Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitab altawheed


باب من تبرك بشجر أو حجر ونحوهما

{وقول الله تعالى: {أَفَرَأَيْتُمُ اللاَّتَ وَالْعُزَّى وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الأُخْرَى

عن أبي واقد الليثي قال: "خرجنا مع رسول الله صلى الله عليه وسلم إلى حنين ونحن حدثاء عهد بكفر، وللمشركين سدرة يعكفون عندها وينوطون بها أسلحتهم يقال لها ذات أنواط. فمررنا بسدرة ; فقلنا: يا رسول الله، اجعل لنا ذات أنواط كما لهم ذات أنواط ; فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: [الله أكبر، إنها السنن. قلتم والذي نفسي بيده كما قالت بنو إسرائيل لموسى: {اجْعَلْ لَنَا إِلَهاً كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ}  لتركبن سنن من كان قبلكم]     رواه الترمذي وصححه
:فيه مسائل
الأولي: تفسير آية النجم
الثانية: معرفة صورة الأمر الذي طلبوا
الثالثة: كونهم لم يفعلوا
الرابعة: كونهم قصدوا التقرب إلى الله بذلك، لظنهم أنه يحبه
الخامسة: أنهم إذا جهلوا هذا فغيرهم أولى بالجهل
السادسة: أن لهم من الحسنات والوعد بالمغفرة ما ليس لغيرهم
السابعة: أن النبي صلى الله عليه وسلم لم يعذرهم الأمر، بل رد عليهم بقوله: [ الله أكبر، إنها السنن. لتتبعن سنن من كان قبلكم ] فغلظ الأمر بهذه الثلاث
{الثامنة: الأمر الكبير، وهو المقصود: أنه أخبر أن طلبهم كطلب بني إسرائيل لما قالوا لموسى: {اجْعَلْ لَنَا إِلَهاً
التاسعة: أن نفى هذا من معنى " لا إله إلا الله " مع دقته وخفائه على أولئك
العاشرة: أنه حلف على الفتيا، وهو لا يحلف إلا لمصلحة
الحادية عشرة: أن الشرك فيه أكبر وأصغر، لأنهم لم يرتدوا بهذا
الثانية عشرة: قولهم: [ ونحن حدثاء عهد بكفر] فيه أن غيرهم لا يجهل ذلك
الثالثة عشرة: التكبير عند التعجب، خلافا لمن كرهه
الرابعة عشرة: سد الذرائع
الخامسة عشرة: النهي عن التشبه بأهل الجاهلية
السادسة عشرة: الغضب عند التعليم
[السابعة عشرة: القاعدة الكلية لقوله: [إنها السنن
الثامنة عشرة: أن هذا علم من أعلام النبوة، لكونه وقع كما أخبر
التاسعة عشرة: أن كل ما ذم الله به اليهود والنصارى في القرآن أنه لنا
العشرون: أنه متقرر عندهم أن العبادات مبناها على الأمر، فصار فيه التنبيه على مسائل القبر. أما "من ربك؟ " فواضح، وأما " من نبيك؟ فمن إخباره بأنباء الغيب. وأما " ما دينك؟ " فمن قولهم: " اجعل لنا " إلى آخره
الحادية والعشرون: أن سنة أهل الكتاب مذمومة كسنة المشركين
"الثانية والعشرون: أن المنتقل من الباطل الذي اعتاده قلبه لا يؤمن أن يكون في قلبه بقية من تلك العادة، لقولهم: "ونحن حدثاء عهد بكفر


MLANGO WA 08 MWENYE KUTABARUKU KWA MTI NA JIWE NA MFANO WA HIVYO


Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

[Je! Mmemuona Lata na Uzza?Na Manaat, mwingine wa tatu?]

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Waaqid Al-Laythiyy (Radhi za Allah ziwe juu yako) amesema: “Tulitoka pamoja na Mtume ﷺ kwenda vita vya Hunayn nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri, na washirikina walikuwa na Mkunazi wanaufanyia ‘Ibada na walikuwa wakitundika silaha zao [kupata Baraka]. Wakiuita ‘Dhaatu Anwaatw’. Tukapita mbele ya mkunazi tukasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu , tufanyie nasi dhaata-anwaatw kama walivyokuwa nao [makafiri] dhaatu-anwaatw”  Mtume  akasema: [Allaahu Akbar! (Mwenyezi Mungu ni mkubwa) Hivi ni kama walivyosema watu wa Musa “Tufanyie nasi muabudiwa kama walivyokuwa nao waabudiwa” Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mtafuata nyendo za walio kabla yenu ]   [Imepokewa na At-Tirmidhiy na ameikiri ni Swahiyh]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1- Tafsiri ya Aya katika Suratu An-Najm.

