AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)
قَالَ ابْنُ كَثِيرٍ (رَحِمَهُ اللهُ): الخَالِقُ لِهَذِهِ الأَشْيَاءَ هُوَ الْمُسْتَحِقُّ لِلْعِبَادَةِ. وَأَنْوَاعُ الْعِبَادَةِ الَّتِي أَمَرَ اللهُ بِهَا مِثْلُ: الإِسْلامِ، وَالإِيمَانِ، وَالإِحْسَانِ، وَمِنْهُ: الدُّعَاءُ، وَالْخَوْفُ، وَالرَّجَاءُ، وَالتَّوَكُّلُ، وَالرَّغْبَةُ، وَالرَّهْبَةُ، وَالْخُشُوعُ، وَالْخَشْيَةُ، وَالإِنَابَةُ، وَالاسْتِعَانَةُ، وَالاسْتِعَاذَةُ، وَالاسْتِغَاثَةُ، وَالذَّبْحُ، وَالنَّذْرُ، وَغَيْرُ ذَلَكَ مِنْ أَنْوَاعِ الْعِبَادَةِ الَّتِي أَمَرَ اللهُ بِهَا. كُلُّهَا للهِ تَعَالَى
:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى
{وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا}
فَمَنْ صَرَفَ مِنْهَا شَيْئًا لِغَيْرِ اللهِ؛ فَهُوَ مُشْرِكٌ كَافِرٌ
:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى
{وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ}
[وَفِي الْحَدِيثِ: [الدُّعَاءُ مخ الْعِبَادَة
:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى
{وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ }
:وَدَلِيلُ الْخَوْفِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ}
:وَدَلِيلُ الرَّجَاءِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا}
:وَدَلِيلُ التَّوَكُلِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ}
:وقوله
{وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ}
:وَدَلِيلُ الرَّغْبَةِ، وَالرَّهْبَةِ، وَالْخُشُوعِ، قَوْلُهُ تَعَالَى
{إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ}
:وَدَلِيلُ الْخَشْيَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي}
:وَدَلِيلُ الإِنَابَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ}
:وَدَلِيلُ الاسْتِعَانَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ}
[وَفِي الْحَدِيثِ: [...وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللهِ
:وَدَلِيلُ الاسْتِعَاذَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ}
:وَدَلِيلُ الاسْتِغَاثَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ}
:وَدَلِيلُ الذَّبْحِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ}
[وَمِنَ السُنَّةِ: [لعَنَ اللهُ مَنْ ذَبَحَ لِغَيْرِ اللهِ
:وَدَلِيلُ النَّذْرِ قَوْلُهُ تَعَالَى
{يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا }
Asema Ibn Kathiyr (Mungu amrahamu): "Muumbaji wa vitu hivi Ndiye Anayestahiki kuabudiwa." Na aina za Ibada ambazo Mwenyezi Mungu Ameziamrisha ni mfano: Uislamu, na Imani, na Ihsani. Miongoni mwazo ni: Du’a, Kuogopa (kuogopa mtu au adhabu au kitu), Ar-Rajaa (kutarajai), Kumtegemea Mwenyezi Mungu, Ar-Raghbah (Matumaini ya jambo la kupendwa), Ar-Rahbah (tisho au kuogopa), Al-Khushuu’ (unyenyekevu), Al-Khashyah (khofu kutokana na utukufu wa Mwenyezi Mungu nayo inahusiana na elimu), At-Taqwa (uchaji Mungu), Al-Inaabah (kurejea kutubu na utiifu), Al-Isti’aanah (kuomba msaada wa mambo ya kidunia au ya Aakhirah), Al-Isti’aadhah (kuomba kinga), Al-Istighaathah (kuomba msaada, kutaka kuokolewa), Kuchinja, Kuweka nadhiri, na mengineyo ya aina za Ibadah ambazo Mwenyezi Mungu Ameziamrisha. Zote ziwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu] [Surat Al-Jinn:18]
Basi atakayeelekeza chochote katika hizo (Ibada) kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi yeye ni mshirikina, kafiri.
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu :
[Na anaye muomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi] [Surat Al-Muuminun:117]
Na katika Hadithi: [Du’a ni ubongo wa ‘Ibada] [Impokewa na At-Tirmidhiy] (1)
Na dalili ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.] [Suuratul Ghaafir:60]
Na dalili ya Kuogopa ni neno lake Mwenyezi Mungu:
[Basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.] [Suurat Al 'Imran:175]
Na dalili ya Ar-Rajaa (kutaraji) ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.] [Sura Al Kahf:110]
Na dalili ya kumtegemea Mwenyezi Mungu ni neno lake Mwenyezi Mungu:
[Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.] [Suurat Al-Maida:23]
Na kauli yake Aliyetukuka:
[Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha.] [Suuratul Att'alaaq:3]
Na dalili ya Ar-Raghbah (shauku, ya jambo la kupendwa) na Ar-Rahbah (tisho au kuogopa) na Unyenyekevu ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukuf:
[Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na wakituomba hali yakuwa na tamaa ya pepo na kuwa na khofu na Moto na walikuwa kwetu ni wanyenyekevu] [Suuratul Anbiyaa:90]
Na dalili ya Al-Khashyah (khofu kutokana na utukufu wa Mwenyezi Mungu), ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi] [Sura Al-Baqara:150]
Na dalili ya Al-Inaabah (kurejea kwa Mwenyezi Mungu) ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake] [Azzumar:54]
Na dalili ya kuomba msaada ni kauli yake Mwenyezi Mungu :
[Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada.] [Suurat Al-Faatih'a:5]
Na katika Hadithi: [Ukitaka kuomba msaada, basi mwombe Mwenyezi Mungu] [Imepokewa na At-Tirmidhiy]
Na dalili ya Al-Isti’aadhah (kuomba kinga) ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko] [Surat Al-Falaq] na [Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu] [Surat AnNas:1]
Na dalili ya Kuomba msaada, wa kutaka kuokolewa), ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Na (kumbukeni) Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi,(ili awaokoweni) naye akakujibuni] [Al Anfaal:9]
Na dalili ya Kuchinja (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.] [Suurat An'aam:162-163]
Na katika Sunna (Asema Mtume) : [Mwenyezi Mungu Amemlaani aliyechinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu ] [Imepokewa na Muslim]
Na dalili ya Nadhiri ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[Wanatimiza Nadhiri,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,] [Suuratul Al Insan:7]
(1) [Hadith kwa temko hili ni dhaifu. Lakini ipo Hadithi kama hiyo ambayo ni sahihi isemayo [Du’a ni ‘Ibadah] Taz. Swahiyh Al-Jaami’ Asw-Swaghiyr (3407)]
Today | 166 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.