KINGA YA MUISLAMU
Amesema Jaabir Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akitufundisha Swala ya Istikhara kama vile anavyotufunza sura ya Qur’an. Anasema ﷺ ‘Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:
اللهم إني أستخيرك بعلمك ، وأستقدرك بقدرتك ، وأسألك من فضلك العظيم فإنك تقدِرُ ولا أقدِرُ ، وتعلم ولا أعلم ، وأنت علام الغيوب ، اللهم إن كنت تعلم أن هذا الأمر -يسمي حاجته - خير لي في ديني ومعاشي وعاقبة أمري - أو قال : عاجلة وآجله - فاقدره لي ويسره لي ، ثم بارك لي فيه ، وإن كنت تعلم أن هذا الأمر شر لي في ديني ومعاشي وعاقبة أمري - أو قال : عاجله وآجله - فاصرفه عني واصرفني عنه ، واقدر لي الخير حيث كان ، ثم ارضني به
[Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakutaka ushauri (muelekezo) kwa ujuzi Wako, na nakuomba uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe unaweza, nami siwezi, nawe unajua nami sijui, nawe nimjuzi wa yale yaliyofichikana. Ewe Mwenyezi Mungu iwapo jambo hili kutokana na ujuzi wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali ) basi nakuomba uniwezeshe nilipate, na unifanyie wepesi, kisha unibariki, na iwapo unajua kwamba jambo hili ni shari kangu katika dini yangu namaisha yangu na mwisho wa jambo langu (karibu na mbali) basi liepushe na mimi naminiepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo.] [Imepokewa na Bukhari]
وما ندم من استخار الخالق ، وشاور المخلوقين المؤمنين وتثبت في أمره ، فقد قال سبحانه { وَشَاوِرْهُمْ فِي الأَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ
Na hajuti mwenye kumtaka ushauri (muelekezo) Mwenyezi Mungu na akawashauri waja waumini na akajidhatiti jambo lake Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ
kumwambia Mtume Wake ﷺ [Na ushauriane nao katika mambo, na ukiazimia kufanya jambo, basi tegemea kwa Mwenyezi Mungu] Suratul Imraan: 159
SIKILIZA DUA YA SWALATUL-ISTIKHARA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.