Menu

MTU ATAFANYA NINI ATAKAPO KOSA MAWE YA KUJISAFISHIA?


 

 

Swali:Tumekataza kutumia mfupa au choo cha hayawani katika kujisafishia. Je mtu atakapo kosa Maji na kukosa mawe atafanya nini?


Jibu: Mtu atakapo kosa maji au mawe ya kujisafishia basi atatumia kile atakacho pata kama ni mfupa au hata kama ni choo cha myama. Kwa sababu baadhi ya Wanachuoni wanasema katazo la kutumia mfupa au choo si katazo la kuharamishwa bali ni katazo la karaha. Yaani ni makruhi mtu kutumia mfupa au choo lakini atakapo kosa cha kusafishia na kukawa hakuna kitu kingine basi atafaa kutumia ili kujisafishia ili apata kuswali na asipo pata kitu chochote basi afaa kutumia mkono wake kujisafishia kisha ausafishe mkono wake kwa mchanga kisha atayamamu na aswali kisha atakapo pata maji atajisafisha vizuri kwa neno lake Mtume (S.A.W).


الصعيد الطيب وضوء المسلم، وإن لم يجد الماء عشر سنين، وإذا وجد الماء فليمسه بشرته.] الحديث رواه أحمد في المسند]

[Mchanga msafi ni udhuu wa Muislamu hata asipo pata Maji miaka kumi,na atakapo pata Maji basi ayagusishe Ngozi yake]  yaani awe ni mwenye kutumia maji kwa kujisafisha.
Hadihi imepokewa na Imam Ahmad katika Musnad yake.


Na Allah ndie Mjuzi zaidi.

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785493
TodayToday494
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 27

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a98c24b0cf42966647381755941924
title_68a98c24b0de01300998931755941924
title_68a98c24b0ec4228282541755941924

NISHATI ZA OFISI

title_68a98c24b24f94856172211755941924
title_68a98c24b25ec20744091491755941924
title_68a98c24b26b89955552381755941924 Add content here

HUDUMA MPYA

: 4 + 3 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com