KINGA YA MUISLAMU
[ أستغفر الله " ثلاثاً .." اللهم أنت السلام ، ومنك السلام ، تباركت يا ذا الجلال والإكرام]
مسلم1/ 414
[Naomba msamaha Mwenyezi Mungu” (mara tatu) Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ndie Amani, na Kwako ndiko kutokako amani, Umetukuka Ewe Mwenye Utukufu na Ukarimu] [Imepokewa na Muslim]
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ اللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ
البخاري 1 /255 ومسلم 1 / 414
[Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika, niwake Ufalme, na ni Zake sifa njema, na Yeye ni muweza wa kila kitu. Ewe Mwenyezi Mungu hapana anaeweza kukizuia ulichokitoa, na wala kutoa ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri kwani kwako wewe ndio utajiri.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
لا إله إلا الله وحده لا شريك له،له الملك وله الحمد وهو على كل شئ قدير،لا حول ولا قوة إلا بالله،لا إله إلا الله،ولا نعبد إلا إياه ، له النعمة وله الفضل ،وله الثناء الحسن،لا إله إلا الله مخلصين له الدين ولو كره الكافرون مسلم 1/ 415
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na Yeye juu ya kila kitu ni Mueza, hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Mwenyezi Mungu hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, wala hatumuabudu ila Yeye, ni Zake neema, na niwake ubora, na nizake sifa nzuri zote, hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila Mwenyezi Mungu, hali ya kumtakasia dini yake, ijapokuwa wanachukia makafiri.] [Imepokewa na Muslimu.]
[سبحان الله ، والحمد لله ، والله أكبر ( ثلاثاً وثلاثين ) لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير ]
مسلم 1/ 418من قال ذلك دبر كل صلاة غفرت خطاياه وإن كانت مثل زبد البحر مسلم 1/ 418
[Ametakasika Mwenyezi Mungu” (mara thelathini na tatu) "Sifa njema zote niza Mwenyezi Mungu” (mara thelathini na tatu) "Mwenyezi Mungu ni Mkubwa” (mara thelathini na tatu), Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu , hali ya kuwa peke yake hana mshirika wake, ni wake Ufalme na nizake sifa njema na Yeye ni Mueza wa kila kitu.] [Imepokewa na Muslim.]
Kisha utasoma Suratul-Ikhlaas, Na Suratul-Falaq na Suratu-Nnas, yaani
بسم الله الرحمن الرحيم{ قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ*اللَّهُ الصَّمَدُ*لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ * وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَدٌ} بسم الله الرحمن الرحيم {قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ * مِن شَرِّ مَا خَلَقَ *وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ * وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ * وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ } بسم الله الرحمن الرحيم{ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ * مَلِكِ النَّاسِ * إِلَهِ النَّاسِ *مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ * الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ * مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ } بعد كل صلاة مرة واحدة , وبعد صلاة المغرب والفجر ثلاث مرات
أبو داود 2/86 والنسائي 3/ 68 وانظر صحيح الترمذي 2/8
Kila baada ya swala mara moja, na baada ya swala ya Alfajiri na Magharibi utasoma hizo mara tatu tatu.
Pia ni katika sunna kusoma Aayatul Kursiy baada ya kila Swala Nayo ni:
اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ } عقب كل صلاة
من قرأها دبر كل صلاة لم يمنعه من دخول الجنة إلا أن يموت . والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 100 ، وابن السني برقم 121 وصححه الجامع 5/339 وسلسلة الأحاديث الصحيحة 2/697 برقم 972
[Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu.] [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy.]
لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك وله الحمد ، يحيي ويميت وهو على كل شئ قدير ] عشر مرات بعد صلاة المغرب والصبح]
رواه الترمذي 5/515 وأحمد 4/ 227 وانظر تخريجه في زاد المعاد 1/300
[Hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki, ila Mwenyezi Mungu, hali yakuwa peke yake, hana mshirika wake, ni wake Ufalme, na nizake sifa njema, anahuisha, anafisha, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.] Mara kumi baada ya Swala ya Alfajiri na ya Magharibi.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Ahmad.]
[ اللهم إني أسألك علماً نافعاً ، ورزقاً طيباً ، وعملاً متقبلاً "بعد السلام من صلاة الفجر ]
ابن ماجه وغيره وانظر صحيح ابن ماجة1/ 152 ومجمع الزوائد 10/111
[Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa.] Baada ya kutoa salamu ya Swala ya Alfajiri [Imepokewa na Ibnu Maajah]
SIKILIZA NYIRADI BAADA YA KUTOA SALAM
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.