HUKMU YA KUINGIA CHOONI NA KASETI ZA QUR'ANI
SWALI :YAFAA MTU KUINGIA CHOONI NA KASETI YA QUR'ANI AU NA SIMU ILOHIFADHI QUR'ANI ?
JIBU: KWANZA KABISA NI MAKRUHI MTU KUINGIA CHOONI NA KITU CHOCHOTE KILICHOANDIKWA JINA LA MWENYEZI MUNGU AU KITU KILICHOANDIKWA CHOCHOTE KUHUSU QUR'ANI,
NA MADHHABU YA JAMHURI YA WANACHUONI KATIKA MADHABU YA HANAFIA NA MALIKIA NA SHAFIA KUWA NI MAKURUHU MTU KUINGIA CHOONI NI DIRHAMU ILIANDIKWA JINA LA MWENYEZIMUNGU NA HAIKUSITIRIWA, LAKINI IKIWA IMESIRITIRIWA BASI HUNDOKA UKARAHA WAKE,NA HUU VILE VILE NI MSIMAMO WA IMAM AHAMD KATIKA MOJA YARIWAYA ZAKE,
AMA KUINGIA NA KASETI ZA QUR'ANI AU SIMU ILIOHIFADHI WA NDANI YAKE QUR'ANI NA IKAWA HAIKU NJEYA SCREEN BASI ITAKUWA YAFAA KWA SABABU HAINGII KATIKA KATAZO WALILIOILEZEA WANACHUONI KUWA NI MAKRUHU KUNGIA CHOONI NA KITU CHOCHOTE KILICHOANDIKWA JINA LA MENYEZIMUNGU KWA KUTOPATOKANA HERUFI ZILIZO WAZI NDANI YAKE
Na Allah ndie mjuzi zaidi
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.