RUHUSA YA KUKUSANYA SWALA KWA MGONJWA
Suala; Je mgonjwa alie lala kitandani anaruhusiwa kukusanya Swala na kupunguza?
Jawabu: Mtu akishikwa na ugonjwa na akawa hawezi kusimama kuswali, basi Sheria imemruhusu kuswali kwa kukaa, na ikiwa hawezi kukaa basi aswali kwa ubavu na akishindwa kuswali kwa ubavu basi anaswali kwa kuashiria rukuu na kusujudu na hii ni kwa hadithi ya Imraan bin Huswein asema nilikuwa na bawasili, nikamuliza Mtume ﷺ Kuhusu Swala akasema:
صل قائماً، فإن لم تستطع فقاعداً، فإن لم تستطع فعلى جنب] رواه الجماعة إلا مسلما]
[Swali kwa kusimama ikiwa hutoweza basi swali kwa kukaa na ikiwa hutoweza swali kwa ubavu] [Imepokewa na Jamaa ila Muslim]
Na amejuzisha Imam Ahmad kukusanya swala, sawa kwa kutanguliza au kuakhirisha kwa udhuru wa ugonjwa, kwa sababu ugonjwa uko na shida zaidi kuliko shida ya Mvua.
Na Amesema Imam Annawawiy "ni Huja ya nguvu," yaani Hoja ya Imamu Ahmad
Na imekuja katika kitabu cha Al-Mughniy cha Ibnu Qudaama "Na ugonjwa unao ruhusiwa kukusanya ni ule unao mpatia mtu shida na udhaifu ikwa ataswali kila swala kwa wakati wake"
Na kauli hii ndio inayo kwenda sambamba na sheria yetu kwa sababu shida huleta wepesi.
Ama kupunguza swala kwa kuswali adhuhuri na alasiri na Ishaa rakaa mbili hili halifai kwa sababu lingekuwa lafaa mtume angemruhusu huyu Swahaba Imraan Bin Huswein alipo muuliza pamoja na kuwa Mtume alimruhusu kuacha baadhi ya nguzo kama kusimama kwa ajili ya kumsahilishia na hili lakupunguza kama lafaa basi Mtume ﷺ ange mruhusu.
Na Allah ndie Mjuzi zaidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.