HUKMU YA KUSWALI IJUMAA KWA MSAFIRI
Suali: Ni ipi hukmu ya kuswali Swala ya Ijumaa kwa Msafiri?
Jawabu: Kwanza kabisa msafiri haimpasi kuswali Ijumaa, imekuja katika kitabu cha Imamu Al Nnawawiy "Al Majmuu" Haimpasi kuswali Ijumaa kwa msafiri"
Lakini ikiwa msafiri ataamua kuswali Ijumaa pamoja na watu basi itamtosheleza na hatoswali Adhuhuri, Asema Sheikh Ibnu Baaz katika Fatawa za Nuur ala Al Darbi : "Na lau msafiri ataswali Ijumaa na watu itamtosheleza na kutoswali Adhuhuri, kwa sababu msafiri halazimiki kuswali Ijumaa, lau ataingia kwenye mji na yeye ni msafiri akaswali na wao Ijumaa itamtosheleza na kutoswali Adhuhuri".
Ama kuswali Ijumaa peke yake au kuchanganya swala ya Ijumaa pamoja na Alasiri hilo halifai wala halitamtosheleza, lakini la uwajibu kwake ni kuswali Adhuhuri hali ya kuipunguza na hakuna ubaya ikiwa itakusanya pamoja na Alasiri kwa kupunguza.
Na Allah ndie Mjuzi zaidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.