DUA YA KUSOMWA AKIWA AMESIMAMA KATIKA MLIMA WA SWAFAA NA MARWA
Amesema Jaabir radhi za Allah ziwe juu yake, Mtume ﷺ alipokurubia Swafaa alisoma:
[...إِنَّ الصَّفَا والمَرْوَةَ مِنْ شَعائرِ الله]
[Hakika Swafaa na Marwah ni katika alama za kumtukuza Mwenyezi Mungu]
[ أَبْدَأُ بِمَا بَدَأَ اللهُ بِهِ ]
[Ninaanza kwa alichoanza Mwenyezi Mungu]
Akaanza Swafaa akapanda mpaka akaiona Al-Kaabah kisha akaielekea na kusema:
[اللهُ أكْبَرُ, اللهُ أكْبَرُ, اللهُ أكْبَرُ]
[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa]
kisha atasema yafuatayo mara tatu akomba dua (yoyote apendayo) baada ya kila mara:
لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa peke yake, wala hana mshirika wake, ni wake Ufalme nani zake sifa njema naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake, ametekeleza ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na amivishinda vikosi peke yake.]
….. Mtume ﷺ alisoma hivi mara tatu na baina yake akiomba dua, kisha akafanya akiwa Marwah kama alivyofanya Swafaa. [Imepokewa na Muslim.]
DUA YA KUSOMWA AKIWA AMESIMAMA KATIKA MLIMA WA SWAFAA NA MARWA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.