KINGA YA MUISLAMU
Amesema Mtume ﷺ [muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mumini dhaifu, na wote wana kheri. Fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha na taka msaada kwa Mwenyezi Mungu wala usichoke na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme “lau” kama ningefanya kadha na kadha yasingenitokea haya, lakini sema:
[ قدر الله وما شاء فعل ]
[Amepanga Mwenyezi Mungu na analolitaka anafanya]
…… hakika neno la “lau” linafungua matendo ya shetani’ [Imepokewa na Muslim.]
Hakika Mwenyezi Mungu analaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo na ukishindwa na jambo kabisa sema:
[ حسبي الله ونعم الوكيل ]
[Mwenyezi Mungu ananitosheleza, naye ni Mbora wa kutegemewa.]
SIKILIZA DUA HII
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.