DUA KABLA YA KULA
:إذا أكل أحدكم الطعام فليقل
Atakapo kula mmoja wenu chakula basi aseme:
[ بِسْمِ الله ]
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu]
Na akisahau mwanzo wake basi aseme:
[بِسمِ الله في أوله وآخره]
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake] [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy]
Amesema Mtume ﷺ:
من أطعمه الله الطعام فليقل
Yeyote ambae Mwenyezi Mungu amemruzuku chakula aseme:
[اللهم بارك لنا فيه وأطعمنا خيراً منه]
[Ewe Mwenyezi Mungu tubariki katika chakula hichi na tulishe bora kuliko hichi.]
ومن سقاه الله لبناً فليقل
Na yoyote ambae amemruzuku maziwa basi aseme:
[اللهم بارك لنا فيه وزدنا منه]
[Ewe Mwenyezi Mungu tubarikie kinywaji hichi na utuzidishie] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]
DUA KABLA YA KULA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.