Menu

 

HUKMU YA KUTAWADHA NA MAJI YALIO INGIA MENDE

 

Swali : Mende/Kombamwiko akiingia kwenye maji kidogo ambao hajafikia Qullatayn maji yale hunajisika?

Jibu:  kuingia wadudu ambao hawana damu kama vile mende,inzi na wengineo kwenye maji au yasio kuwa maji basi hayanajiski. Hata maji yakawa ni kidogo,hata kama atafia ndani na huu ndio Msimamo wa Jamhuri ya wanchuoni. Maji yale yatakuwa yafaa kutumia katika ibada kama kujitwahirishia au ada kama kunywa na

kupikia,kwa Hadihti iliopokelewa na imamu Bukhari:

عنأبي هريرة ـرضي الله عنه ـ أن النبي صلى الله عليه و سلم قال:إذا وقع الذباب في شراب أحدكم فليغمسه كله ثم ليطرحه، فإن في أحد

جناحيه داءً، وفي الآخر دواءً.

Kutoka kwa Abuu Hurayra radhi za Mungu zimfikie yeye,kwamba Mtume rehma na amani zimfikie yeye, asema:

[inzi anapo ingia katika kinywaji cha mmoja wenu basi naamzamishe yeye mzima kisha amtoe,kwa sababu kwenye ubawa wake mmoja uko na ungonjwa,na mwengine uko na dawa].

Asema Ibnul Qayyim katika kitabu chake 'Al-Zzaad' hadithi hii ni dalili ilo wazi kwamba inzi anapo kufa kenye maji au vitu vya majimaji,havinajisiki,na hii ndio kauli ya jamhuri ya wanachuoni. Wala hajulikani katika Salaf (watu wema walio tangulia) mwenye kukhalifu hilo. Kisha hukmu yake ikaenea kwa wadudu wote wasio kuwa na damu ya kutirizika kama vile,nyuki, na Zanbur (wasp) na Ankabut (spider) na mfano wa hao.

Na baadhi ya wanchuoni wamemtoa Mende wa choni na kila mdudu alitokamana na najisi, wakasema kila mdudu alitoka kwenye kitu twahara huwa ni twahara. Mdudu alitoka kwenye najisi huwa ni najisi.

Kiufupi ni kuwa wadudu wasio kuwa na damu wanapo ingia kwenye maji au kitu chochote, kitu kile au maji yale huwa ni twahara wala si najisi.

Wallahu aalam.

 

LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487591
TodayToday697
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 64

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e65945cc0713057797111735288212
title_676e65945ccf42268906231735288212
title_676e65945cdd718434597751735288212

NISHATI ZA OFISI

title_676e65946961416616047581735288212
title_676e6594697c35673028041735288212
title_676e6594699e65775449061735288212 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com