Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitab altawheed


باب (9) ما جاء في الذبح لغير الله


وقول الله تعالى: {قُلْ إِنَّ صَلاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لا شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ} الأنعام:161-162

وقوله: {فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ}     الكوثر:2
عن علي بن أبي طالب رضي الله عنه قال: [حدثني رسول الله صلى الله عليه وسلم بأربع كلمات: لعن الله من ذبح لغير الله. لعن الله من لعن والديه. لعن الله من آوى محدثا ; لعن الله من غير منار الأرض]   رواه مسلم

وعن طارق بن شهاب: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [دخل الجنة رجل في ذباب، ودخل النار رجل في ذباب. قالوا: وكيف ذلك يا رسول الله؟ قال: مر رجلان على قوم لهم صنم لا يجوزه أحد حتى يقرب له شيئا، فقالوا لأحدهما: قرب. قال ليس عندي شيء أقرب قالوا له: قرب ولو ذبابا. فقرب ذبابا، فخلوا سبيله. فدخل النار. وقالوا للآخر: قرب. فقال: ما كنت لأقرب لأحد شيئا دون الله ، فضربوا عنقه؛ فدخل الجنة]    رواه أحمد
:فيه مسائل
{الأولي: تفسير {إِنَّ صَلاتِي وَنُسُكِي
{الثانية: تفسير {فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ
الثالثة: البداءة بلعنة من ذبح لغير الله
الرابعة: لعن من لعن والديه، ومنه أن تلعن والدي الرجل فيلعن والديك
الخامسة: لعن من آوى محدثا، وهو الرجل يحدث شيئا يجب فيه حق الله، فيلتجئ إلى من يجيره من ذلك
السادسة: لعن من غير منار الأرض، وهي المراسيم التي تفرق بين حقك وحق جارك، فتغيرها بتقديم أو تأخير
السابعة: الفرق بين لعن المعين ولعن أهل المعاصي على سبيل العموم
الثامنة: هذه القصة العظيمة، وهي قصة الذباب
التاسعة: كونه دخل النار بسبب ذلك الذباب الذي لم يقصده، بل فعله تخلصا من شرهم
العاشرة: معرفة قدر الشرك في قلوب المؤمنين، كيف صبر ذلك على القتل ولم يوافقهم على طلبتهم، مع كونهم لم يطلبوا إلا العمل الظاهر

الحادية عشرة: أن الذي دخل النار مسلم. لأنه لو كان كافرا لم يقل: "دخل النار في ذباب
[الثانية عشرة: فيه شاهد للحديث الصحيح: [الجنة أقرب إلى أحدكم من شراك نعله، والنار مثل ذلك
الثالثة عشرة: معرفة أن عمل القلب هو المقصود الأعظم، حتى عند عبدة الأوثان


MLANGO WA 09 KUCHINJA KWA AJILI ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU


Ni kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. ]   [Al-An’aam:162-163]

Na kauli Yake:

[Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.]   [Al-Kawthar: 2]

Imepokelewa kutoka kwa Ali bin Abiy Twaalib (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu alinihadithia maneno manne: [Mwenyezi Mungu Amemlaani anayechinja kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Amemlaani anayewalaani wazazi wake, na Mwenyezi Mungu Amelaani anayemuhami mkhalifu, na Mwenyezi Mungu Amelaani anayebadilisha mipaka ya Ardhi]   [Imepokewa na Muslim]

Na kutoka kwa Twaariq bin Shihaab (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: [Mtu mmoja ameingia Pepeni kwa ajili ya Nzi, na Mwengine ameingia motoni kwa ajili ya Nzi]. Wakasema: Ni vipi hivyo ewe Mtume wa Mungu? Akasema: [Watu wawili walipitia mbele ya watu walikuwa na sanamu lao, hapiti mtu hadi mtu atolee mihanga na kafara. Wakamwambia mmoja wao: Litolee kafara! Akasema: Sina kitu cha kutolea kafara. Wakasema: Toa japo kwa nzi. Akapeleka nzi [kwa sanamu lao] Wakamwachia apite njia akaingia Motoni. Wakamwambia mwengine: Litolee kafara! Akasema: Sikuwa natoa chochote kuwa kafara kwa ajili ya yeyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu ﷻ. Wakampiga shingo (wakamuua) akaingia Peponi]    [Imepokewa na Ahmad]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1.Tafsiri ya Aya:

[Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu,].

2. Tafsiri ya Aya:

[Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.]

3. Kuanza laana kwa anayechinja mnyama kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

4. Kumlaani anayewalaani wazazi wake, hii inajumuisha unapowalaani wazazi wa mtu na hivyo yeye kuwalaani wazazi wako.

5. Kumlaani mwenye kumpa hifadhi mkhalifu au mzushi naye ni mtu anaefanya jambo ambalo linsahiki haki ya Mwenyezi Mungu (nao ni Haddi adhabu) kisha akaenda kwa mtu atakae mpa hifadhi juu ya dhambi ile

6. Kumlaani anayebadili mipaka ya ardhi, nayo ni mipaka inayotofautisha baina ya haki yako na haki ya jirani yako, hivyo akaibadilisha kwa kukadimisha au kuakhirisha.

7. Kutofautisha baina ya kumlaani mtu maalumu, na kuwalaani wenye kufanya masia kwa ujumla.

8. Kisa hiki muhimu nacho ni kisha cha nzi.

9. Mtu ameingizwa motoni kwa sababu ya nzi ambaye hakumkusudia kumtoa kafara, bali alifanya hivyo kwa sababu ya kuepuka na shari yao.

10. Kutambua kiwango cha kuchukia shirki katika nyoyo za Waumini, namna alivyo subiri kuuliwa lakini hakuwakubalia ombo lao, pamoja nakuwa walichotaka kwake ni kitendo cha dhahiri.

11. Aliyeingia motoni alikuwa Muislamu, kwani angelikuwa kafiri, (Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ) asingelisema: [Ameingia motoni kwa sababu tu ya nzi.]

12. Inathibitisha Hadith Sahihi:

[Pepo iko karibu ya mmoja wenu kuliko kamba za viatu vyake, na moto (uko karibu) kadhalika]   [ Imepokewa na Bukhaariy na Ahmad ]

13. Kujua kuwa ‘amali za moyo ndio hitajio muhimu hata baina ya waabudu masanamu.


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487351
TodayToday457
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 45

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5e7dd23cc11102007151735286397
title_676e5e7dd24af14330305181735286397
title_676e5e7dd25857164319481735286397

NISHATI ZA OFISI

title_676e5e7dd3aaa7233855621735286397
title_676e5e7dd3b817206691171735286397
title_676e5e7dd3c5a10944032841735286397 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com