Menu

AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)


misingi


فَإِذَا قِيلَ لَكَ: مَا الأُصُولُ الثَّلاثَةُ التِي يَجِبُ عَلَى الإِنْسَانِ مَعْرِفَتُهَا؟

فَقُلْ :مَعْرِفَةُ الْعَبْدِ رَبَّهُ، وَدِينَهُ، وَنَبِيَّهُ مُحَمَّدًا صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّ

الأصْلُ الأوَّلُ: مَعْرِفَةُ الرَّب

فَإِذَا قِيلَ لَكَ :مَنْ رَبُّكَ؟

فَقُلْ: رَبِّيَ اللهُ الَّذِي رَبَّانِي، وَرَبَّى جَمِيعَ الْعَالَمِينَ بِنِعَمِهِ، وَهُوَ مَعْبُودِي لَيْسَ لِي مَعْبُودٌ سِوَاهُ

:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

{الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ}

وَكُلُّ مَنْ سِوَى اللهِ عَالَمٌ، وَأَنَا وَاحِدٌ مِنْ ذَلِكَ الْعَالَمِ

فَإِذَا قِيلَ لَكَ: بِمَ عَرَفْتَ رَبَّكَ؟

فَقُلْ: آيَاتِهِ وَمَخْلُوقَاتِهِ، وَمِنْ آيَاتِهِ: اللَّيْلُ، وَالنَّهَارُ، وَالشَّمْسُ، وَالْقَمَرُ، وَمِنْ مَخْلُوقَاتِهِ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرَضُونَ السَّبْعُ وَمَنْ فِيهِنَّ، وَمَا بَيْنَهُمَا

:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

{وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ}

:وَقَوْلُهُ تَعَالَى

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

وَالرَّبُ هُوَ الْمَعْبُودُ

:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ  الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ


Basi utakapoulizwa: Ni ipi Misingi mitatu ambayo mwana wa Adamu anawajibika kuifahamu?

Basi sema: Ni mja kumjua Mola wake, na Dini yake, na Mtume wake Muhammad .

Msingi Wa Kwanza: Kumjua Mola Mlezi:

Basi utakapoulizwa: “Nani Mola wako?”

Sema: "Mola wangu ni Mwenyezi Mungu Aliyenilea na Aliyewalea walimwengu wote kwa neema zake. Naye ndiye ninayemwabudu, na sina mwengine ninayemwabudu asie kuwa yeye.

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu:

[Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote]  [Suurat al-Faatih'a:2]

Na kila kitu kisichokuwa Mwenyezi Mungu, ni kilichoumbwa nami ni mmojawapo katika kilichoumbwa.

Basi utakapoulizwa: “Umemjua vipi Mola wako?”

Sema: “Kutokana na Alama (ishara) zake na Viumbe vyake. Na miongoni mwa Alama zake ni: Usiku, Mchana, Jua, Mwezi. Na miongoni mwa viumbe vyake ni Mbingu saba na Ardhi saba, na kila kilichokuwemo ndani yake na baina yake”

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.]  [Suuratul Fuss'ilat: 37]

Na kauli yake Aliyetukuka:

[Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote]  [Suurat Al-A'raaf:54]

Na Mola mlezi ndiye Mwenye kuabudiwa

Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka.Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika, na hali nyinyi mnajua.]   [Sura Al-Baqara: 21-22]


SHEREHE YA KITABU USUULU THALATHA



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6668035
TodayToday723
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 12

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68669867761436184925161751554151
title_686698677622d16483867111751554151
title_686698677630d11008458791751554151

NISHATI ZA OFISI

title_68669867778e020131186481751554151
title_68669867779c8539681181751554151
title_6866986777aa45221158701751554151 Add content here

HUDUMA MPYA

: 4 + 11 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com