Menu

 HUKMU YA KUTUMIA MAJI YALIO TUMIWA


 

Swali: Je yafaa mtu kutumia maji yalio tumiwa kujitwayarisha kukamilishia Udhu wake. Mfano; mtu akayakusanya maji ya kutawadhia kwenye chombo kisha maji

yale akayatumia katika kuoshea miguu je yafaa kufanya hivyo?

Jibu: kutumia maji yaliotumika katika twahara ni katika Mas'ala wanchuoni walio ikhtilalifiana  sawa au si sawa katika kuyatumia maji yale kukamilisha Udhu au kutawadhia upya.

Madh'habu ya Imamu Malik anaona yafaa kutumia kwa sababu maji yale ni twahara na waweza kutwahirishia ikiwa maji yale hayakubadilika lakini ni Makruhu kutumia.

Na msimamo huu ndio msimamo wa Sheikhul islam Ibn Taimiyah. Asema kwa sababu maji yalio tumika katika kuondoshea hadathi yamebaki katika utwahara wake,na imesihi

kutoka kwa Mtume ﷺ Akisema:

إن الماء طهور لا يُنجِّسُه شيء]   رواه أبو داود ، والترمذي]

 

[Hakika ya Maji ni Twahara hayanajisiki kwa kitu chochote]     [Imepokewa na Abuu

Dawud na Attirmidhiy] 

Maji hayawezi kuwa na janaba,wala hayawezi kuchukuwa hukmu ya janaba.

Lakini msimamo wa wengi katika wanachuoni wanaona maji yalio tumiwa hayafai kuyatumia katika kuondoshea hadathi. sawa iwe ni hadathi ndogo kama kutawadhia, au Hadathi kubwa, kama kuoga janaba na msimamo huu ndio msimamo wa wengi na ni katika kujiondoa kwenye shaka na khilafu.

Kwa hivyo itakuwa ni bora kutumia maji ambao hajatumiwa katika kuondoshea hadathi sawa kukamilishia Udhu au kutawadhia.

Na allah ndie Mjuzi zaidi.


 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785498
TodayToday499
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 30

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a98c24b0cf42966647381755941924
title_68a98c24b0de01300998931755941924
title_68a98c24b0ec4228282541755941924

NISHATI ZA OFISI

title_68a98c24b24f94856172211755941924
title_68a98c24b25ec20744091491755941924
title_68a98c24b26b89955552381755941924 Add content here

HUDUMA MPYA

: 15 + 7 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com