KITAAB AT-TAWHIID
باب (10) لا يذبح لله بمكان يذبح فيه لغير الله
وقول الله تعالى: {لا تَقُمْ فِيهِ أَبَداً لَمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَى مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَنْ تَقُومَ فِيهِ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَنْ يَتَطَهَّرُوا وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ} التوبة:108
عن ثابت بن الضحاك رضي الله عنه قال: " نذر رجل أن ينحر إبلا ببوانة، فسأل النبي صلى الله عليه وسلم فقال: هل كان فيها وثن من أوثان الجاهلية يُعبد؟ قالوا: لا. قال: فهل كان فيها عيد من أعيادهم؟ قالوا: لا. فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: أوف بنذرك، فإنه لا وفاء لنذر في معصية الله، ولا فيما لا يملك ابن آدم" رواه أبو داود. وإسناده على شرطهما
:فيه مسائل
{الأولي: تفسير قوله: {لا تَقُمْ فِيهِ أَبَداً
الثانية: أن المعصية قد تؤثر في الأرض، وكذلك الطاعة
الثالثة: رد المسألة المشكلة إلى المسألة البينة، ليزول الإشكال
الرابعة: استفصال المفتي إذا احتاج إلى ذلك
الخامسة: أن تخصيص البقعة بالنذر لا بأس به، إذا خلا من الموانع
السادسة: المنع منه إذا كان فيه وثن من أوثان الجاهلية، ولو بعد زواله
السابعة: المنع منه إذا كان فيه عيد من أعيادهم، ولو بعد زواله
الثامنة: أنه لا يجوز الوفاء بما نذر في تلك البقعة، لأنه نذر معصية
التاسعة: الحذر من مشابهة المشركين في أعيادهم، ولو لم يقصده
العاشرة: لا نذر في معصية
الحادية عشرة: لا نذر لابن آدم فيما لا يملك
MLANGO WA MWENYE KUTABARUKU KWA MTI NA JIWE NA MFANO WA HIVYO
Na kauli Yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Usisimame kwenye msikiti huo kabisa. Msikiti ulio jengwa juu ya msingi wa uchamngu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo watu wanao penda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao jitakasa.] [At-Tawba: 108]
Imepokelewa kutoka kwa Thaabit bin Adhwahaak (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Mtu mmoja aliweka nadhiri kuchinja ngamia katika mahali paitwapo Buwaanah. Mtume ﷺ akauliza: [Je, hapo mahali palikuwa pana sanamu miongoni mwa sanamu ya jahiliya linaloabudiwa?] Wakajibu: “Hapana.” Akauliza: [Je, mahali hapo palikuwa panafanywa sherehe miongoni mwa sherehe zao (Mushrikina?)] Wakajibu: “Hapana.” Akasema Mtume ﷺ: [Timiza nadhiri yako, kwani hakika hakuna kutekeleza nadhiri katika kumuasi Mwenyezi Mungu, au ambazo kutekelezwa kwake kuko nje ya uwezo wa Mwanadamu] [Imepokelewa na Abuu Daawuwd kwa sharti ya kuthibitishwa na Al-Bukhaariy na Muslim]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1. Maelezo ya kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Usisimame kwenye msikiti huo kabisa.].
2. Kwamba kufanya maasia huleta athari (mbaya) duniani na vile vile Utifu (huleta Athari mzuri).
3. Kurejesha suala lenye utata kwa lisilo na utata kwa ajili ya kuondoa utata.
4. Ruhusa kwa Mufti kutaka ufafnuzi anapohitajia .
5. Kwamba kuhusisha sehemu maalumu katika kufanya nadhiri hakuna ubaya, madamu hakuna makatazo sehemu ile.
6. Katazo la kutekeleza nadhiri mahali ambako kulikuwa na masanamu hata kama yameshaondoshwa zamani.
7. Kukatazwa nadhiri mahali ambapo washirikina hupatumia kwa sherehe zao za ushirikina hata kama hawaendelei kupatumia mahali hapo.
8. Hairuhusiwi kutekeleza nadhiri mahali kama hapo kwa sababu hiyo ni nadhiri ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
9. Tahadhari ya kujifananisha na washirikina katika sherehe zao, japo bila ya kukusudia.
10. Hakuna nadhiri katika maasi.
11. Haipasi kwa Mwanadamu kuweka nadhiri kwa kitu asichokimiliki.
Today | 592 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.