KINGA YA MUISLAMU
اللهم صل على محمد وعلى آل محمد ، كما صليت على إبراهيم ، وعلى آل إبراهيم ، إنك حميد مجيد ، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم ، وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد البخاري مع الفتح 6/ 408
[Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad na jamaa zake Muhammad kama uliyomrehemu Ibrahim, na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Ewe Mwenyezi Mungu mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad, kama ulivyo mbariki Ibrahim na jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu.] [Imepokewa na Bukhari.]
اللهم صل على محمد وعلى أزواجه وذريته،كما صليت على آل إبراهيم، وبارك على محمد وعلى أزواجه وذريته كما باركت على آل إبراهيم إنك حميد مجيد
البخاري مع الفتح 6/ 407 ومسلم 1/ 306 واللفظ له
[Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowarehemu jamaa wa Ibrahim. Na mbariki Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama ulivyowabariki jamaa zake Ibrahim, hakika Wewe Umesifika na Umetukuka.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
KUMSWALIA MTUME ﷺ BAADA YA TASHAHHUD
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.