Menu

KINGA YA MUISLAMU


 azkar 


Imepokelewa kutoka kwa  Anas  Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:  Amesema Mtume [Kukaa pamoja na watu wanaomtaja Mwenyezi Mungu  Aliyetukuka  kuanzia Swalah ya Al-Fajiri  mpaka kuchomoza jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuacha huru watu wanne miongoni mwa wana wa Ismail na kukaa na watu wanaomtaja  Mwenyezi Mungu  Aliyetukuka  kuanzia baada ya Swalah ya Al-Asiri mpaka kuchwa jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuwaacha huru watu wanne.]      [Imepokewa na Abuu Daud].

 

اللّهُ لاَ إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

 

Mwenye kusoma (Ayatul-Kursiy) pindi anapoamka atalindwa  kutokana na majini mpaka jioni, na atakaeisoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi.     [Imepokewa na Hakim na Al-Twabraniy na kusahihishwa na Al-Baaniy]

 

قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ


قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ


قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

ثلاث مرات

من قالها ثلاث مرات حين يصبح وحين يمسي كفته من كل شيء . أبو داود 4/ 322 والترمذي 5/ 567وانظر صحيح الترمذي 3/ 182

 

[Mwenye kusisoma (sura hizi) mara tatu asubuhi na jioni zinamtosheleza na kila kitu.]      [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]

 

أصبحنا وأصبح الملك لله، والحمد لله، لا إله إلا الله وحده لا شريك له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير، ربِّ أسألك خير ما في هذا اليوم وخير ما بعده وأعوذ بك من شر ما في هذا اليوم وشر ما بعده ربِّ أعوذ بك من الكسل وسوء الكبر، ربَّ أعوذ بك من عذابٍ في النار وعذاب في القبر

مسلم 4/ 2088

[Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah , na sifa njema ni zake Allaah , hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Allaah , hali yakuwa peke yake, hana mshirika.  Niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ee Mola, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajilinda Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Ee Mola, najilinda Kwako, kutokana  na uvivu, na ubaya wa uzee (uzee mbaya) Ee Mola najilinda Kwako kutokana na adhabu ya  moto na adhabu ya kaburi.]    [Imepokewa na Muslim.]

Na ikiingia jioni useme

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير ، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر     مسلم 4/ 2088

[Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah , na sifa njema ni zake Allaah , hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki, ila Allaah , hali yakuwa peke yake, hana mshirika.  Niwake Ufalme, na nizake sifa njema, na yeye juu ya kila kitu ni muweza, Ee Mola, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajilinda Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Ee Mola, najilinda Kwako, kutokana  na uvivu, na ubaya wa uzee (uzee mbaya) Ee Mola najilinda Kwako kutokana na adhabu ya  moto na adhabu ya kaburi]     [Imepokewa na Muslim.]

 

[اللهم بك أصبحنا وبك أمسينا وبك نحيا وبك نموت وإليك النشور]

الترمذي 5/ 466 وانظر صحيح الترمذي 3/ 142

[Ee Allaah  kwa sababu yako tumeingia katika asubuhi, na kwa ajili yako tumeingia jioni, na kwa ajili yako ndio  tumekuwa hai, na kwa ajili yako tutakufa, na kwako tutafuliwa.]      [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]

 

Na ikifika jioni aseme

 

[اللهم بك أمسينا، وبك أصبحنا، وبك نحيا وبك نموت، وإليك المصير]

الترمذي 5/ 466 وانظر صحيح الترمذي 3/ 142

[Ee Allaah  kwa ajili yako tumefika jioni, na kwa ajili yako tumefika asubuhi, na kwa ajili yako tuko hai na kwa ajili yako tutakufa na ni kwako tu marejeo.]        [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]

 

اللهم أنت ربي لا إله إلا أنت خَلَقتني وأنا عَبْدُك وأنا على عهدك ووعدك ما استطعت أعوذ بك من شر ما صنعت أبوء لك بنعمتك علي وأبوء بذنبي فاغفر لي فإنه لا يغفر الذنوب إلا أنت          أخرجه البخاري 7/150

 

[Ee Allaah  Wewe ni Mola wangu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja wako, nami niko juu ya  ahadi yako, na agano lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda kwako kutokana  na shari ya nilicho kifanya, nakiri  kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe.]    [Imepokewa na Bukhari.]

 

اللهم إني أصبحت  أشهدك وأشهد حملة عرشك ، وملائكتك وجميع خلقك ، أنك أنت الله لا إله إلا أنت وحدك لا شريك لك ، وأن محمداً عبدك

ورسولك"  (أربع مرات حين يصبح أو يمسي 

أخرجه أبو داود 4/ 317 والبخاري في الأدب المفرد برقم 1201 والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 9، وابن السني

 

[Ee Allaah  hakika mimi nimefika asubuhi nakushuhudia na nina washuhudia wabeba wa arshi yako na malaika wako, na viumbe vyako vyote kwamba Wewe ndiye Allaah  hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, hali ya kuwa peke yako huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wako na ni Mtume wako.]     (Atasema hivi mara nne, asubuhi au jioni)  Atakaye yasema haya asubuhi au jioni mara nne Mwenyezi Mungu aliyetukuka atamuepusha na moto. [Imepokewa na Abuu Daud na Bukhari katika Adabul-Mufrad na Al-Nnasai na Ibnu Sunniy.]

