Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


sera


Amri ya Kwanza ya Kudhihirisha Da'wa Jambo la mwanzo ambalo lilishuka kuhusiana na suala hili ni kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ Aliye Mtukufu: 

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ}  الشعراء:214}

 

[Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.]   [26:214]. 

Hii ni aya kutoka katika Suratu Sshuaraa, ambamo ndani yake kimetajwa kisa cha Mussa (a.s.) tokea mwanzo wa Utume wake mpaka kuhama kwake pamoja na wana wa Israili, na kusalimika kwao kutoka katika makucha ya Firauni na watu wake, na kugharikishwa Firauni na watu wake. Kisa hiki kimekusanya hatua zote alizozipitia Musa (a.s.) wakati wa kumlingania Firauni na watu wake kumwelekea Mwenyezi Mungu ﷻ . 

Ninaona kuwa kisa cha Nabii Musa kilielezwa wakati Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ Alipoamrishwa kuwalingania . watu wake kumuelekea Mwenyezi Mungu ﷻ, ili uwe mbele yake na masahaba wake mfano wa yale ambayo watakutana nayo, katika mambo ya kukadhibishwa na kukandamizwa wakati watakapoudhihirisha ulingano, na imani yao tokea mwanzo wa Da'wa yao. 

Kwa upande mwingine sura hii imekusanya pia maelezo ya kutajwa kwa mwisho mbaya wa watu wanaowakadhibisha Mitume, watu wa Nuhu, Aad, baadhi ya Thamud, watu wa
Ibrahim, watu wa Lut na Ashabul-Aykah (watu wa Mtume Shuaib); zaidi ya yale ambayo yametajwa katika mambo ya Firauni na watu wake. Kusudio ilikuwa ni kuwajuza wale ambao wangesimama na kukadhibisha ukweli walioletewa kuwa watapata adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu ﷻ iwapo wataendelea na kukanusha ukweli ulio wazi mbele yao. Waumini wajue ya kuwa mwisho mwema ni wao na wala si wa wale wanaokadhibisha. 


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

8355461
TodayToday577
Highest 09-30-2026 : 21356
US
Guests 60

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6ac8e6fa1b5f55198842901791551226
title_6ac8e6fa1b64712093315421791551226
title_6ac8e6fa1b6944136681091791551226

NISHATI ZA OFISI

title_6ac8e6fa1bc6720736625411791551226
title_6ac8e6fa1bcb4641226431791551226
title_6ac8e6fa1bd011930812051791551226 Add content here

HUDUMA MPYA

: 12 + 4 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

Go to top
UongofuUongofu.com