HUKMU YA MTOTO KUSALISHA SWALA YA FARADHI
Swali: Yafaa kwa mtoto ambae hajabaleghe kusalisha watu Swala ya faradhi?
Jawabu: Kwanza kabisa wanazuoni wameafikiana kujuzu kuswalisha mtoto ambae hajabaligi Swala ya Sunna.
ama kuswalisha Swala ya Fardhi wanazuoni wa fiqhi wamekhtalifiana kuhusu kuswalisha kwa mtoto ambae hajabalighi, imekuja katika [Al Mausuuatul Fiqhiyyah] ukurasa wa 203 na 204 juzuu ya 6 yakwamba wanazuoni wengi wa fiqhi madhehebu ya (hanafi,maaliki,hanaabila) yakwamba ni sharti Umamu wa Swala ya faradhi uwe sahihi ni lazima imamu awe ni Baaligh, hivyo basi haisihi uimamu wa mtoto anaepambanua kulingana na madhehabu yao, kwa sababu uimamu ni hali ya ukamalifu na mtoto sio katika watu waliokamilika,na yakwamba imamu ni mwenye dhamana na asie balighi sio katika watu wenye dhamana,na kwa sababu yeye haaminiki na kukosea katika kusoma Qur'ani wakati wa siri"
Na madhehebu ya Imam Shafi'i hawajashurutisha kwamba Imamu lazima awe amebalighi Hivyo basi kwao inaswihi Uimamu wa Mtoto anaepambanua kwa aliebalighi, sawa iwe ni Swala ya faradhi au Swala ya sunna kwa hadithi ya Amru bin salamah yakwamba yeye alikua akiwaswalisha watu wake wakati wa Mtume ﷺ na alikua na umri wa miaka sita au saba, lakini wamesea yakuwa aliebalighi ni bora kuliko mtoto, hata kama mtoto anajua kusoma na ni mwenye elimu zaidi kwa kusihi Uimamu aliebaleghe kwa ijmai ya wanazuoni.
na baadhi ya wanchuini wa madhebu ya Imamu Shafi wamesema kuwa ni Makruhu kuswalisha mtoto ambae hajabaleghe Swala ya faradhi.
Na hii ndio kauli sahihi yakwamba yafaa mtoto anaepambanua kuswalisha ikiwa anajua kuswali vizuri ingawaje aliebalighi ni bora zaidi, ikiwa anajua kusoma Qur'aan na hilo ni kwa hadithi iliyoko katika Bukhary (4302) na Abuu Daud (585) na Al Nasaaiy (767) yakwamba Amru bin salamah r.a anasema
لَمَّا رَجَعَ قَوْمِي مِنْ عِنْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالُوا إِنَّهُ قَالَ : لِيَؤُمَّكُمْ أَكْثَرُكُمْ قِرَاءَةً لِلْقُرْآنِ . قَالَ : فَدَعَوْنِي فَعَلَّمُونِي الرُّكُوعَ وَالسُّجُودَ ، فَكُنْتُ أُصَلِّي بِهِمْ
[Walivyorudi watu wangu kutoka kwa Mtume ﷺ walisema mtume amesema awaswalishe nyinyi mwenye kujua zaidi kusoma Qur'anI anasema watu wangu wakaniita na kunifundisha kurukuu na kusujudu basi nikawa nawaswalisha.]
Anasema ibnu hajar Mwenyezi Mungu amrehemu "katika hadithi hii kuna hoja kwa wanazuoni wa madhehebu ya Imamu Shafii yakwamba uimamu wa mtoto anaepambanua katika swala ya faradhi".
Na anasema Sheikh Ibnu Baaz Mungu amrehemu:
"Hakuna tatizo kwa mtoto kua imamu ikiwa amefikisha miaka saba au zaidi na anajua kuswali vizuri kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume ﷺ yanayoashiria hilo,lakini bora ni kumchagua mwenye kujua kusoma Qur'ani zaidi katika kundi na ikiwa katika kusoma wako sawa basi mwenye kujua Sunna zaidi,na ikiwa katika Sunna wako sawa basi alietangulia kuhama,na ikiwa katika kuhama wako sawa basi mwenye umri zaidi kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume ﷺ.
Angalia [Majmu'ul fataawa ibnu baaz] Juzuu ya 30 ukurasa wa 166.
Na anasema Sheikh Ibnu Uthymeen Mungu amrehemu.
Unafaa uimamu wa mtoto kwa aliemzidi kiumri lakini ikiwa huyu aliemzidi kiumri amebalighi basi kauli mashhuri katika madhehebu yetu ni kwamba mtoto huyo hawezi kua imamu wake haswa katika swala ya faradhi lakini sahihi ni kwamba yafaa yeye kua imamu katika swala ya sunna na faradhi kama ilivyoashiria hadithi ya Amru bin salamah.
Angalia [Fataawa wa Rasaail ibnu uthymeen] 15/81.
Na ikiwa yafaa mtoto kua imamu katika swala ya faradhi na sunna ikiwa yuajua kuswali vizuri basi vile vile yuwafaa yeye kutoa khutba ya Ijumaa ikiwa anaweza kuitoa vizuri na kutekeleza nguzo zake, kwani sharti ya swala kama ilivyo ni nzito kuliko sharti ya khutba.
Na Allah ndie mjuzi zaidi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.