 

[اللهم ما أصبح بي من نعمة أو بأحد من خلقك فمنك وحدك لا شريك لك ، فلك الحمد ولك الشكر]

أخرجه أبو داود 4/318 ، والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 7وابن السني برقم 41 وابن حبان

[Ee Allaah  sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe chako chochote, na neema ila inatoka kwako hali ya kuwa peke yako huna mshirika wako, ni zako  sifa njema na nizako shukurani.]  

Atakae yasema haya kila asubuhi basi atakuwa ametekeleza  shukurani ya siku nzima, na atakae yasema jioni atakuwa ametekeleza shukurani ya usiku mzima

[Imepokewa na Abuu Daud na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy na Ibnu Hibban.]

 

اللهم عافني في بَدَني، اللهم عافني في سمعي، اللهم عافني في بصري، لا إله إلا أنت .اللهم إني أعوذ بك من الكفر، والفقر، اللهم إني أعوذ بك من عذاب القبر لا إله إلا أنت         ثلاث مرات

أبو داود 4/ 324، وأحمد 5/ 42 والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم   22 وابن السني برقم 69 والبخاري في الأدب المفرد

[Ee Allaah nipe afya ya mwili wangu, Ee Allaah nipe afya ya usikizi wangu, Ee Allaah nipe afya ya uwoni wangu,hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe Ee Allaah hakika mimi najilinda kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.]   mara tatu   [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad na Al-Nnisaai.]

 

[ حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم ]

أخرجه ابن السني 

[Allaah ananitosha, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Yeye, kwake Yeye nimetegemea, na Yeye ni Mola wa Arshi Tukufu.]     [Imepokewa na Ibnu Sunniy]

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ  وَأهْـلي وَمالـي ، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي ، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي ، وَمِن فَوْقـي ، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

أبو داود وابن ماجه وانظر صحيح ابن ماجه 2/332

[Ee Allaah  nakuomba msamaha na afya duniani na akhera.  Ee Allaah  hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika dini yangu na dunia yangu na jamaa zangu, na mali yangu, Ee Allaah nisitiri uchi wangu, na unitulize  khofu yangu, Ee Allaah  nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, najuu yangu, na najilinda kwa utukufu wako kwakutekwa chini yangu.]     [Imepokewa na Abuu Daud.]

 

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيْبِ وَالشّـهادَةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه ، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت ، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ   نَفْسـي  وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه ، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى  نَفْسـي  سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم

 الترمذي وأبو داود .انظر :صحيح الترمذي3/ 142

[Ee Allaah , Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyowazi, muumba wa mbingu na ardhi, Mola wa kila kitu, na Mfalme wake, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki  ila Wewe, najilinda kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na shari ya shetani na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu.]     [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy na Abuu Daud]

 

 بسم الله الذي لا يضرُّ مع اسمه شيء في الأرض ولا في السماء وهو السميع العليم]    ثلاث مرات]

 أخرجه أبو داود 4/ 323 والترمذي 5/ 465 وابن ماجه وأحمد 

 

[Kwa jina la Allaah  ambae hakidhuru kwa jina lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, nae ni Msikivu na ni Mjuzi.]    (mara tatu )     [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy na Ahmad.]

 

رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّـاً وَبِالإسْلامِ ديـناً وَبِمُحَـمَّدٍ  صََلى الله عليه وسلم  نَبِيّـاً ]    ثلاث مرات ]

أحمد 4/ 337 والنسائي في عمل اليوم والليلة برقم 4 وابن السني برقم 68 وأبو داود 4/418 والترمذي 5/465

[Nimeridhika kuwa Allaah ndie Mola wangu, na Uislamu ndio dini yangu, na Muhammad ﷺ  kuwa ni Mtume wangu.]          [Imepokewa na Ahmad na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy.]

 

 

يا حَـيُّ يا قَيّـومُ بِـرَحْمَـتِكِ أَسْتَـغـيث ، أَصْلِـحْ لي شَـأْنـي كُلَّـه ، وَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـين

الحاكم وصححه ووافقه الذهبي 1/ 545 وانظر صحيح الترغيب والترهيب 1/273

 

[Ewe Uliyehai, Uliyesimama kwa dhati yako, kwa rehema zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu  yote, wala usiniachie  mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia) hata kwa muda (mdogo kama muda) wa kupepesa jicho]      [Imepokewa na Haakim na akasahihisha na kuafikiwa na Al-Dhahabiy.]

