AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)
اعْلَمْ أَرْشَدَكَ اللهُ لِطَاعَتِهِ، أَنَّ الْحَنِيفِيَّةَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ: أَنْ تَعْبُدَ اللهَ وَحْدَهُ، مُخْلِصًا لَهُ الدِّينَ. وَبِذَلِكَ أَمَرَ اللهُ جَمِيعَ النَّاسِ، وَخَلَقَهُمْ لَهَا
:كَمَا قَالَ تَعَالَى
{وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ }
وَمَعْنَى ((يَعْبُدُونِ)) :يُوَحِّدُونِ، وَأَعْظَمُ مَا أَمَرَ اللهُ بِهِ التَّوْحيِدُ، وَهُوَ :إِفْرَادُ اللهِ بِالْعِبَادَةِ. وَأَعْظَمُ مَا نَهَى عَنْه الشِّركُ، وَهُوَ: دَعْوَةُ غَيْرِهِ مَعَهُ
:وَالدَّلِيلُ قَوْلُهُ تَعَالَى
{وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا}
فَإِذَا قِيلَ لَكَ: مَا الأُصُولُ الثَّلاثَةُ التِي يَجِبُ عَلَى الإِنْسَانِ مَعْرِفَتُهَا؟
فَقُلْ :مَعْرِفَةُ الْعَبْدِ رَبَّهُ، وَدِينَهُ، وَنَبِيَّهُ مُحَمَّدًا صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ
Fahamu, Mwenyezi Mungu Akuongoze katika utiifu wake, kwamba al-Hanifiyyah (kuelemea Dini ya haki na kujiepusha na dini potofu) ni Dini ya Ibrahim. Nikumuabudu Mwenyezi Mungu Peke yake hali yakumtakasia Dini, na kwa hilo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha watu wote, na Amewaumba kwa sababu hiyo.
Kama Anavyosema Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.] [Surat Adh-dhaariyaat:56]
Na maana ya (waniabudu) ni: Wanipwekeshe. Na jambo kuu kabisa Aloamrisha Mwenyezi Mungu ni At-Tawhid ambayo ni: Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada.
Na jambo kuu kabisa Alokataza ni Shirki, ambayo ni: Kumuomba mwengine pamoja Naye.
Na dalili ni kauli Yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote] [Surat An-Nisaai:36]
Basi utakapoulizwa: Ni ipi Misingi mitatu ambayo mwana wa Adamu anawajibika kuifahamu?
Basi sema: Ni mja kumjua Mola wake, na Dini yake, na Mtume wake Muhammad ﷺ.
SHEREHE YA KITABU USUULU THALATHA
Today | 504 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.