KINGA YA MUISLAMU
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :" لا تدخلوا الجنة حتى تؤمنوا ، ولا تؤمنوا حتى تحابوا ، أو لا أدلكم على شيءٍ إذا فعلتموه تحاببتم
أفشوا السلام بينكم
مسلم 1/74 وغيره
Amesema Mtume ﷺ: [Hamtaingia peponi mpaka muamini, na hamtakuwa waumini wa kweli mpaka mpendane. Hivi niwafahamishe kitu mkikifanya mtapendana? Salimianeni baina yenu.] [Imepokewa na Muslim na wengineo.]
ثلاث من جمعهن فقد جمع الإيمان : الإنصاف من نفسك ، وبذل السلام للعالم ،والإنفاق من الإقتار
البخاري مع الفتح 1/ 82
Amesema Ammar Bin Yaasir radhi za Allah ziwe juu yake [Mambo matatu anaeyakusanya basi amekusanya Imani: uadilifu wa nafsi yako, na kutowa salam kwa watu wote na kutoa (sadaka) hali ya kuwa ni mchache wa mali] [Imepokewa na Bukhari.]
وعن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما : أن رجلاً سأل النبي صلى الله عليه وسلم أي الإسلام خير قال :" تطعم الطعام وتقرأ السلام على من عرفت ومن لم تعرف
البخاري مع الفتح 1/55 ومسلم 1/65
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omar radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ Ni uislamu gani bora? Mtume ﷺ akamjibu, [Kulisha (maskini) na kumsalimia unaemjua na usiemjua] [Imepokelewa na Bukhari na Muslim.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.