MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA UTUMWA (5)
MAMBO YA MSINGI KUYAFAHAMU NI:
Uislamu pekee ndio ulio punguza njia za kuwaingiza watu utumwani? Kwa kuandaa njia za kutoka utumwani na kubakisha njia moja tu ya kuingia watu utumwani, nayo ni vita.
Hata hivyo hii njia ya vita nayo ni kama sio njia ya kuingia utumwani kwa sababu ukilinganisha tukio la kumuuwa mateka na kutokumuwa, badala yake kumfanya mateka, hii ni kama kumwacha huru tu.
Uislamu umekuja hali ya kuwa utumwa upo na biashara za utumwa zilikuwepo. Uislamu ulipokuja haukukubaliana na kuendeleza utumwa bali ulikubaliana na jambo zima la kuukomesha utumwa usiwepo kwa watu, na ukaliunga mkono jambo hili la kuukomesha utumwa.
Swali: Ni nahi aliyefanya biashara ya kuuza watu na kuwafanya ni watumwa, ikiwa nyinyi waislamu mnasema kuwa uislamu umepinga vita utumwa na umekuja kuwa komboa watumwa?!
Jawabu: Waliofanya biashara ya kuwafanya watu watumwa na kuwauza ni haya mataifa yafuatayo:-
Taifa la Kwanza : BRITAINIA (Uingreza) : mfalme elizabeti wa kwanza wa nchi ya bur-tania alimiliki katika mwaka 1561 : pato kubwa la nchi kwa kufanya biashara ya watumwa katika nchi ya guiney na alikuwa mtumishi mkuu wa malikia alizabeti bwana (JOHN HAMUNIS) alikuwa akiwakusanya watumwa kutoka nchi ya (Qiney) na kuwapelekea BRITANA. Hadi ikapelekea katika wakati huo wa utawala wake mf. Malikia alizabeti wa kwanza BRITANA akawa ana mvutano mkubwa na Hispania kwa sababu nao wahispania walikuwa na biashara hiyo ya utumwa.
Taifa la pili : ISPANIA: Ulikuwa mji mkuu wa ISPANIA ISHBALIA: Katika zama hizo ndio ilikuwa ni soko kuu la kuingiza watumwa, na ndio kilikuwa kituo malumu kwa ajili ya watumwa. Na walipata fedha nyingi sana ambazo ziliingia katika benki yao ya ISPANA. Na hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1520 hadi 1530 na watumwa walichukuliwa kutoka katika makabila mawili: wahindi wekundu kutoka nchi ya Mexico, na kutoka AL-AKA kutoka katika Ardhi ya (AL-BIIRU.
Taifa la tatu: BURTUGHALIA: Ambao walikuja katika nchi ya KONGO wakiwa wameambatana na Mapadri wa kikristo, nao ni watu ambao waliofanya biashara ya utumwa kutoka KONGO kwenda BURTUGHALIA kwa kila wiki walitumwa watumwa wasiopungua 320 mpaka ikafikia idadi ya watumwa waliotumwa ndani ya mwaka mzima ni watumwa wasiopungua 25 elfu kila mwaka. Si hivyo tu bali hali ilizidi mpaka ikafikia watumwa wanaopelekwa huko kwa mwaka ni watumwa wasiopungua 75 elfu, na ilikuwa ni tukio la kipindi cha mwaka kuanzia 1570-1836, kiasi kwamba watumwa walio tumwa ndani ya miaka hiyo (1570-1836) ni watumwa waisopungua milioni nne.
Taifa la nne : WAFARANSA: Walianzisha shirika rasmi kwa ajili ya biashara ya utumwa wakipitia katika ufukwe wa Afrika magharibi kutoka katika nchi ya mor-tania na kuingia KONGO. Pia kituo kingine kilikuwepo katika Kisiwa cha JARIA kilichopo karibu na Mji Mkuu wa SENEGAL – RAKARI, na Kisiwa hicho ndio kilikuwa ni kituo kikuu cha kukusanyia watumwa na kulikuwa na jengo kubwa kabisa ambalo kuta zake zilikuwa na minyororo ya kufungia watumwa, walikuwa wanarundikwa ndani ya jingo hilo. Walifungwa humo bila ya huruma kabisa kama kuku kwenye tenga huku wamefungwa wote kwa minyororo miguuni na shingoni kama ng’ombe.
Taifa la tano; AMERIKA iliweka Wilaya ya Karolina katika nchi ya Amerika mwaka 1638 kanuni ya mwanzo kuhusu watumwa kwa kuwa walikuwa nao wakiwatumia watumwa katika kulima mashamba yao makuu ya mazao mbalimbali, hadi wakaweka kanuni isemayo: “Hakika mtumwa ni mtu asiekuwa na nafsi wala roho ya uhai, na ni mtu ambae hana akili wala werevu, Wala hana matashi ya kiutu, wala hana maamuzi ya kipekee, (yaani ni kama punda ambae haendi ila kwa mjeledi). Na hana uhai mwili mzima, bali upo tu katika mikono yake”.
Kanuni hii ya kinyama ilisainiwa na Mahakimu wakuu wa Nchi ya Marekani Mwaka 1867 na wakathibitisha kuwa inafaa kuwatenga na kutofaa kuamiliana nao kwa lolote. Kanuni hii iliendelea kufanyiwa kazi tokea Mwaka 1867 hadi kufikia Mwaka 1954.
Hivyo, ndiyo maana utaona baadhi ya wamagharibi wanatimua vumbi dhidi ya uislamu na waislamu kuhusu utumwa ili wafiche madhambi na manyanyaso yao waloyafanya dhidi ya waafrika, khasa katika kuwafanya watumwa .
Badala yake wanatuhumu waislamu na waarabu kuwa ndiyo walofanya bishara ya utumwa, hali ya kuwa wamagharibi ndiyo walokuwa wadau wakubwa wa biashara ya utumwa, kwa kuteka waafrika kwa wingi na kuwauza au kuwatumikisha katika mashamba yao.
Kulingana na historia hii inatupasa tuelewe kuwa babu zetu Waafrika waliuzwa kama mbuzi kupitia mataifa haya tuliyo yataja, wala Waarabu hawakuhusika kabisa na biashara hiyo ya watumwa, ispokuwa nadra sana, kama nchi ya omani iliwahi kuwa wakala wa kuchukua watumwa na kuwapeleka ulaya8, na hadi sasa ukienda katika baadhi ya nchi tulizozitaja wameziacha sehemu hizo kama majengo ya makumbusho.
Kwa sababu ya uharibifu walioufanya mataifa ya magharibi kutoka katika makoloni yao basi kwa zama zetu hizi ndizo wanapotaka kujionyesha kwamba wao ni wema, na wamewapakazia waislam na waarabu kuwa ndio waliokuwa wanafanya biashara ya kuuza watu wa Afrika, ingawa historia inapingana na madai yao.
Wanafanya hivyo kwa kuyaambia mataifa kwamba uislamu na waarabu ndio chanzo cha utumwa duniani kumbe ukweli hauko hivyo bali wao ndio walio watesa Waafrika katika mashamba yao na mpaka sasa bado katika mataifa yao kuna watu weusi kama vile Wamarekani weusi na nchi nyinginezo pia za Ulaya.
Hasa tunasema kuwaambia watu wa magharibi kuwa oneni haya historia ya kweli inawasuta na historia ipo na imeandikwa.
Wallah aalam.
MAKALA YAENDELEA
IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL
TAFSIRI:
BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.