KUACHA SWALA YA IJUMAA BILA YA DHARURA
Suali: Ni ipi hukmu ya mtu kuacha swala ya ijumaa bila yakuwa na dharura?
Jawabu: Swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima kwa kila Muislaam isipokuwa kwa wale waliokuwa na nyudhuru za kisheria. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ} الجمعة:9}
[Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.] [al Jumua:9]
Na amepokea Twaarik bin shihaab asema Mtume ﷺ:
الجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلاَّ أَربَعَة : عَبدٌ مَملُوكٌ ، أَو امرَأَةٌ ، أَو صَبِيٌّ ، أَو مَرِيضٌ] رواه أبوداود]
[Ijumaa ni haki na ni wajibu kwa kila Muislamu iswaliwe kwa jamaa isipokua watu wa nne: mtumwa na Mwanamke na vilevile kijana mdogo na mgonjwa'] [Imepokewa na Abuu Daud].
Amesema Imamu Al Nnawawiy "amenakili ibnul mundhir kwenye vitabu vyake viwili :kitabul'ijmaai na kitabul ishraaf- ijamai ya waislamu kuhusu uwajibu wa ijumaa."
Na amesema mwanachuoni ibnu Qaasim katika hashiya yake na amesema al-Muwafaq: "Waislamu wote wameafikiana kua swala ya ijumaa ni faradhi ".
Na amesema ibnul Arabiy yakuwa "Swala ya ijumaa ni faradhi kwa kuafikiana waislamu wote, Amesema Mwenyezi Mungu.
"Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na ametoa amri kwa hiyo na onyo dhidi ya yule anae acha ,na anakufuru anae pinga ufaradhi wake ,kwa kuthubutu ufaradhi wake kwa dalili zisokua na shaka."
Na maneno ya Wanavuoni kuhusu hili ni mengi sana.
Ndio utajua kua wanavyo fanya baadhi ya watu kuacha swala ya ijumaa kimakusudi na waka swali adhuhuri (badali yake) ni jambo lisilofaa; haswa Ikiwa masharti ya kusihi swala ya ijumaa yamekamilika, na wasiwe wana udhru wa kisheria kutoswali, bali hili jambo la kuacha kuswali ijumaa pasina udhru wowote kumekuja makemeo na onyo kali kabisa kutoka kwa Mtume ﷺ, Amepokea Abdillahi bin Mas'ud radhi za Allah ziwe juu yake Mtume amesema kuwaambiya watu wasioswali ijumaa:
لقد هممت أن آمر رجلا يصلي بالناس ثم أحرق على رجال يتخلفون عن الجمعة بيوتهم] رواه أحمد ومسلم]
[Nimefanya hamu ni muamrishe mtu aswalishe watu kisha niende nikachome nyumba za wale wasio hudhuria ijumaa.] [Imepokewa na Imamu ahmad na Imaam Muslim.]
Na amepokea Abu Hureira na ibnu Umar radhi za Allah ziwe juu yao yakua wamemsikiya Mtume
akisema akiwa yuko ju ya minmbari yake:
لينتهين أقوام عن ودعهم الجمعات، أو ليختمن الله على قلوبهم، ثم ليكونن من الغافلين] رواه مسلم]
[Hawataendelea watu kuacha swala ya Ijumaa, mpaka Mwenyezi Mungu apige muhuri nyoyo zao, kisha watakuwa niwenye kuishi katika mughafala] [Imepokewa na Muslim.]
Na imepokewa na Abuu Ja'ad Al Dhumiriy -na huyu ni swahaba- asema kwamba Mtume ﷺ Amesema:
من ترك ثلاث جمع تهاونا بها طبع الله على قلبه] رواه الخمسة وأحمد وإبن ماجة]
[Yeyote atakae acha majuma mataatu kwa dharau tu basi Mwenyezi Mungu atampiga muhuri juu ya moyo wake] [Imepokewa na watano na ame pokea Ahmad na Ibnu majah]
Kwa hivyo niwajibu kuwapa nasaha kwa wote wale wanaoacha kuswali swala ya ijumaa bila ya dharura na wakumbushwe maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na maneno ya wanachuoni katika kukemea jambo hili. Huenda Mwenyezi Mungu akawaongoza na wakatubia na kuacha jambo hili la kuacha kuswali swal ya ijumaa.
Na Mwenyezi Mungu ndie Mjuzi zaidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.