 

أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم ، فَـتْحَهُ ، وَنَصْـرَهُ ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ ، وَهُـداهُ ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه

 أبو داود 4/ 322 وحسن إسناده شعيب وعبد القادر الأرناؤوط في تحقيق زاد المعاد 2/ 273

 

[Tumeingia asubuhi  na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Allaah, Mola wa viumbe vyote, Ee Allaah   hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii.]      [Imepokewa na Abuu Daud.]

 

Na ikiingia jioni useme:

 

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين ، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة ، فَتْحَهـا ، وَنَصْـرَهـا ، وَنـورَهـا وَبَـرَكَتَـهـا ، وَهُـداهـا ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا 

 

[Tumeingia jioni  na imefika jioni na Ufalme ni wa Allaah, Mola wa viumbe vyote, Ee Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya usiku huu,  ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najilinda kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu.]

 

أَصْـبَحْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام ، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص ، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

 أحمد  3/ 406 و 407 وابن السني في عمل اليوم والليلة برقم 34 وانظر : صحيح الجامع 4/ 209

 

[Tumeingia asubuhi na maumbile ya kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad  ﷺ na mila (dini) ya baba yetu Ibraahiym iliyo sawa hali yakuwa  musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.]       [Imepokewa na Ahmad na Ibnu Sunniy.]

Na ikiingia jioni Aseme:

 

أَمْسَيْنا  علـى فِطْـرَةِ الإسْلام ، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص ، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

 

[Tumeingia jioni na maumbile ya kiislamu na neno la ikhlasi na dini ya Mtume wetu Muhammad ﷺ na mila (dini) ya baba yetu Ibraahiym iliyo sawa hali yakuwa  musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Allaah.]

 

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ]  مائة مرة ]

 رواه مسلم4 / 2071 

[Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema zote nizake.]   mara mia moja      [Imepokewa na  Muslim.]

 

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير]    عشر مرات أو مرة واحدة عند الكسل]

أبو داود 4/319 وابن ماجه وأحمد 4/60

 

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah  peke yake, hana mshirika wake, niwake Ufalme, na nizake sifa njema zote na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah]

 

Amesema Mtume  Mwenye kusema inapoingia asubuhi

 

[ لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير ]

 

[Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah  peke yake hana mshirika wake, niwake Ufalme na nizake  sifa njema zote, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.]

kwa siku mara mia, basi ana thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikwa thawabu mia  moja na atafutiwa madhambi mia moja, na atakuwa na kinga ya shetani kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake.   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

 

 سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنََـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه ]       ثلاث مرات إذا أصبح]

مسلم 4/2090

[Ametakasika Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni zake, kwa hisabu ya viumbe vyake, na radhi yake, na uzito wa arshi yake, na wino wa maneno yake.]  mara tatu kila asubuhi  [Imepokewa na Muslim.]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً وَرِزْقـاً طَيِّـباً ، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً]   إذا أصبح]

 أخرجه ابن السني في عمل اليوم والليلة برقم 54وابن ماجه برقم 925وحسن إسناده عبد القادر وشعيب الأرناؤوط في تحقيق زاد المعاد 2/375

 

[Ee Allaah, nakuomba elimu yenye kunufaisha, na riziki iliyo nzuri, na ibada yenye kukubaliwa]    Kila Asubuhi.      [Imepokewa na Ibnu Sunniy na Ibnu Maajah.]

 أَسْتَغْفِرُ الَّلهَ وَ أَتُوبُ إِلَيْهِ ]   مائة مرة في اليوم]

البخاري مع الفتح 11/ 101 ، ومسلم 4/ 2075

[Namuomba msamaha Mwenyezi Mungu na ninarejea Kwake.]  mara  mia kwa siku    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

Alikuwa Mtume ﷺ akisema asubhuhi  na jioni :

 

[ أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ ]

 

[Najilinda na maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari aliyoiumba.]  mara tatu jioni  

Mwenye  kuisema jioni mara tatu hatodhuriwa na mdudu wa sumu (kama nyoka au kitumbo-ng'e) usiku huo . [Imepokewa na Ahmad na Al-Nnasaai na Ibnu Sunniy]

 

 اللهم صل وسلم على نبينا محمد ]   عشر مرات]

 

[Ewe Mwenyezi Mungu mfikishie rehma na amani Mtume wetu Muhammad ﷺ]

Asema Mtume 

[Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shifaa (msamaha) siku ya Qiyaamah.]        [Imepokewa na Al-Twabraniy.]


SIKILIZA NYIRADI ZA ASUBUHI NA JIONI 



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6497236
TodayToday921
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 5

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_677858d3bd71313216318121735940307
title_677858d3bd85419532084341735940307
title_677858d3bd98e7246525871735940307

NISHATI ZA OFISI

title_677858d3bf9ce19802275041735940307
title_677858d3bfb0712124197401735940307
title_677858d3bfc315594705031735940307 Add content here

HUDUMA MPYA

: 14 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com