KINGA YA MUISLAMU
أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، وأشهد أن محمداً عبده ورسوله] رواه مسلم1/ 209]
[Nakiri kwa moyo na kusema kwaulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu , peke yake, wala hana mshirika wake, na ninakiri kwamba Muhammad ﷺ ni mja wake na ni Mtume wake.] [Imepokewa na Muslim.]
اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين] الترمذي 1/ 78 وانظر صحيح الترمذي1/ 18]
[Ewe Mwenyezi Mungu nijaaliye niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, na nijaalie miongoni mwa wale waliosafi.] [Imepokewa na Al-Tirmidhiy.]
سبحانك اللهم وبحمدك أشهد أن لا إله إلا أنت أستغفرك وأتوب إليك] النسائي في عمل اليوم والليلة ص173]
[Utakatifu ni Wako, Ewe Mola wangu, na shukurani zote zinarudi Kwako, nakiri kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Wewe, naomba msamaha wako, na narejea kwako (kwa kutubia )] [Imepokewa na Al-Nasai.]
SIKILIZA DUA BAADA YA KUTAWADHA
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.