2- Kujua kiini cha jambo walilolitaka Maswahaba (kuhusu kuweka mti kama wa dhaat anwaatw).

3- Ya kwamba (Maswahaba) hawakutekeleza walichoomba.

4- Yalikuwa makusudio yao (Maswahaba) ni kujikuruibisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuomba huko, wakidhani kuwa (Mwenyezi Mungu Atalipenda hilo.

5- Ikiwa (Maswahaba) hawakujua kosa hilo, wengineo ni wepesi zaidi kutokulijua kosa hilo (na kuingia katika shirki).

6- (Maswahaba) wana malipo mema na walikuwa na ahadi ya kughufuriwa jambo ambalo wengineo hawana.

7- Ni kwa Mtume  hakuwapa udhuru kwa hili, bali aliwakanushia kwa kusema, [Allaahu Akbar! Hivi ni kama… na mtafuata nyendo za walio kabla yenu…] Hivyo alidhihirisha uzito wake kwa mambo hayo matatu.

8- Lililo muhimu katika jambo hili ni fundisho lililokusudiwa kwamba Mtume  alifananisha ombii lao ni kama ombi la wana wa Israail (pindi walipomuomba Musa, “Tufanyie muabudiwa.”)

9- Kukanushwa ombi hilo ni Maana ya laa ilaaha illaa Allaah, Pamoja na kuwa liko wazi, na kufichika hilo kwa (Maswhaba).

10- Kuapa kwa Mtume  juu ya Fatwa, na haapi (Mtume ﷺ ) isipokuwa kwa maslahi.

11- Na kwamba Shirki kuna ndogo na kubwa, kwa sababu Maswahaba hawakuritadi kwa ombi lao hilo.

12- Kauli yao, (Maswahaba) [ndio kwanza tumetoka katika ukafiri] inatujulisha kwamba Maswahaba wengineo hawakuwa wajinga wa hilo.

13- Kufaa Kusema "Allah Akbar" wakati kustaajabu juu ya jambo, kinyume na wanavyodhania wengine (kuwa ni makruuh).

14- Kufunga njia zote zinazopeleka kwenye shirki.

15- Kukatazwa kuwaiga watu wa Jaahiliyyah.

16- Kufaa kukasirika kwa Mwalimu (kwa ajili ya kukosoa jambo ovu).

17- Qaaida yenye kukusanya katika neno lake Mtume  [Hizi ni ada].

18- Na kwamba hili ni alama za Utume, kwa sababu yametokea kama alivyojulisha.

19- Kwamba Kila jambo ambalo Mwenyezi Mungu amewakemea  Mayahudi na Wakristo katika Qur'ani basi ni kemeo kwetu pia.

20- Limepita kwao (Maswahaba) kuwa jambo la Ibaada nilizama linatokamane na Kuamrisha, Ndipo kukawa na ukumbusho kuhusu anapoulizwa kaburini; “Ni nani Mola wako?” Hilo liko wazi. Na kuhusu “Nani Mtume wako?” Hilo linatokana na Wahyi kuhusu khabari za mambo ya ghaibu. Lakini kuhusu “Ni ipi Dini yako?”  basi hilo linahusu ombi lao (Mayahudi kwa Muwsaa), “Tufanyie muabudiwa…” mpaka mwisho.

21- Ada (Desturi) za Ahlul-Kitaab (Mayahdi na Manaswara) zinakanushwa sawa na za washirikina.

22- Ni kwamba Aliyetoka katika batili iliyoizoea katika Moyo wake, huwa hajasalimika kabisa na ada zao. Hii ni kutokana na kauli yao, [Nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri.]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487353
TodayToday459
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 48

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5e7dd23cc11102007151735286397
title_676e5e7dd24af14330305181735286397
title_676e5e7dd25857164319481735286397

NISHATI ZA OFISI

title_676e5e7dd3aaa7233855621735286397
title_676e5e7dd3b817206691171735286397
title_676e5e7dd3c5a10944032841735286397 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 6 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com