhari.]
DUA YA ANAEKUTANA NA ADUI AU MWENYE KUTAWALA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.