AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Jambo la kwanza alilolifanya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ baada ya kushuka kwa aya hii, ni kuwaita Banu Hashim. Walihudhuria kundi kutoka katika ukoo wa Banu Al- Muttwalib bin Abdi Manafi, kwa jumla walikuwa kiasi cha watu arubaini na watano. Kabla ya kusema alichowaitia Abu Twalib alimuwahi na kusemai.Hawa ndiyo ammi zako na watoto wa ammi yako, kwa hiyo zungumza na acha upuuzi na fahamu kuwa jamaa zako Waarabu wote hawana uwezo na mimi nina haki zaidi ya aliyekuchukua, kwa hiyo wewe wanakutosha watoto wa batfa yako. Iwapo utaamua kuendelea na khabari zako, hilo ni jepesi sana kwao kuliko kukushambulia watu wote wa kabila la Quraishi, na wakasaidiwa na Waarabu wengine. Hajawahi mtu yeyote kuja kwa watoto wa baba yake na shari kuliko hii ambayo umekuja nayo wewe.' Akanyamaza, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷻ hakusema katika baraza hilo.
Aliwaita mara ya pili na akasema, kusema:
الحمد الله، أحمده وأستعينه، وأومن به، وأتوكل عليه. وأشهد أن لا إله إلا االله وحده
لا شريك له. ثم قال: إن الرائد لا يكذب أهله، واالله الذي لا إله إلا هو، إنى رسول االله إليكم خاصة
وإلى الناس عامة، واالله لتموتنكما تنامون، ولتبعثنكما تستيقظون، ولتحاسبن بما تعملون، وإنها الجنة أبدا
أو النارأبدا
[Sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu ﷻ, ninamsifu, ninamuamini, ninategemea kwake na ninakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu ﷻ na hana mshirika. Kisha akasema: Kwa hakika kiongozi (Raid) hawezi kuwadanganya watu wake, ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ ambaye hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Kwa hakika mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu, hali ya kuhusishwa na nyinyi na kwa watu wote, ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu mtakufa kama mnavyo lala na mtafufuliwa kama mnavyoamka. Mtahesabiwa kwa yale ambayo mnayatenda. Hakika mambo yalivyo,ni ama kuingizwa peponi milele au motoni milele]
Abu Twalib akasema; 'Tungependa kukusaidia, tunakubali ushauri wako, na kusadikisha kauli yako. Hapa wapo watoto wa baba yako wamekusanyika, mimi ni mmoja wao, isipokuwa mimi ni mwepesi kuliko wao katika kutenda lile ambalo unalipenda. Endelea kufanya lile ambalo umeamrishwa kwalo. Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu sitaacha kuwa ni mwenye kukulinda na kukusaidia, lakini sitoiacha dini ya Abdul Muttwalib.' Abu Lahab akamwambia Abu Twalib, "Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu huu ndiyo ubaya wenyewe, ikamateni mikono yake kabla hawajaishika watu wengine." Abu Twalib akaingilia na kusema: "Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu ﷻ, kuwa tutamlinda maadamu tuko hai. (1)
1) Ibn Al-Athir, Fiqhi Sira, Uk. 77-78.
* Arraheeq Al Makhtum 125-127
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.