AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Baada ya uchunguzi inaonekana kuwa japokuwa mpaka wakati huo Da'awa ilikuwa bado ni ya siri, Makuraishi walikuwa wamekwisha kusikia khabari za Mtume ﷺ na mafundisho yake, lakini wao walizipuuza khabari hizo.
Muharnmad Al-Ghazali amesema, "Khabari hizi zilienea kwa Makuraishi, lakini wao hawakuzipa umuhimu wowote, na huenda walimdhani kuwa Muhammad ﷺ ni mmoja wa hao watu ambao wanajihusisha na masuala ya dini, wanaozungumzia mambo ya Uungu na haki zake, kama alivyofanya Umayya bin Abi As-Salti na Quss bin Sa'idah, , Amru bin Nufail, na wengineo. Makuraishi walizinduka baada ya kipindi fulani kupita, walianza kupata khofu kwa jinsi ujumbe wake ulivyoenea kwa kasi na jinsi watu walivyokuwa wakiupokea na kuenea kwa athari yake, wakaanza kufuatilia safari zake na Da'wa yake kwa makini zaidi." (1)
Wito wa siri uliendelea kwa muda wa miaka mitatu, na katika kipindi hiki, liliibuka kundi la Waislamu ambalo lilisisitiza udugu na ushirikiano, kuueneza ujumbe na kumtia hima Mtume ﷺ katika msimarno wake. Baada ya hapo ndio sasa ukashuka Wahyi uliomtaka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ kuwatangazia Dini watu wake kwa kuwabainishia haki na batili pamoja na kuyahujumu rnasanarnu yao. *
1) Fiqlti Sira, Uk. 76.
* Ar Raheeq Al Makhtuum 123
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.