DUA YA WAKATI WA KUFUNGUA SAUMU
[ ذَهبَ الظَّمأُ، وابتلَّت العروقُ وثَبَتَ الأجرُ إنْ شاء الله ]
أخرجه أبي داود 2/306 وغيره
[Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na amethibiti malipa Allaah Akipenda.] [Impokewa na Abuu Daud na wengineo]
Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ: [Aliyefunga wakati wa kufuturu kwake ana du'aa isiyorudishwa.]
[ اللهم إني أسألك برحمتك التي وسعت كل شيءٍ أن تغفر لي ]
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kwa rehema zako ambazo zimeenea kila kitu, unisamehe.] [Imepokewa na Ibnu Maajah.]
DUA YA WAKATI WA KUFUNGUA SAUMU
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.